• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

WATOA HUDUMA ZA KISHERIA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA KAMPENI YA MAMA SAMIA LEGAL AID.

Posted on: December 12th, 2024


Watoa huduma za kisheria kwenye kampeni itakayozinduliwa kesho ya Mama Samia Legal AID wametakiwa kuzingatia miongozo ya utumiaji huduma, kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia ufanisi, weledi, usawa na bila upendeleo.

Wito huo umetolewa leo Disemba 12, 2024 na Katibu Tawala Msaidizi Section ya Miundombinu Mkoa wa Morogoro Mhandisi Ezron Kilamhama wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu hao kutoka kada mbalimbali katika kughulikia changamoto za kisheria kwa wananchi.

Akiongea katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro idha Mhandisi Kilamhama amesema ni jukumu la kila mtaalam kwenda kushughulikia changamoto za wananchi kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kusuluhisha migogoro mbalimbali na kutoa elimu juu ya sheria mbalimbali ili waweza kuondoa changamoto zinazowakabili.

".. Wananchi wengi wanahitaji sana hii huduma ambayo mnaenda kuifanya, isijitokeze miongoni mwetu tukaanza kutumia njia kinyume na sheria katika kutoa huduma hiyo."

Sambamba na hayo kiongozi huyo amesema, mafunzo hayo yanajumuisha wataalamu mbalimbali wakiwemo maafisa ardhi, wanasheria, maafisa maendeleo ya jamiii, na dawati la  jinsia kutoka jeshi la polisi, mawakili wa kujitegemea, na wasaidizi wa sheria, hivyo kupitia viongozi hao elimu na huduma zitatolewa kwa ufanisi mkubwa.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea  uelewa wa pamoja kuhusu msaada wa Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia "Mama Samia legal AID Campaign" pia kufahamu majukumu ya kila mmoja kuandaa utoaji huduma wa msaada wa kisheria ambapo kupitia mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao ya kikazi ipasavyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi amesema mafunzo hayo watakayoyapata wataalamu  hao yataenda kuwasaidia kutoa huduma ndani ya siku 9 kuanzia Disemba 14 hadi 22, 2024 katika Mkoa wa Morogoro ikiwezo kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.

Naye mwanasheria kutoka Halmadhauri ya Wilaya ya Ulanga Bw. Elikarim Samwel amesema mafunzo hayo aliyoyapata yataenda kumasaidia katika kutatua changamoto hususan migogoro ya wakulima na wafugaji na kusuluhisha migogoro ya mirathi katika familia.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA ATAKA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAFUGAJI

    May 15, 2025
  • Vyama vya Ushirika Vyatakiwa Kutumia TEHAMA

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI SHERIA, KATIBA NA KANUNI YA VYAMA VYENU - MUTUNGI.

    May 14, 2025
  • WANAFUNZI 214 WA KIDATO CHA KWANZA SEKONDARI ZA MONGOLA, MGETA WAPEWA MICHE 2140 YA MIKARAFUU

    May 13, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.