• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Moro awataka madiwani Ulanga kujitathmini

Posted on: January 8th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amelitaka Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mkoani humo kujitathmini na Kujipanga upya katika kusimamia fedha pamoja na rasilimali nyingine za Halmashauri hiyo.

Dkt. Kebwe ameyasema hayo Januari 7, mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga mbele ya Madiwani na watumishi wengine wa Halmashauri hiyo ikiwa ni kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa ya matokeo ya uchunguzi ya utendaji usioridhisha wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Tume Maalum ya Uchunguzi iliyoundwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi (OR – TAMISEMI), ilipendekeza Mkuu wa Mkoa kutakiwa kuiwasilisha taarifa hiyo ya matokeo ya Uchunguzi mbele ya Baraza hilo la Madiwani kwa hatua zaidi kwa kuwa Baraza hilo ndilo lenye mamlaka Kuhusu utendeji mzima wa Halmashauri na masuala mengine ya kiutumishi.

Baada ya kutekeleza jukumu hilo, Dkt. Kebwe anatumia fursa hiyo kuwataka madiwani kujitathmini na kujipanga upya katika kusimamia fedha na rasilimali nyingine za Halmasauri yao kama ambavyo mwongozo wa Serikali unaeleza.

“Ninachojiuliza hapa ni kwanini ubadhilifu wote huu unatokea na Baraza la Madiwani lipo. Mjitathmini na kujipanga upya kusimami fedha za Halmashauri wakati Serikali inaendelea kulifuatilia suala hili”. Dkt. Kebwe alishauri.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga ameishukuru Serikali kwa hatua ilizozichukua kuhusu sakata hilo ambalo amesema kimsingi sio geni kwani limekuwa likijadiliwa sana katika vikao vya Baraza hilo lakini kulikuwa na hali ya kusuasua katika kuwachukulia hatua watumishi waliokuwa wanatuhumiwa hali iliyompelekea kutumia Ofisi yake kuibua hoja hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Furaha Lilongeri amesema amefarijika kwa hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuokoa fedha za Halmashauri hiyo huku akiahidi kwa niaba ya Baraza lake la Halmashauri kuyachukua na kuyatekeleza mara moja mapendekezo yaliyotolewa na tume maalum ya uchunguzi.

Aidha, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Clifford Tandari amewakumbusha Madiwani hususan Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kuchukua nafasi zao pindi wanapogundua kuna harufu ya ubadhilifu wa fedha kutoka kwa wakaguzi wa Serikali idara ya fedha ili Mkoa nao uweze kuchukua hatua Stahiki mapema.

Huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Yusufu Semuguruka ambaye pamoja na mambo mengine anatuhumiwa kutumia shilingi 117mil. kwa mwaka kama posho yake ya safari badala ya kutumia shilingi 75mil. alizopangiwa amesema amepokea kwa utulivu tuhuma hizo hata hivyo anaamini vyombo vya utaalamu wa kifedha watafanya uchunguzi wao na uhalisia utabainika.

Hivi karibuni Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga imekabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa fedha kiasi cha shilingi 2.9Bil. ambapo baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo walikosa uaminifu na kuisababishia Halmashauri hiyo hasara.

Hadi sasa Watumishi 12 tayari wameshakamatwa na vyombo vya Dola na uchunguzi wa ubadhirifu huo unaendelea na itakapodhibitika wana kesi ya kujibu watafikishwa mahakamani.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • ZAIDI YA BIL. 7 ZATARAJIWA KUTUMIKA MOROGORO.

    March 04, 2021
  • Serikali inapoteza Bil. 18 kwa mwaka

    March 03, 2021
  • Wahasibu Halmashauri za Morogoro waonywa.

    March 03, 2021
  • Mkoa wa Morogoro wajipanga kuwa wa kiutalii.

    February 26, 2021
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.