• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC morogoro ampongeza Mufti wa Tanzania

Posted on: December 29th, 2018


Na. Andrew Chimesela - Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amempongeza Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuber kwa Ofisi yake kuwa chimbuko la mshikamano wa dini zote unaoendelea kushamiri hapa nchini na kuondoa tofauti zilizokuwepo siku za nyuma.

Dkt. Kebwe ametoa pongezi hizo Disemba 28 mwaka huu wakati akitoa salamu za Serikali ngazi ya Mkoa aliposhiriki mazishi ya Sheikh wa Wilaya ya Morogoro Mjini Abdulrahaman Kiswabi (55) aliyefariki Dunia Disemba 27 saa tatu asubuhi nyumbani kwake Mjini Morogoro.

Dkt. Kebwe amesema ushirikiano mzuri, Amani na utulivu ambavyo vipo Mkoani Morogoro chimbuko lake ni Mufti wa Tanzania baada ya kuanzisha kamati ya Amani ambapo sasa kamati hizo zimesambaa karibu nchi nzima ukiwemo Mkoa wa Morogoro kwani kamati hiyo ni moja ya mafanikio ya Amani na Utulivu wa Mkoa.

“mshikamano huu wa dini zote katika nchi yetu, chimbuko lake ni Mufti. Kwa hiyo naomba mfikishie salamu namshukuru sana, kazi hii nzuri ambayo ameifanya, kamati ya Amani ya  Dar es Salaam ilianza na sasa imesambaa kote  nchini” alisema Dkt. Kebwe.

Dkt Kebwe aliongeza akisema siku hizi hakuna mihadhara ambayo ilikuwa inatokea siku za nyuma, dini moja kukashfu dini nyingine hii inatokana na matunda ya kazi nzuri ambayo Mufti ameifanya pamoja na timu yake.

Katika hatua nyingine, Dkt. Kebwe amesema Sheikh Abdulrahaman Kiswabi aliishi vizuri na watu na kutoa wito kwa watu wengine kumuenzi marehemu kwa kuyaishi mema  aliyoyatenda marehemu kipindi cha uhai wake katika kutunza Upendo, Amani na Utulivu mambo ambayo pia Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa akisisitiza mara zote.

Naye Kiongozi wa ULAMAA ambaye pia ni Msemaji wa Mufti hapa nchini Sheikh Hassan Chizenga ambaye alishiriki katika mazishi hayo alisifu ushirikiano uliopo baina ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Serikali kwa jumla na madhehebu ya Dini na kutaka ushirikiano huo udumishwe.

“Kitendo cha Mkuu wa Mkoa na Meya na wote kuhudhuria mazishi haya, kinaonesha kwamba Serikali inatambua mchango wa Viongozi wa Dini katika kujenga Amani na maendeleo ya nchi yetu” alisema Sheikh Chizenga.

Kiongozi huyo wa kidini pia aliwataka waombolezaji waliofika katika msiba huo kuishi kulingana na maelekezo ya mwenyezi Mungu kama alivyofanya Sheikh Abdulrahaman Kiswabi.

Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga kwa niaba ya wananchi wa Manispaa hiyo, aliwaasa wananchi kuishi vizuri huku akisema kifo kiliumbwa na hakuna haja ya kuhoji kwanini kipo badala yake kila mmoja aishi vizuri kulingana na imani ya dini yake.

Nao waombolezaji waliofika kushiriki mazishi hayo wamemuelezea marehemu kuwa alikuwa na moyo wa kuwapenda watu, alipenda dini yake, alipenda kujifunza na alijituma wakati wote kutumikia dini yake.

Marehemu Sheikh Abdulrahaman Kiswabi amezikwa Disemba 28 kijijini kwao Kikundi (Kilungule) katika Wilaya ya Morogoro Vijijini.



Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • ZAIDI YA BIL. 7 ZATARAJIWA KUTUMIKA MOROGORO.

    March 04, 2021
  • Serikali inapoteza Bil. 18 kwa mwaka

    March 03, 2021
  • Wahasibu Halmashauri za Morogoro waonywa.

    March 03, 2021
  • Mkoa wa Morogoro wajipanga kuwa wa kiutalii.

    February 26, 2021
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.