• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

SERIKALI KUJENGA MADARAJA YA CHAKWALE, NGUYAMI.

Posted on: February 23rd, 2024

SERIKALI KUJENGA MADARAJA YA CHAKWALE, NGUYAMI

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema iko katika hatua za mwisho kuanza kujenga madaraja mawili ya Chakwale na Nguyami Wilayani Gairo ili kuwaondolea kero ya muda mrefu wananchi wa maeneo hayo.

Hayo yamebainishwa Februari 22 na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa wakati wa ziara yake ya siku Nne Mkoani Morogoro ya kukagua miundombinu ya Barabara ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumtaka Waziri huyo kufika kusiko fikika ili kutatua kero za wananchi hususan miundombinu ya Barabara.

Akiwa Wilayani Gairo amewaambia wananchi kuwa Serikali chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan imekwisha ridhia ujenzi wa madaraja hayo mawili ya Chakwale na Nguyami ambao ujenzi wake unatarajiwa kuanza Juni 2024, Daraja la Chakwale likiwa na urefua wa mita 80 na lile la Nguyami likiwa na urefu wa mita 100, lengo ni kuwaondolea wananchi kero ya kupoteza Maisha wa eneo hilo na mali zao.

Aidha, Waziri Bashungwa amemuagiza Mtendaji wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROAD), kufanya usanifu wa kina wa madaraja hayo ili yawe ya viwango na yaje kutumika pia wakati watakapoamua kujenga Barabara hiyo kwa kiwango cha lami.


Akiwa Wilayani Kilosa Waziri Bashungwa amemtaka mkandarasi anayejenga Barabara ya kutoka Rudewa  hadi Kilosa mjini kwa Kiwango cha lami kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha Barabara hiyo ifikapo Aprili 22 mwaka huu kwa kuwa hana kisingizio tena kwani fedha alizokuwa anazidai shilingi Bilioni 4 amekwisha lipwa.

Mbunge wa Jimbo la Gairo Mhe. Ahamed Shabiby ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kujali wananchi katika kuwaletea maendeleo yao kwa sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Miundombinu na kuweka bayana kuwa hakuna Serikali iliyotoa fedha nyingi kwa Sekta ya Miundombinu kama Serikali ya awamu ya sita.


Akimkaribisha Waziri Bashungwa kuongea na wananchi wa maeneo ya Chakwale, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema Wilaya ya Gairo ndiyo Wilaya maskini kuliko zote Mkoani humo, hata hivyo amesema endapo Barabara za kutoka Gairo Kwenda Kilindi Mkoani Tanga na Barabara ya kutoka Mjini Gairo Kwenda Nongwe zitaboreshwa, Wilaya hiyo ndiyo yenye Uchumi mkubwa kupita Wilaya nyingine.

MWISHO.

Kwa upande wao wananchi wa Kata ya chakwale akiwemo Robert John na Simon John, wameiomba Serikali iwajengee  madaraja hayo kwa kuwa yamepoteza Maisha ya watu wengi kuchukuliwa na maji Pamoja na mali zao na kwamba Barabara hiyo ndiyo Barabara inayotumika Kwenda Makao makuu ya Wilaya ya Gairo na Hospitali ya Wilaya hiyo.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA ATAKA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAFUGAJI

    May 15, 2025
  • Vyama vya Ushirika Vyatakiwa Kutumia TEHAMA

    May 14, 2025
  • ZINGATIENI SHERIA, KATIBA NA KANUNI YA VYAMA VYENU - MUTUNGI.

    May 14, 2025
  • WANAFUNZI 214 WA KIDATO CHA KWANZA SEKONDARI ZA MONGOLA, MGETA WAPEWA MICHE 2140 YA MIKARAFUU

    May 13, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.