Na Andrew Chimesela, Morogoro
Zaidi ya shilingi Bil. 7 za kitanzania zinatarajiwa kutumika kwenye ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja Mkoani Morogoro kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Hayo yamebainishwa Oktoba 22 mwaka huu na Mratibu wa Wakala wa Barabara Vijijini TARURA Mhandisi Benjamini Maziku wakati wa hafla fupi ya kusaini mikataba ya miradi 35 kati ya 46 iliyotangazwa kutekelezwa Mkoani humo.
Baadhi ya viongozi wakati wa hafla ya kusaini mikataba ya miradi mbalimbali Mkoani Morogoro. kutoka kulia ni Mratibu wa TARURA Mkoa wa Morogoro Mhandisi Benjamini Maziku, Mhandisi Emmanuel Kalobelo(RAS) na Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Miundombinu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ezron Kilamhama
Kwa mujibu wa Mratibu huyo ametaja idadi ya miradi hiyo itakayotekelezwa kwa kipindi hicho kwa kila Halmashauri na thamanai yake kwenye mabano kuwa ni pamoja na Wilaya ya Gairo miradi 3 (437,489,610.00), Ifakara miradi 3(370, 135,786.00), kilosa 5(Tsh. 887,694,910.00) na Kilombero 3(Tsh. 350,300, 340.00).
Baadhi ya wakandarasi, mameneja wa TARURA na Washiriki wa hafla hiyo
Miradi 6 ya Morogoro vijijini (Tsh. 850,904,100.00), Mvomero miradi 8(Tsh. 583,582,360.00) Malinyi mradi mmoja (Tsh. 167,154,000.00, na Halmashauri ya Manispaa Morogoro 5(Tsh. 1, 598,275,495.00)
Akifungua kikao hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewataka TARURA kuwa na utaratibu wa kuwalipa kwa wakati wakandarasi wanaoingia nao mikataba katika miradi mbalimbali ili wakandarasi hao waweze kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo akiongea na Wakandarasi na Mameneja wa TARURA wa Halmashauri wakati wa hafla fupi ya kusaini Mikataba
Mhandisi Kalobelo amesema hatua ya kuwalipa mapema wakandarasi hao itasaidia kuwasukuma wakandarasi katika utendaji kazi wao wa kutaka kukamilisha miradi yao kwa wakati bila kuwa na kigugumizi kwa kuwa tayari watakuwa hawana hoja ya kujitetea “Ili tuweze kuwabana hao wakandarasi vizuri na sisi TARURA …..tunapowapa Wakandarasi kazi pia tutimize wajibu wetu kwa kuwalipa kwa wakati” alisema Mhandisi Mhandisi Kalobelo.
Baadhi ya Wakandarasi na Meneja wa TARURA wakimsikiliza Mhandisi Kalobelo
Kwa upande wa Wakandarasi Katibu Tawala huyo amesema kama wapo Wakandarasi wenye tabia ya kutokamilisha kazi zao kwa wakati waone aibu na mara watakapo saini mikataba hiyo wawasilishe mipango kazi yao kwa TARURA na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya ufuatiliaji.
Kwa upande wao Wakandarasi hao wakiwakilishwa na Mhandisi Stanslaus Mkude wa Kampuni ya Luba Contractors pamoja na kuishukuru Serikali kwa kuwaona wanafaa kufanya kazi nao na kuwasihi wakandarasi wenzake kufanya kazi kwa ufanisi, weledi na kwa kuzingatia muda, huku akiwashawishi wenzake kuwatoa wafanyakazi wasiowajibika ipasavyo na kuwaajiri wengine kwa muda ili lengo la kukamilisha kwa wakati miradi husika liweze kutimia hivyo kuaminiwa na Serikali.
Hii ni baadhi ya Mikataba ya Miradi mbalimbali inayosubiriwa kusainiwa
MWISHO
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.