Waziri Lukuvi apeleka timu ya Wataalamu Kilosa Kuhakiki Mashamba yaliyofutiwa umiliki.
Na. Andrew Chimesela – Morogoro
Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Williamu Lukuvi amepeleka timu ya Wataalamu wa Masuala ya Ardhi kwa ajili ya uhakiki ya Mashamba yaliyofutwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKt. John Pombe Magufuli kwa lengo la kujua mipaka ya mashamba hay, kuayahkiki na kuyafufua upya.
Waziri Lukuvi ameyasema hayo Leo Aprili 16, 2019 akiwa katika ziara yake Wilayani Kilosa na kufanya mikutano hadhara katika Vijiji vya Chanzuru na Mvumi ambako aliwaeleza wananchi wa Vijiji hivyo kuwa ameleta timu hiyoikiwa na lengo la kutaka kuhakiki mashamba 15 yaliyofutiwa umiliki wake Wilayani humo na kuyahakiki kujua Mipaka yake, na kuyagawa kulingana na mahitaji yaliyopo.
“kwa hiyo nimekuja kuleta timu kutoka Wizarani, timu hii nataka ifanye kazi pamoja na viongozi wa ngazi ya Wilaya , Mkoa na Vijiji vinavyohusika, mashamba haya yafufuliwe tuyajue mipaka yake na historia ya wananchi walioko kwenye mashamba hayo wanaoitwa wavamizi” amesema Waziri Lukuvi.
Waziri Lukuvi amesema timu hiyo ambayo inaanza kazi kuanzia leo hii watafanya kazi hiyo na baada ya kukamilisha watapendekeza namna nzuri ya kuyatumia hayo mashamba ambayo ni pamoja na kuweka maeneo kwa ajili ya uwekezaji na kugawa kwa wananchi waliopo kwenye mashamba hayo hususan watakaobainika wanauhitaji kulingana na historia watakayoeleza kwa wataalamu hao.
Aidha, Lukuvi amesema viiongozi wa Serikali wa ngazi yoyote ambao walikuwa wanajimilikisha kwenye mashamba hayo yaliyofutwa umiliki wake na Mhe. Rais walikuwa wanafanya makosa na kama kuna kiongozi ambaye aligawa mashamba hayo kwa mwananchi au kuuza alifanya makosa na kwa sasa anafuta umiliki wake hadi pale uhakiki utakaofanywa na wataalamu aliowaleta
Mwisho Mhe. Lukuvi amewataka wananchi wa Wilaya ya Kilosa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Timu hiyo iliyoanza kufanya kazi ya uhakiki kwenye mashamba hayo ili kutatua migogoro ya Ardhi ambayo imekuwa kero kubwakwao na kwa Serikali kwa muda mrefu kwa kuwa huo ndio mwarobaini wa mwisho katika kutatuo changamoto hiyo.
MWISHO
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.