Jeshi la Mgambo
Jeshi la Mgambo Mkoani limeendelea kuimarishwa na kuboreshwa kwa kutoa mafunzo kwa wananchi wake . Lengo ni kutoa mafunzo kwa wanamgambo 600 kila mwaka utekelezaji ni kama ifuatavyo;-
S/N |
Mwaka |
Lengo |
Utekelezaji |
Ongezeko/Pungufu |
1. |
2010/11
|
600 |
690 |
90 |
2. |
2011/12
|
600 |
616 |
16 |
3. |
2012/13
|
600 |
492 |
-108 |
4. |
2013/14
|
600 |
531 |
-69 |
5 |
2014/15
|
600 |
640 |
40 |
Wanamgambo wanashirikiana vyema na vyombo vingine vya Usalama katika kudumisha amani na utulivu Mkoani. Aidha dhana ya ulinzi shirikishi jamii imesaidia sana katika kuboresha ulinzi.
Mapambano dhidi ya Rushwa
Mkoa umeendelea kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita na kukemea vitendo vya RUSHWA kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Jamii imeendelea kuhamasishwa na kuelimishwa juu ya athari za rushwa na madhara yake katika jamii na Taifa zima kwa ujumla.
Mwenge wa Uhuru
Katika kipindi chote nilipokuwa hapa, Mwenge wa Uhuru ulikuwa ukipita na kukimbizwa Mkoani kwa mafanikio makubwa ikiwa pamoja na kufikisha jumbe mbalimbali za Mwenge wa Uhuru. Mwenge kila unapokimbizwa umeweza kusaidia kuendeleza umoja na mshikamano wa wananchi kwani wamekuwa washiriki pamoja bila kujali itikadi zao za kisiasa, kidini, hali zao n.k. Mwenge pia umekuwa ni kichocheo cha kuwezesha miradi ya maendeleo kutekelezwa haraka, kutoa elimu na ujumbe maalumu kwa wananchi kote ulikopita. Taarifa ya mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2012 inaonesha kuwa, Mkoa ulishika nafasi ya kumi ( 10 ) kitaifa na mwaka 2013 ulishika nafasi ya Nne ( 4 ) kitaifa kati ya Mikoa 30 iliyopo nchini. Kwa mwaka 2015 Mwenge wa Uhuru utapokelewa kutoka Mkoa wa Tanga na kukabidhiwa Mkoa wa Iringa.
Watumishi wa Mkoa
Mpaka tarehe 15 Desemba, 2014, idadi ya Watumishi wote katika Sekretarieti ya Mkoa na Serikali za Mitaa ni 18,725. Mchanganuo wa watumishi hawa ni kama ifuatavyo:
Idadi ya Watumishi katika Mkoa
Mkoa/Halmashauri |
Idadi ya Watumishi |
Asilimia
|
Mkoa
|
820 |
5 |
Manispaa
|
3,664 |
16 |
Morogoro DC
|
2,854 |
12 |
Mvomero
|
2,986 |
15 |
Kilosa
|
3,868 |
23 |
Kilombero
|
3,483 |
17 |
Ulanga
|
1,050 |
13 |
JUMLA |
18,725 |
100 |
Chanzo: Taarifa za Uhakiki wa Madai ya Watumishi ,2014
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.