ENEO LA MRADI
• Eneo la Mradi lipo katika Shamba namba 217 eneo Mkulazi - Ngerengere, Morogoro vijijini kilometa 153 kutoka Manispaa ya Mororgoro Mjini.
• Shamba hili lenye ukubwa wa hekta 63,227 sawa na ekari 156,237 linapakana na vijiji 5 ambavyo ni Usungura, Chanyumbu, Mkulazi, Kidunda na Kwaba ambapo wenyeji wake wanajishughulisha na kilimo na ufugaji.
TAARIFA YA MRADI WA SHAMBA NAMBA 217 MKULAZI
• Mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya Taifa ya serikali ya awamu ya tano ambayo ni ujenzi wa uchumi wa kati wa kilimo na viwanda.
• Pia mradi huu umeainishwa katika mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano ijayo
• Aidha ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la serikali kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kupanua wigo wa uwekezaji badala ya kujikita katika ujenzi wa majengo nk.
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.