• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

WAZIRI Dr. ASHATU ATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO ILI KUJIINUA KIUCHUMI.

Posted on: May 15th, 2022

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dr. Ashatu Kijaji amewataka wananchi Mkoani Morogoro na watanzania wengine kwa ujumla kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na taasisi mbalimbali hapa nchini ili kujiinua kiuchumi na kuchangia pato la Taifa.



Waziri Kijaji ametoa kauli hiyo Mei 14 Mwaka huu katika hotuba yake wakati wa kufunga Maonesho ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi kiuchumi yaliyofanyika Kitaifa  uwanja wa Jamhuri Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mkoani humo.

Dr. Ashatu Kijaji amebainisha kuwa, Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi zinafanya jitihada kubwa ya kuanzisha Mifuko na Programu mbalimbali za kusaidia na kuwezesha wananchi kushiriki katika shughuli za kiuchumi lakini ushiriki wa wananchi wenyewe umekuwa si wa kuridhisha.




“Imetamkwa thamani mbalimbali za fedha ambazo tayari kupitia Programu hizi Serikali imeshatoa fedha kwa Wananchi aidha kupitia mikopo ya moja kwa moja au kupitia mipango mbalimbali ya kutengeneza miundombinu ya msingi kwa ajili ya shughuli zetu sisi wananchi za kiuchumi”. amesema Dkt. Kijaji


“Hatuna sababu ya kurudia lakini tujiulize kama wananchi tunatumiaje fursa hizo? Tupo tayari kuhakikisha na kuona kwamba tunanufaika na jitihada hizi ambazo Serikali yetu ya awamu ya sita imewekeza kwetu”. Amesisitiza Dr. Kijaji.

Katika hatua nyingine, Dr. Ashatu Kijaji amewsihi wananchi na wajasiriamali kuwa, kila mwananchi ajitahidi kwa makusudi na kuitumia vema mikopo kama njia ya kutekeleza shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kwa pamoja taifa litasonga mbele kimaendeleo endelevu.





Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akiwasilisha salamu za Mkoa ameweka wazi kuwa, kupitia vikao vya kiutendaji, Mkoa utatumia mikakati mbalimbali na kubainisha Mifuko na Programu za kuwasaidia wananchi kiuchumi kwa kuongeza uzalishaji hasa katika Sekta ya Kilimo na kukaribisha wawekezaji wa kada hiyo kwani ardhi ipo ya kutosha.



Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Baraza la Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa amesema tangu kuanzishwa kwake Baraza hilo lina jumla ya Mifuko na Programu 62, kati hiyo 52 inatoka Selrikalini na 10 katika Sekta binafsi, ambapo hadi sasa Mifuko hiyo imeshato Mikopo zaidi ya shilingi trilioni 5.38 kwa zaidi ya wajasiriamali zaidi ya Milioni 8 katika kuimarisha mzunguko wa uchumi.





Naye Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuchochea Kilimo Tanzania Bw. John Kyaruzi amebainisha kuwa Mfuko una lengo la kuwatatulia wakulima wadogo changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo changamoto ya kukidhi viwango vya soko, uhaba wa masoko ya bidhaa, miundombinu isiyo faaa kwa usafirishaji na Mabenki yasiyo na mikopo rafiki.



Changamoto nyingine ni maslahi kwa wakulima  na mikataba isiyofaa kwa wakulima hao hali inayopelekea wakulima kuendelea kuwa masikini kila kukicha hivyo taifa nzima kutokuwa endelevu.




MWISHO.




























 



















Matangazo

  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro April 13, 2023
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • MAONESHO YA NANENANE July 27, 2022
  • MJADALA WA KITAIFA WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA October 31, 2022
  • View All

Habari Mpya

  • KAZI YANGU YA KWANZA NI KUHAKIKISHA KUWA MOROGORO INAKUWA NA MISINGI YA AMANI - MHE. ADAM MALIMA, RC MORORORO

    May 27, 2023
  • RC Adam Malima aahidi kuifungua Wilaya ya Ulanga

    May 25, 2023
  • RC Adam Malima aahidi kuifungua Wilaya ya Ulanga

    May 25, 2023
  • RC MOROGORO AANZA KAZI RASMI, ATOA MAAGIZO.

    May 25, 2023
  • View All

Video

Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.