• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RAS MOROGORO AAGIZA USHIRIKIANO KWA WATAALAM WA KILIMO, AFYA, WALIMU KUIMARISHA LISHE MASHULENI

Posted on: October 25th, 2024

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa amewaagiza wataalamu wa kilimo, afya na walimu wa shule za msingi na sekondari kushirikiana vema katika maeneo yao ili kuwa na mpango utakaozisaidia shule kupata vyakula vya kuwalisha wanafunzi wa madarasa yote ili kujenga afya na kuongeza umakini darasani.

Dkt. Mussa ametoa agizo hilo Oktoba 25, Mwaka huu wakati wa mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea shule za Msingi na Sekondari zilizopo Mkoani humo  akitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga lengo likiwa ni kuangalia hali ya lishe mashuleni.

Akifafanua zaidi, Dkt. Mussa amesema shule nyingi zina maeneo makubwa ambayo wanaweza kushirikiana na maafisa kilimo kulima mazao mbadala ya kimkakati hususan michikichi, kokoa na mikarafuu na kubainisha kuwa miche ya mikarafuu 40 inaweza kuleta faida ya shilingi milioni 9  ndani ya miaka minne, hivyo shule inaweza kujiendesha yenyewe na kutoa chakula kwa wanafunzi bila ya usaidizi kutoka kwa wazazi.

"... suala la lishe ni la wote ninyi watu wa kilimo, walimu, watu wa afya na wengine wengi lazima tuungane pamoja ili tuweze kufikia lengo..." Ameagiza Dkt. Mussa Ali Mussa

Aidha, Dkt. Mussa amekemea vikali wanafunzi kula chakula cha aina moja hususan makande na ugali bila mboga mboga wala matunda kwani amesema chakula cha aina moja  hudumaza afya ya akili na mwili kudhoofika.

Sambamba na hayo, Katibu Tawala huyo wa Mkoa amezipongeza Shule za Sekondari za Celina Kombani na Msogezi kwa kuanzisha mpango mkakati wa wanafunzi wa vidato vyote waliopo shuleni kupata chakula chenye lishe bora na kutaka shule hizo kuwa mfano ili shule zingine kwenda kujifunza.

Kwa sababu hiyo, Dkt. Mussa amempandisha cheo aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Msogezi Mwl. Zena Idd Salum kwa kutafuta ufumbuzi wa wanafunzi wa madarasa yote kula mlo kamili kwa kulima mazao ya asili ikiwemo mihogo na mbaazi kwa ajili ya wanafunzi kula shuleni.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Best Richard Magoma amefurahishwa na utendaji kazi wa aliyekuwa Kaimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Msogezi na kuwataka walimu wakuu kuwa mfano katika uchangiaji wa chakula na kutawajenga wanafunzi kuwa na ushirikiano wa kula chakula kwa pamoja kuepuka vyakula vya kununua migahawani.

Naye, Afisa lishe wa Mkoa wa Morogoro Bi. Salome Magembe amesema shule zinapaswa kuanzisga vitalo vya kulima mboga mboga pamoja na kulima mazao jamii ya mikunde na mbaazi na kutoa vyakula vya aina nyingi hususan vinavyozingatia lishe bora kama wanga, protini na vitamini ili kupata wanafunzi mahiri ambao ndio wataalamu wa Taifa la kesho.


Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • Zaidi ya Mil. 125 zachangwa kupitia chakula cha hisani kukarabati Hospitali ya Rufaa Morogoro.

    May 18, 2025
  • RC MALIMA ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI, ASEMA HOSPITALI YA RUFAA INAHIMILI WAGONJWA.

    May 17, 2025
  • VYAMA VYA SIASA NCHINI VYATAHADHARISHWA

    May 15, 2025
  • RC MALIMA ATAKA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAFUGAJI

    May 15, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.