Rai hiyo imetolewa na Prof. Paramagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianao wa Afrika ya Mashariki wakati akizindua sherehe za Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Uvuvi Kanda ya Mashariki zilizofanyika katika viwanja vya Mwl. Julius Kambaragae Nyerere katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mkoani humo.
Prof. Kabudi amsema hivi karibuni Tanzania imeingia kwenye Uchumi wa Kati hatua hiyo imechangiwa na Ujenzi wa Viwanda iliyofanywa na Serikali ya awamu ya Tano ikiongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Amesema kwa sasa viwanda vitahitaji mali ghafi hivyo ni jukumu la Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kuongeza juhudi katika kuzalisha mazao hayo kwa kutumia teknolojia mpya ambayo wataipata kupitia Maonesho ya Wakulima na Wafugaji maarufu kama Nanenane.
Ameongeza kuwa nia ya Serikali ni kuongeza uchumi wa Taifa na wa mtu mmoja mmoja ili kupata mazao mengi na bora hivyo vema wakulima wakawa na tabia ya kutembelea maonesho hayo ili kupata Elimu mpya katika kuzalisha mazao yao.
Katika Hatua nyingine Prof. Kabudi amewataka watanzania kuanza kujielekeza katika kilimo cha mimea dawa badala ya kuendelea kulima mazao ya kawaida pekee kwa kuwa mimea dawa ina soko katika nchi nyingi hapa Duniani.
“Wakati umefika sasa kwa watanzania kuanza kulima mimea dawa au miti dawa, nawahakikishia baada ya miaka mitano ijayo Tanzania itakuwa na biashara kubwa sio Tanzania tu bali pia Duniani” alisema Prof. Kabudi.
Akijibu maombi yaliyotolewa mbele yake juu ya sherehe hizo kufanyika Kitaifa katika kanda ya Mashariki, Prof. Kabudi amesema amelichukua ombi hilo na ataliwasilisha ngazi ya Taifa na ataendelea kufuatilia ombi hilo ili mwakani Maonesho hayo ya nanenane ikiwezekana yafanyike Kanda ya Mashariki inayoundwa na Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga na mwenyeji Mkoa wa Morogoro.
Maonesho ya Nanenane mwaka huu ni ya 27 tangu kuanzishwa kwake na ni ya Nne tangu yaanze kuratibiwa na Sekretarieti za Mikoa. Kaulimbiu ya maonesho ya mwaka huu ni “Kwa maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi chagua Viongozi Bora 2020” yakibeba tukio la kitaifa la kuwepo kwa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
MWISHO.
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.