Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Mzee Philip Mangula amevitaka vyuo vya elimu ya juu nchini kupika wataalamu watakao muenzi Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo hasa katika kuelekea Tanzania ya viwanda kwa kuwa wasomi wanao utaalam unaoweza kulisaidia Taifa kufika huko.
Mzee Mangula aliyasema hayo wiki hii katika ukumbi wa Samola uliopo Chuo kikuu cha Mzumbe wakati wa kongamano la kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Nyerere ambalo lilikuwa na lengo la kujadili mambo mbalimbali aliyokuwa akiyafanya Mwl. Nyerere hususani kwenye sekta ya elimu.
Aidha Mzee Mangula alisema kuwa vyuo vya elimu ya juu ni vyombo vinavyo paswa kuwapatia wanafunzi uwezo wakuelewa na kuchakata fikra mbalimbali kwa malengo ya kujibu na kutatua changamoto na matatizo yanayoikabili jamii katika Nyanja mbalimbali kwa kuwa wasomi wanamchango mkubwa katika usitawi wa Taifa letu.
Akieleza namna alivyo mfahamu Mwl. Nyerere na kabla na baada ya Uhuru Mzee Mangula alisema “mimi namfaham Mwalim kwakuwa nilifanyanae kazi mda wote alisistiza uzalendo, maadili, pamoja na uwajibikaji kwa nchi yetu kwa hiyo na waasa wasomi wetu kuwa wazalendo wa kweli na tuipende nchi yetu kama mwalimu”.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe S. Kebwe alieleza kuwa Mwl. Nyerere alipanda mbengu nzuri ya kutuweka pamoja watanzania bila kubaguana kiukabila, udini wala rangi kitu ambacho kimetufanya kuwa wamoja tangu uhuru hadi leo.
Pia Dkt. Kebwe aliwaasa watanzania wanao tumia mitandao ya kijamii vibaya hadi wengine kufikia hatua ya kubeza juhudi alizofanya Baba wa Taifa kuacha mara moja “Tusitumie mitandao kupandikiza chuki kwa watu tena kuna watu wanabeza juhudi za Mwalimu hivi hamuoni nchi nyingine zilivyo na matatizo ya ukabiala naomba kama kuna mtu wa namana hiyo aache mara moja” alisema Dkt. Kebwe.
Nae Mkurugenzi wa Shirika la utangazaji Tanzania TBC Dr. Ayoub Liyoba amesema juhudi alizofanya Mwl. Nyerere tangu uhuru, Muungano, Azimio la Arusha, Elimu ya kujitegemea na namna zilivyo wasaidia watanzania hadi leo tuna vyuo vikuu vingi ambavyo vinatoa elimu ya utaalam wa mambo mbalimbali hivyo amewaomba watanzania kuwa wazalendo wa taifa lao ili kumuenzi Mwl. Nyerere kwa vitendo.
Kumbukizi la Mwl. Nyerere hufanyika kila mwaka tarehe 14 ya mwezi Oktoba ikiwa ni kukumbuka na kuyaenzi mambo aliyoyafanya Baba wa Taifa enzi za uhai wake ambapo hufanyika midahalo mbalimbali, mwaka huu maada iliyoandaliwa na Chuo kikuu cha Mzumbe ilikuwa ‘’niupi mtazamo wa Mwl. Nyerere kuhusu elimu ya juu’’
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.