• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Huduma za maji

                                                                     SEKTA YA MAJI

TAARIFA YA MIRADI YA MAJI MKOA WA MOROGORO 

 

Hali ya Huduma ya Maji Vijijini

Hadi kufikia mwezi Januari, 2019 asilimia 68.87 ya wakazi waishio Vijijini katika Mkoa wa Morogoro wanapata huduma ya majisafi na salama kupitia miradi ya maji iliyopo, ambapo utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji nchini umewezesha ujenzi  wa jumla ya miradi 69 katika vijiji 95. Miradi 52 katika vijiji 68  imekamilika na miradi 17 katika vijiji 27 utekelezaji wake unaendelea katika Halmashauri za Morogoro Manispaa (1), Malinyi (1), Kilosa (1), Mvomero (6), Ulanga (1), Morogoro Vijijini (2), Ifakara (2), na Gairo (3).

Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika kila Wilaya kwa maeneo ya vijijini ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali Na. 1.

Jedwali Na. 1: Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Vijijini katika kila Wilaya

LGA 
Idadi ya watu   (2018)
Idadi ya vituo vya maji
Idadi ya vituo Vinavyotoa huduma
Idadi ya vituo Visivyotoa huduma
Idadi ya watu wanaopata huduma ya Maji
Asilimia ya watu wanaonufaika na huduma
Morgoro Dc

303,922

1222

 828

           394

      207,183

68.17

Kilombero DC

321,029

1686

1,087

              599

261,285

81.39

Ifakara TC

 85,357

567

         380

               187

62,165

72.83

Morogoro MC

       59,985

409

372

                37

49,950

83.27

Mvomero DC

333,012

1310

802

              508

        223,118

67.00

Kilosa DC

467,392

1758

1083

               675

314,750

67.34

Ulanga DC

151,790

774

     519

        255

        106,850

70.39

Gairo DC

199,045

406

           355

          51

           99,641

50.06

Malinyi DC

110,397

668

        303

      365

          74,495

67.48

 Jumla
  2,031,928 
          8,800 
            5,729 
            3,071 
      1,399,437 
                   68.87 

Ujenzi wa Miradi Mingine ya Maji Vijijini

Miradi inayotekelezwa kupitia Halmashauri na Wadau wengine wa Maendeleo

Katika mwaka 2018/2019, Serikali ya Mkoa imepanga kuendelea  na juhudi nyingine mbalimbali za ujenzi wa miradi ya maji vijijini. Juhudi hizo ni zile zinazofanyika kupitia vyanzo mbalimbali vya fedha. Vyanzo hivyo ni pamoja na Halmashauri, Ruzuku ya Serikali kuu na Wadau mbalimbali waliopo katika Mkoa wetu na hata wa nje ya Mkoa. Juhudi hizo zinachangia katika kuinua kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji. Jedwali Na. 4 linaonesha miradi ya maji itakayojengwa kwa kutumia vyanzo vya mapato vya Halmashauri na taasisi mbalimbali katika Mkoa.

Jedwali Na. 4: Miradi inayotekelezwa na Halmashauri pamoja na taasisi mbalimbali mwaka 2018/2019.

Wilaya
Taasisi/ chanzo cha mapato
Idadi ya Miradi
Asilimia za Utekelezaji
Idadi ya Vijiji vitakavyohudumiwa
Gairo
Lion Pures Water

1

Madege- Nhorongo- Sanganjeru- Chakwale- Kimashale- Kilimani (100%)

6

Kilombero
WARIDI

3

Kidatu A- Kidatu B- Chikago-Kidatu Kati- Mkamba (100%), Mwaya- Mgudeni- Kiswanya (97%), Kiberege-Mkasu-Bwawani- Nyamwezi- Kanolo (95%)

14

Kilosa
WARIDI, WORLD VISION

4

Msowero (88%), Kimamba A (100%), Kimamba B (100%), Nyameni-Kibaoni-Mbuyuni (33%)

6

Mvomero
WARIDI

3

Hembeti-Dihombo-Msufini (100%)
Kibaoni- Melela- Mlandizi (100%)

9

SAFINA WOMEN'S ASSOCIATION (SAWA)
Doma-Mtupule-Msongozi (100%)
Ulanga
CARTAS -Mahenge

1

Namgezi - Mbangayao - Isaka (100%)

3

Ifakara TC
Help for Undersaved Community (HUC) & Own source

1

Kata zote za Ifakara (48%)

Jumla

13

 

 

Kukamilika kwa miradi inayotekelezwa kupitia Program ya Maji pamoja na ile ya Wadau wengine wa mMaendeleo katika mwaka wa fedha 2018/2019 kumeongeza upatikaji wa huduma ya maji safi na salama vijiji kutoka asilimia 68.49 mwezi Juni, 2018 hadi kufikia asilimia 68.87 Januari, 2019.

Fedha za utekelezaji wa Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini 

Upungufu wa wahandisi na mafundi sanifu kwa ajili ya usanifu, usimamizi na uendeshaji wa miradi. Mkoa una wahandisi 14, mahitaji halisi ni wahandisi 35, upungufu wa wahandisi 21. Mkoa una mafundi sanifu 24, mahitaji 74 na upungufu wa mafundi sanifu 50.

 Ufanisi mdogo wa vyombo vya watumia maji na hivyo kuathiri uendelevu wa miradi ya maji vijijini

Baadhi ya taasisi za serikali kutolipa gharama za maji kwa wakati hivyo kufanya Vyombo vya Watumia maji kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na upungufu wa mapato kulinganisha na gharama za uendeshaji wa mradi.

Uchafuzi wa vyanzo vya maji unaofanywa na wakulima na wafugaji kwenye vyanzo vya maji na kusababisha magonjwa ya mlipuko.

Wizara kuchelewesha malipo ya hati za wakandarasi

5.0       MIKAKATI YA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA MAJI MKOANI

 

Kufanya utafiti wa vyanzo vipya vya maji na kuhamasisha uvunaji wa maji ya mvua na ujenzi wa mabwawa madogo.

Kushirikisha taasisi za dini na sekta binafsi katika utoaji wa huduma ya maji – kuunga mkono nguvu za Serikali katika kukabiliana na uhaba mkubwa wa huduma za maji uliopo hususani maeneo ya vijijini.

Kuweka ulinganifu/ usawa wa rasilimali watu kwa kuwahamisha kutoka maeneo yenye unafuu kwenda penye upungufu mkubwa zaidi ndani ya Mkoa na kuendelea kuomba vibali vya kuajiri watumishi wapya toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Mpango wa kuvijengea uwezo vyombo vya watumia maji (COWSO’s) kwa kushirikiana na halmashauri kwa kufanya mafunzo na kuvipatia vitendea kazi ili kuboresha utendaji kazi wao.

Mkoa kwa kushirikiana na ofisi za Maji umechukua hatua mbalimbali za utunzaji wa rasilimali maji kwa kuzuia shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji pamoja na kusimamia sheria za utunzaji rasilimali maji. Moja ya shughuli hizo ni kuondoa mifugo kwenye vyanzo vya maji katika milima ya Uluguru kwenye Bonde la Wami/Ruvu.

Kuhimiza upandaji miti na utunzaji wa vyanzo vya maji kupitia kamati za Usafi wa Mazingira zilizopo vijijini.



Jedwali Na. 3:      Jedwali linaloonesha Utekelezaji wa Miradi ya Maji kwa kila Halmashauri 2018/19

 

Na
Halmashauri
Jina la Mradi

Idadi ya Watu wanaonufaika

Idadi ya Vituo

Kazi zilizopangwa kufanyika

Kazi zilizofanyika

Asilimia ya Utekelezaji

Mkandarsi
Gharama ya mradi
changamoto

1

Malinyi
Mradi wa maji Malinyi, Kipingo na Makerere

18,000

47

Ujenzi wa chanzo, bomba kuu 26km, bomba la usambazaji 14km, tanki lenye ujazo wa 150m3, vituo vya maji 47, ujenzi wa ofisi, mataki manne ya uvunaji maji ya mvua
Ujenzi wa chanzo, vituo 47 na ofisi, bomba kuu 24km, bomba za usambazaji maji 13km, matanki ya uvunaji maji yamekamilika, ujenzi wa tanki 150m3 kwenye riser ya 12m

91

Audacia Investment
            3,006,768,441.00
Mradi huu umechukua muda mrefu kukamilika kutokana na usanifu uliokosewa na Mtaalam Mshauri wa mradi Inter Consult.

2

Kilosa
Ujenzi wa miundombinu ya maji katika Kijiji cha Mabwegere.

3,000

12

Uchimbaji visima 2, Kujenga vituo vya maji 6, kujenga nyumba ya mashine, kuchimba mtaro wa maji na kulaza mabomba, ufungaji wa pampu ya kusukuma maji kutoka kisimani hadi tanki la maji
Ujenzi wa miundombinu ya maji umefanyika, uchimbaji wa visima 2umefanyika bado ufungaji wa pump na jenereta

85

Sepro Engineering and General Traders
                 183,097,000.00

3

Morogoro Vijijini
Mradi wa Maji Kifindike

2,179

10

Ujenzi wa banio/chanzo, Ujenzi wa mitambo ya kutibu maji, Ujenzi wa tanki la ujazo wa mita75, vituo vya kuchotea maji 10, matanki ya kuvunia mvua ya ujazo wa 1m,3m na 5m, ulazaji wa mabomba ya usambazaji na laini kuu
Ujenzi wa chazo na vituo, tanki na ulazaji wa bomba umekamilika

80

Jemason Investment Co. Ltd
                 412,779,100.00
Mlolongo mrefu wa malipo ya mkandarasi

4

Morogoro Vijijini
Mradi wa Maji Gwata

2,343

11

Ujenzi wa pump house, Ujenzi wa matanki 2 ujazo mita25 &50, vituo vya kuchotea maji11, tanki la kuvunia maji ya  mvua ya ujazo wa 1m,3m na 5m, ulazaji wa mabomba ya usambazaji 7,648m na laini kuu  6,346m , na kufundisha mafundi 2 kufunga pump 1 ya kusukuma maji
Ujenzi wa matanki 2, ulazaji wa mabomba ya usambazaji 7,648m na ujenzi wa vituo 11. Bado ujenzi wa swamp tank na bomba kuu ambavyo vitajengwa kutoka kwenye mradi wa maji Chalinze

75

Kumba Quality Contractors
                 440,600,000.00
Mradi huu unategemea maji kutoka mradi wa maji wa chalinze ambao haujakamilika.

5

Ifakara
Kibaoni

3,215

10

Uchimbaji na ulazaji mabomba yenye urefu wa 8,100, Ujenzi wa nyumba ya mashine ya kusukuma maji, ununuzi na ufungaji wa pump
Ujenzi wa nyumba ya mashine ya kusukuma maji, uchimbaji mitaro 7.4km

60

ELEISA Co. Ltd
242,667,590

6

Ifakara
Mahutanga

4,720

20

Ukarabati wa nyumba ya mashine ya kusukuma maji, Uchimbaji na ulazaji mabomba yenye urefu wa 15,000m, ujenzi wa vituo 10
Ukarabati wa nyumba ya mashine ya kusukuma maji unaendelea, ulazaji mabomba yenye urefu wa 15km, ujenzi wa vituo 10

85

Sepro Engineering Co. Ltd
393,508,000

7

Ulanga
Ukarabati wa Mradi wa maji Mgolo na RUMWAMCHILI

19,500

78

ukarabati wa kufunga mabomba  6'' GS 240m, PVC  6'' 200m, HDPE 2'' 200m, PVC  4'' 3060m,
Uchimbaji na ulazaji mabomba umbali wa 3,600m

71

Bayona Cons
199,783,400.00

8

Mvomero
Ukarabati wa Mradi wa Maji kijiji cha Lukenge

2,227

13

Uchimbaji wa kisima,  Ulazaji wa bomba, Ujenzi wa Vituo 2 vya kutolea huduma ya Maji,Ukarabati wa vituo 11 vya kutolea huduma kwa binadamu, ukarabati wa birika la kuhifadhi maji la lita 50,000, Ujenzi wa mnara wa kuhifadhi  tenki la Plastik la lita 5,000
Ulazaji wa bomba za usambazaji, Ujenzi wa Vituo 2 na ukarabati wa vituo 11 vya kutolea huduma, ukarabati tanki, uchimbaji wa kisima.  Ufungaji wa pump

95

Mradi huu unasubiri kibali kutoka Wizara ya Maji kwa ajili ya kutangaza zabuni.
NA
Maji yaliyopatikana katika chanzo cha kisima cha awali hayakufaa kwa matumizi ya binadam hivyo kisima kingine kimechimbwa.

9

Mvomero
Ujenzi wa Mrad wa Maji Kijiji cha Dihinda

12,265

21

Kujenga nyumba ya mtambo wa kusukuma maji, Kufanya Pump Testing ili kubaini uwezo wa kisima, Kununua na kufunga Nishati ya jua, Kununua na kufunga Pampu, ,  Kujenga Matenki mawili ya kuhifadhi maji yenye uwezo wa  lita 90,000, Kujenga laini mpya ya mabomba ya urefu wa 12.65km, Kujenga vituo 21 vya kutolea huduma ya maji kwa binadamu
Uchimbaji mtaro na ulazaji bomba umefanyika 95%, ujenzi wa tanki 225m3 umefanyika kwa 75%, ujenzi wa pump house 75%, ujenzi wa vituo 30%

70

Chakwale Company Ltd
603,433,119.26

10

Mvomero
Ujenzi wa Mrad wa Maji Kijiji cha Masimba

4,662

15

Kujenga nyumba ya mtambo wa kusukuma maji, Kufanya Pump Testing ili kubaini uwezo wa kisima, Kununua na kufunga Nishati ya jua, Kununua na kufunga Pampu, ,  Kujenga tenkii la kuhifadhi maji lenye uwezo wa  lita 90,000, Kujenga laini mpya ya mabomba ya urefu wa 4.07km, Kujenga vituo 15 vya kutolea huduma ya maji kwa binadamu
Ujenzi wa nyumba ya mtambo umefikia 60%, ujenzi wa tenki 75%, uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa bomba umefikia 80%, ujenzi wa vituo umefikia 80%.

80

Macea Construction Ltd
      432,585,382.08

11

Mvomero
Ujenzi wa Mrad wa Maji Kijiji cha Lubungo

8,000

16

Ujenzi wa nyumba ya mtambo wa kusukumia maji, kununua na kufunga pampu inayotumia nishati ya jua, uchimbaji, ulazaji na ufukiaji wa bomba, Ujenzi wa tenki la 90m3, Ujenzi wa vituo 16.
Ununuzi wa mabomba

15

Chakwale Co. Ltd
430,104,045.60

12

Mvomero
Ujenzi wa Mrad wa Maji Kijiji cha Vianzi

4000

8

Ujenzi wa nyumba ya mtambo wa kusukumia maji, kununua na kufunga pampu inayotumia nishati ya jua, uchimbaji, ulazaji na ufukiaji wa bomba, Ujenzi wa tenki la 45m3, Ujenzi wa vituo 8.
Uchimbaji na ulazaji mabomba 10.8km, Kupima wingi wa maji kwenye kisima

20

 EKA Investiment Co. Ltd
336,059,209.20

13

Mvomero
Ujenzi wa Mrad wa Maji Kijiji cha Kihondo

5000

10

Ujenzi wa nyumba ya mtambo wa kusukumia maji, kununua na kufunga pampu inayotumia nishati ya jua, uchimbaji, ulazaji na ufukiaji wa bomba, Ujenzi wa tenki la 90m3, Ujenzi wa vituo 10.
Ujenzi wa nyumba ya mashine ya kusukuma maji 60%, ujenzi wa tank 45%, kupima wingi wa maji

30

MACEA Construction Ltd
251,503,725.00

14

Gairo
Mradi wa Maji kisima kirefu wa Italagwe

9500

19

Ujenzi wa tank, ujenzi wa vituo 19, uchimbaji na ulazaji mabomba, ujenzi wa pump house na ufungaji ya jenereta
Ujenzi wa vituo (95%), ujenzi wa nyumba ya mtambo wa kusukumia maji, ujenzi wa tanki 30%, uchimbaji, ulazaji na ufukiaji bomba kuu 1960m, bomba za usambazaji 21,450m.

70

Saxon Company Ltd
933,059,771.60

15

Gairo
Mradi wa Maji kisima kirefu wa Chiwaga - Makuyu

5000

10

Ujenzi wa tank, ujenzi wa vituo 10, uchimbaji na ulazaji mabomba, ujenzi wa pump house na ufungaji ya jenereta
Uchimbaji na ulazaji bomba urefu 4000m, ufyatuaji wa tofali za kujenga tenki

35

Chakwale Company Ltd
745,530,692.02

16

Gairo
Mradi wa Maji kisima kirefu wa Chogoali

4500

9

Ujenzi wa tank, ujenzi wa vituo 9, uchimbaji na ulazaji mabomba, ujenzi wa pump house na ufungaji ya jenereta
Uchimbaji mitaro na ulazaji bomba kuu na usambazji 5,300m.

30

Iwawa Civil & Building Works Co. Ltd
551,011,384.00

17

Morogoro MC
Mradi wa Maji Mserereko wa Mundu na Kilala

                5,080

14

Ujenzi wa tanki la maji mita za ujazo 100, utandazaji wa mabomba 11,057m, ujenzi wa vituo 14 vya maji, ujenzi wa banio la maji
Uchimbaji, ulazaji na ufukiaji wa bomba 80%, ujenzi wa tenki 30, ujenzi wa vituo 50%

40

Iwawa Civil & Building Works Co. Ltd
496,967,856.00

Utafutaji wa vyanzo vya Maji (Uchimbaji Visima Virefu) kwa kila Halmashauri 2018/19

Na
Halmashauri
Jina la Mradi

Idadi ya Watu wanaonufaika

Idadi ya Vituo

Kazi zilizopangwa kufanyika

Kazi zilizofanyika

Asilimia ya Utekelezaji

Mkandarsi
Gharama ya mradi
changamoto

1

Malinyi
Mradi wa utafiti na uchimbaji visima 20

8,000


Utafiti na uchimbaji visima 20 (Kalengakero, Usungule, Kipenyo, Mtimbira, Sofi, Lumbanga, Kiswago, Madibira)
Utafiti umefanyika, visima 20 vimechimbwa kati ya vivyo 14 vina maji ya kutosha, 4 maji kidogo, vingine vilikosa maji

90

Victoria borehole drilling Ltd
                 538,990,000.00
Kazi inaendelea.
Mlolongo mrefu wa malipo kwa wakandarasi.

2

Ulanga
Uchimbaji wa visima 27 katika vijiji 27

6,075


Utafiti na uchimbaji visima 27 (Igumbiro, Ruaha, Chirombola, Mwaya, Mzerezi, Uponera, Nkongo, Chikuti, Mavimba, Mahenge, Mawasiliano, Isongo, Uponera, Msogezi, Vigoi, Nawenge, Mwaya, Mbuga, Ilonga, Ketaketa, Lukande, Euga, Sali, Lupiro, Iragua na Milola)
Utafiti umefanyika, visima 27 vimeshachimbwa 24 vina maji ya kutosha

95

PNR Cons
807,140,650.00

3

Kilombero
Uchimbaji visima virefu vijiji vya Kalengakeru na Mlimba


Utafiti na uchimbaji visima virefu vijiji vya Kalengakeru na Mlimba
Utafiti na uchimbaji visima 2 umekamilika

100

Victoria Drilling Company
62,090,000.00


































































































































































































































Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • RC aendelea na ziara Wilaya ya Morogoro, atatua migogoro ya wananchi.

    June 24, 2022
  • WANANCHI WA KIBWAYA MOROGORO WAMKUNA RC SHIGELA , ACHANGIA MIFUKO 50 YA SARUJI

    June 22, 2022
  • VIONGOZI WA USHIRIKA WATAKIWA KULIPA MADENI

    June 21, 2022
  • WAZIRI JAFFO ATOA MAAGIZO KWA UONGOZI MKOA WA MOROGORO.

    June 18, 2022
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.