• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Serikali inapoteza Bil. 18 kwa mwaka

Posted on: March 3rd, 2021

Serikali inapoteza zaidi ya Shilingi Mil.52 kila siku sawa na zaidi ya Bil.18 kwa mwaka kutokana na magari yanayopita katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi bila kulipa tozo.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Afisa Mhifadhi daraja la pili Mikumi Samwel Mguhachi wakati wa kikao cha kukuza na kuendeleza utalii na vivutio vingine Mkoani Morogoro kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Aidha, Mguhachi amebainisha kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2018 zaidi ya magari 2,218 yanapita hifadhini kwa siku na kuangalia vivutio bila kulipia tozo zozote ambapo mbali na magari hayo yaliyo kwenye safari pia baadhi ya waongoza wageni wamekuwa wakitumia fursa hiyo kufanya utalii bure.

Kutokana na upotevu wa mapato hayo, Mguhachi ameiomba Serikali kuanzisha tozo ya magari yanayopita katika barabara ya TANZAM kama ilivyo katika barabara zilizo katika hifadhi nyingine kwa kuwa hii pia ni fursa ya kuongeza mapato kwa Serikali.

Sambamba na ombi hilo, Mguhachi ameiomba Serikali kuweka utaratibu mahususi wa kupunguza au kuzuia kabisa upitaji wa magari nyakati za usiku kwenye barabara kuu inayopita katikati ya Hifadhi kwani ndio muda pekee ambao kumekuwa na matukio mengi ya wanyama kugongwa na matukio mengine ya uhalifu.

Akibainisha changamoto zilizopo katika sekta ya utalii Mkoani Morogoro  Afisa Wanyamapori wa Mkoa wa Morogoro Joseph Chuwa amesema kuna uwekezaji mdogo katika utalii hususan katika makampuni ya kusafirisha watalii.

Pia, Chuwa amebainisha changamoto nyingine kuwa ni ubovu wa miundombinu, kutotangazwa vivutio vya utalii, uharibifu wa mazingira unaotishia uhai wa vivutio vilivyokuwepo na upungufu wa fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli za kiutalii.

Akitoa taarifa ya hali ya vivutio vya utalii katika Mkoa huo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo amesema, Mkoa huo kwa sasa umejipanga vizuri kuwa wa Kiutalii kwa kutambua vivutio vyote vilivyopo katika Halmashauri tisa za Mkoa huo na kuandaa mwongozo ambao utahusisha mbuga za wanyama na utamaduni yaani vivutio vya asili.

Sambamba na hayo, Mhandisi Kalobelo ametoa wito kwa wadau wa kikao hicho kufikiria  namna  Mkoa wa Morogoro unavyoweza kujikuza kitalii kutokana na vyanzo vingi vya kitalii vilivyopo katika Mkoa huo hali itakayopelekea kuinua uchumi wa wananchi wake, Mkoa na Taifa kwa kwa ujumla.

Akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho amesema lengo kubwa la kikao hicho ni kuweka uelewa wa pamoja wa vivutio vilivyopo katika Mkoa huo, kutambua changamoto na kuweka mikakati ya kuendeleza utalii katika Mkoa  na taifa kwa ujumla.

Pia, Loata Sanare amebainisha kuwa hadi sasa sekta ya utalii inachangia zaidi ya asilimia 17 ya pato la taifa na kiasi kidogo ukilinganisha na utajiri wa vivutio na rasilimali nyingine zilizopo katika Mkoa wa Morogoro.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • Morogoro kumuenzi JPM kwa kudumisha Amani na Utulivu.

    March 24, 2021
  • RC MSTAAFU STEVEN MASHISHANGA ATOA SALAMU ZA POLE.

    March 19, 2021
  • RC Sanare awapa pole Wanamorogoro kwa Msiba Mkubwa, awataka watulie

    April 28, 2021
  • RC SANARE AIAGIZA TAKUKURU.

    March 13, 2021
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.