Mikakati ya Mkoa wa Morogoro
Mkoa kwa upande wake umeendelea kutoa kipaumbele katika suala la upangaji mipango ya matumizi bora ya ardhi ambapo mpaka sasa jumla ya vijiji 276 kati ya vijiji 659 vina mpango wa matumizi bora ya ardhi na zoezi bado linaendelea katika wilaya ya Mvomero.
Aidha, programu mpya ya kitaifa ya kupima maeneo ilizinduliwa rasmi tarehe 18/2/2016 ambapo wilaya za Ulanga,Malinyi na Kilombero zinahusika kama maeneo ya kuanzia. MIKAKATI YA MKOA
Kuimarisha usimamizi wa makusanyo ya fedha katika vituo na kuhakikisha halmashauri zinahakikisha watu wote wenye Bima/CHF hata wa makundi maalum wanatumia kadi zao.Pia kufunga mifumo ya ki electronic kwa ajili ya kukusanyia mapato.Hii itasaidia kuboresha upatikanaji wa dawa na kutatua kero mbalimbali ikiwemo madeni/stahili za watumishi.
Kuboresha uhamasishaji, uchangiaji, upatikanaji wa fedha za tele kwa tele na matumizi ya fedha za uchangiaji wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii.
Kusimamia na kuhakikisha vituo vyote vinafikia nyota tatu ili viweze kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Kuhakikisha kuwa dawa na vifaa tiba zinakuwepo vituoni na kuhimiza Halmashauri pale dawa zinapokosekana katika Kitengo Taifa cha kuhifadhi dawa (MSD) basi dawa hizo zinanunuliwa kwa Mzabuni (Prime Vendor) aliyeteuliwa na Mkoa kwa kufuata taratibu za manunuzi.
Kuzisimamia Halmashauri pamoja na Hospitali za rufaa ili kuhakikisha wametenga fedha za kutosha kwa ajili ya kukarabati majengo,vifaa tiba na magari.
Kuzisimamia halmashauri ili kutenga bajeti kwa ajili ya kuratibu na kuelimisha jamii jinsi ya kuwahudumia na kuwatambua watoto walio katika mazingira hatarishi, wazee na watu wenye ulemavu.
Kushirikiana na wadau mbalimbali ndani na nje ya Mkoa ili kusaidia kutatua baadhi ya changamoto.
Kuimarisha upatikanaji wa watumishi wa afya
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.