Kazi kubwa ya Idara ya Mipangao na Uratibu ni kutoa huduma za kitaalamu katika nyanja za Mipango, Bajeti na vilevile kuratibu shughuli za Sekretarieti ya Mkoa katika kutoa uwezeshaji wa utaalamu kwa mamlaka za Serikali za Mitaa. Seksheni hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi anayewajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Sehemu ya Mipango na Uratibu
Kuratibu suala zima la maendeleo ya kiuchumi kwenye Mkoa ikijumuisha Sekta Binafsi, Mashirika ya serikali, Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na Asasi za kijamii.
Kushauri na kuratibu utekelezaji wa sera za sekta mbalimbali katika Mkoa
Kuratibu maandalizi, usimamizi na tathimini ya mipango (Mpango Mkakati, Mpango Kazi na Bajeti) kwa ajili ya Sekretarieti ya Mkoa
Kuratibu mikutano ya Kamati ya Ushauri ya Mkoa
Kuchambua, kuunganisha na Kusimamia maandalizi na utekelezaji wa Mpango wa Sekretarieti ya Mkoa na Bajeti
Kuratibu miradi inayofadhiliwa na wafadhili/wadau wa maendeleo na kushauri shughuli za utekelezaji wa Miradi.
Kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa kuhusu shughuli na majukumu ya mashirika, taasisi za kijamii na sekta binafsi
Kushauri na kuratibu shughuli za utafiti katika Mkoa
Kuratibu mazoezi ya sensa ya watu na makazi
Kuratibu shughuli zitokanazo na majanga katika Mkoa
Kuzisaidia na kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuandaa maandiko ya miradi
Kuratibu utekelezaji au ushughulikiaji wa masuala mtambuka ikijumuisha masuala ya Jinsia, Ulemavu, HIV/AIDS, na Kuwa mratibu au msimamizi wa masuala ya Jinsia katika Mkoa.
Kuratibu utekelezaji na kusimamia ushiriki wa sekta binafsi katika masuala mbalimbali ya maendeleo
Kusimamia na kutathimini utendaji wa Mamlaka za Seriklai za Mitaa katika Mkoa.