Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa, anawatangazia Watu wote wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika Mkoa wa Morogoro.
Maeneo ya kipaumbele katika uwekezaji huo ni pamoja na uanzishaji wa Kilimo cha kibiashara, Viwanda vya usindikaji wa mazao ya kilimo, Uanzishwaji wa Viwanda vikubwa, Utalii, Uchimbaji wa Vito na Madini na viwanda vya kusindika nyama.
Serikali ya Mkoa wa Morogoro imejipanga kuhakikisha kwamba wale watakaoonesha nia ya kuwekeza katika Mkoa wa Morogoro wanafanikiwa kutekeleza malengo yao kwa amani na utulivu.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Dawati la uwekezaji Mkoa wa Morogoro
Kwa simu Na:
+255232604237 au +255689641088
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.