Ugatuaji Madaraka
Kipindi cha 2008 hadi 2014 ni cha utekelezaji wa dhana ya Ugatuaji na Upelekaji wa Madaraka kwa Umma ambapo hadi sasa sekretarieti za Mikoa zimekabidhiwa majukumu yaliyokuwa yakitekelezwa na Kanda za Maboresho.
Majukumu hayo matatu (3) ni yafuatayo:-
Kutunga na kusimamia sheria ndogo ili kudhibiti uvunjaji wa sheria.
Halmashauri zote na Sekretarieti ya Mkoa zimeanzisha Ofisi za kushughulikia malalamiko na kero za wananchi. Rejesta na masanduku ya maoni yamewekwa katika sehemu zote za huduma. Aidha, Ofisi zote za Tarafa, Kata na Serikali za Vijiji zinapokea malalamiko na kero za wananchi na kuzifuatilia.
Kuwashirikisha wananchi katika kupanga mipango ya bajeti kwa kutumia mfumo wa fursa na vikwazo vya maendeleo (O & OD).
Taarifa zote za Halmashauri zinazohusu mapato na matumizi, zabuni na taarifa za miradi ya maendeleo zimetangazwa kwenye magazeti na kubandikwa katika mbao za matangazo ili kukuza dhana ya uwazi na uwajibikaji kwa wananchi na wadau wengine.
Halmashauri na Mkoa zimezingatia masuala ya jinsia katika ajira na shughuli mbalimbali za kiutumishi.
Halmashauri na Mkoa zimeunda Kamati za Kisheria na kuendesha vikao vya kamati husika kwa mujibu wa sheria na miongozo iliyopo.
Halmashauri zote ndani ya Mkoa zimeendelea kuendesha vikao vya Serikali za Vijiji/Mitaa na mikutano ya wananchi ili kutoa fursa kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika shughuli za utawala na uendeshaji wa mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo yao.
Mkoa wa Morogoro tayari umeunda kamati ya Ushauri ngazi ya Mkoa (RCC) na Wilaya (DCC) na kufanya vikao kila mwaka.
Matokeo ya mikakati hiyo imepelekea Makusanyo ya ndani ya Halmashauri kuongezeka kutoka sh.1,513,529,439.89 mwaka 2005 hadi kufikia sh.12,938,688,999.19 mwaka 2014. Kiasi hiki ni sawa na ongezeko la asilimia .88.30
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.