MOROGORO MARATHON KUTANGAZA UTALII
Mashindano ya Riadha ya nayotarajiwa kufanyika Mkoani Morogoro hivi karibuni maalufu kama Morogoro Marathon ya tasaidia kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Mkoani humo zikiwemo mbuga za Wanyama Mikumi, Selous, Ruaha misitu ya Udizungwa na nyingine nyingi.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ofisini kwake Novemba 2 mwaka huu Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Kebwe S. Kebwe amewaasa wananchi wote Mkoani humo kujitokeza kwa wingi kushiriki mashindano hayo ili waweze kupata fulsa ya kujifunza umuhimu wa utalii na kuzijua vizuri sehemu za vivutio vya utalii Mkoani humo.
“Siku hiyo wanamorogoro naomba wajitokeze kwa wingi kwa kadri watakavyo weza na washiriki kikamilifu ili tuutangaze Mkoa wetu kiutalii kwa sababu Mkoa wetu ndio Mkoa pekee Tanzania kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii”alisema Dkt. Kebwe.
Aidha, Dkt. Kebwe amewataka wananchi wa Mkoa huo kuto wa wekea Watoto wao mikanda ya Wanyama badala yake wawapeleke katika mbuga za Wanyama na sehemu nyingine zenye vivutio vya kitalii katika Mkoa huo wakatalii ili wajionee moja kwa moja Wanyama wanaowaona kwenye TV.
Kwa upande wake afisa utamaduni Mkoani humo Bi. Grace Njau amesema mashindano hayo ya takayofanyika Morogoro kwa mara ya kwanza ya takuwa na zawadi mbalimbali kwa washindi hivyo amewataka wanamorogo watakaoshiriki kujiandaa kikamilifu ili waweze kuibuka washindi.
Nae Katibu wa Riadha Mkoa wa Morogoro Bw. Omary Chamlungu amesema mashindano hayo yatakuwa na umbali wa kilometa 21 na umbali wa kilometa tano 5 ambapo amebainisha kuwa vipomo vimesha fanyika na marekebisho madogo ya liyobaki watayakamilisha hivi punde.
Morogoro Marathon ni mashindano ya Riadha ya nayotarajiwa kufanyika Mkoani Morogoro kuanzia Disemba 2 mwaka huu ambapo watu Zaidi ya 4,000 kutoka sehemu mbalimbali wanatarajia kushiriki mashindano hayo huku ya kibeba dhima ya kutangaza vivutio vya utalii Mkoani humo.
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.