Idara ya Elimu inalo jukumu la kusimamia utoaji wa Elimu katika ngazi za Awali, Msingi, Sekondari, Elimu ya Watu Wazima na Elimu ya Juu. Taasisi za elimu, zilizopo Mkoani hadi sasa ni kama inavyoonekana katika jedwali hapa chini:-
UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI
Katika mwaka 2017, uandikishaji wa wanafunzi katika madarasa ya awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza ni kama ifuatavyo:-
Jedwali 2: Uandikishaji wa wanafunzi
DARASA |
LENGO |
HALISI |
|||||
WAV |
WAS |
JUMLA |
WAV |
WAS |
JUMLA |
% |
|
AWALI
|
31796 |
31905 |
63701 |
35828 |
35317 |
71145 |
111.7 |
DARASA LA I
|
38566 |
36918 |
75484 |
45146 |
43416 |
88554 |
117.3 |
KIDATO CHA I
|
12560 |
13600 |
26160 |
10664 |
11360 |
22024 |
86 |
JUMLA
|
82922 |
82423 |
165345 |
91638 |
90093 |
181723 |
109.9 |
Chanzo:Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Uandikishaji wa wanafunzi madarasa ya awali na darasa la kwanza umeongezeka kutoka asilimia 83 mpaka asilimia 117.3 kwa darasa la kwanza, na asilimia 78 mpaka 117.7 kwa madarasa ya awali. Ongezeko hili limetokana sera ya utoaji wa elimu msingi bila malipo iliyoanza kutekelezwa katika kipindi cha mwaka 2016.
IDADI YA WANAFUNZI KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZA SERIKALI NA BINAFSI 2017
Mahudhurio ya wanafunzi darasani yameongezeka toka asilimia 86 Kwa mwaka 2016 hadi asilimia 95 kwa mwaka 2017, hii imetokana pia na kuondolewa shuleni kwa michango mbalimbali waliyokuwa wanatozwa wazazi. Pamoja na mahudhurio hayo yanayoridhisha bado wapo wanafunzi wanaokatiza masomo yao kwa utoro. Halmashauri kwa kushirikiana na Kamati na bodi za shule wanaendelea kuchukua hatua kwa wazazi wanaosababisha utoro kwa watoto wao kwa mujibu wa sheria.
Uwiano wa mwalimu na mwanafunzi ni 1: 57 kwa sasa badala ya 1:40 kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sera ya elimu. Halmashauri zinafanya jitihada za kurekebisha ikama kwa shule zenye upungufu mkubwa kila zinapopata fedha za kuhamisha. Tunaiomba serikali ione uwezekano wa kutoa ajira kwa walimu ili kuziba mapengo yaliyopo katika shule zilizo nyingi.
Jedwali 6: Mahitaji ya Walimu Shule za Sekondari
S/N |
MAHITAJI YA WALIMU |
MAHITAJI |
WALIOPO |
PUNGUFU/ZIADA |
1 |
SANAA |
3135 |
3848 |
+713 |
2 |
SAYANSI NA HISABATI |
1869 |
1231 |
744 |
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 2017
Kwa shule za sekondari upungufu upo kwa walimu wa sayansi na hisabati, lakini kuna ziada ya walimu wa masomo ya sanaa kama inavyoonekana katika jedwali. Hata hivyo tunaishukuru sana serikali kwa kutuletea walimu wa sayansi 152 kwa kipindi cha 2016/2017 idadi hii ya walimu imeongeza nguvu kazi katika shule na matarajio ni wanafunzi kufaulu mitihani yao kwa kiwango cha juu kwa kuwa sasa wanapata vipindi kwa masomo yote.
MIUNDOMBINU YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Takwimu zinaonesha kwamba upo upungufu mkubwa wa miundombinu katika shule za msingi na sekondari Mkoani. Jitahada zinaendelea kufanyika kuhakikisha kwamba miundombinu katika shule inatosheleza mahitaji. Jitihada hizi ni pamoja na
Jedwali Na : 7 Miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari
AINA |
MSINGI |
SEKONDARI |
||||
MAHITAJI |
YALIYOPO |
PUNGUFU |
MAHITAJI |
YALIYOPO |
PUNGUFU |
|
MADARASA |
11700 |
5268 |
6432 |
2286 |
2057 |
229 |
NYUMBA ZA WALIMU |
12729 |
1812 |
10917 |
4845 |
494 |
4351 |
MATUNDU YA VYOO |
20415 |
7812 |
12603 |
3489 |
2043 |
1446 |
MADAWATI |
162248 |
160695 |
1553 |
71568 |
70359 |
1209 |
OFISI ZA WALIMU |
843 |
0 |
843 |
187 |
49 |
138 |
MAABARA |
0 |
0 |
0 |
549 |
272 |
277 |
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 2017
Tunaishukuru sana Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa kutuletea vifaa vya maabara kwa shule zote za sekondari Mkoani, hadi sasa watahiniwa wote wa kidato cha nne (4) wamefanya mitihani ya “real practical” na sio “altenative to practical” kwa kuwa shule sasa zina vifaa vya kutosha. Mkoa unaendelea kuhimiza na kusimamia ukamilishaji wa ujenzi wa maabara kwa shule zote ifikapo JUNI 2018.
MAENDELEO YA UTOAJI WA TAALUMA
Mkoa unaendelea kusimamia utoaji wa taaluma katika shule za msingi na sekondari na umeendelea kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani mbalimbali ya kitaifa. Mfano kwa mwaka 2016 katika mtihani wa darasa la saba mkoa ulikuwa na wastani wa alama hamsini na nane (58) na kushika nafasi ya 23 kitaifa , kwa mwaka 2017 Mkoa umepata wastani wa alama sabini (70.78) na kushika nafasi ya kumi na moja (11) Kitaifa.
Mkoa umeweka mikakati ifuatayo ili kuendelea kuimarisha utoaji wa taaluma katika shule za msingi na sekondari:-
Mikakati ya kuboresha taaluma Mkoani.
|
UTEKELEZAJI WA UTOAJI WA ELIMU MSINGI BILA MALIPO MKOANI
Mkoa umeendelea kutekeleza utaoaji wa elimu msingi bila malipo kwa kutoa elimu kwa wadau wote wa elimu ili kila mmoja awe na uelewa wa nini kinatakiwa kufanyika, Elimu hiyo inatolewa kupitia vikao mbalimbali kuanzia ngazi za mitaa hadi Mkoa. Vile vile idara ya elimu imesambaza nyaraka zote muhimu zinazotoa maelekezo kuhusu elimu ya msingi bila malipo sambamba na kutoa ufafanuzi wa Sera hiyo pale panapohitajika. Hadi sasa shule zote za Msingi na Sekondari zinaendelea kutekeleza sera hiyo bila matatizo. Pale ambapo imeonekana viongozi ngazi ya shule kwenda kinyume na sera, hatua zimechukuliwa dhidi yao mara moja.
i. MAPOKEZI YA FEDHA ZA ELIMU MSINGI BILA MALIPO
Hadi kufikia Oktoba 2017, halmashauri zimepokea kiasi cha Tshs 2,731,302,76 kama inavyoonekana katika jedwali lifuatalo:-
Jedwali Na.8 Mapokezi ya fedha za Elimu Msingi kwa mwaka 2017/2018
S/N |
HALMASHAURI |
MSINGI |
SEKONDARI |
SHULE ZA BWENI/MAALUM |
JUMLA |
1 |
KILOMBERO |
130,970,344 |
95,819,585 |
0 |
226,789,929 |
2 |
KILOSA |
291,973,500 |
859,521,897 |
881,999,549 |
226,789,929 |
3 |
MOROGORO |
205,945,559 |
118,952,863 |
0 |
453,579,858 |
4 |
MANISPAA |
87,148,594 |
150,385,749 |
126,270,127 |
907,159,716 |
5 |
ULANGA |
65,002,597 |
38,168,110 |
90,984,011 |
194,154,718 |
6 |
MVOMERO |
212,192,893 |
65,786,961 |
96,970,795 |
374,950,649 |
7 |
GAIRO |
67,771,750 |
27,247,270 |
0 |
95,019,020 |
8 |
MALINYI |
43,915,726 |
22,966,896 |
0 |
66,882,622 |
9 |
IFAKARA |
65,081,520 |
59,645,352 |
61,249,448 |
185,976,320 |
10 |
JUMLA MKOA |
1,170,002,483 |
1,438,494,683 |
1,257,473,930 |
2,731,302,761 |
Chanzo:-Halmashauri za Wilaya 2017
Angalizo:-Fedha hizi ni kwa ajili ya uendeshaji wa shule, ukarabati mdogo mdogo, chakula kwa shule za bweni na watoto wenye mahitaji maalumu .Fedha hizi huingizwa katika akaunti za shule moja kwa moja.
ii. MAPOKEZI YA FEDHA ZA UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARI NA UKARABATI
Tunaishukuru sana serikali ya awamu ya tano kwa kutuletea fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu kwa shule za sekondari. Tunayo furaha kukujulisha kwamba tayari tumepokea fedha kama ifuatavyo:-
3.1.7 USIMAMIZI WA MASLAHI YA WALIMU MKOANI
i. Madeni ya walimu
Mkoa umeratibu zoezi la uhakiki wa madeni ya walimu Mkoani na jumla ya madai ya walimu ni Tshs 3,107,986,281.99. yakiwemo madai ya Uhamisho ,likizo,Matibabu.
ii. Upandishwaji madaraja ya walimu
Mkoa umewasilisha kwa Katibu Mkuu OR-TAMISEMI jumla ya walimu 5288 wakiwemo wa shule za msingi 4240 na sekodari 1048 wanaostahili kupanda madaraja kwa mwaka 2017 kama ilivyoelekezwa na Katibu Mkuu OR-TAMISEMI
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.