• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Kamati ya amani na maridhiano yatoa tamko.

Posted on: October 20th, 2020


Kamati ya amani na maridhiano Mkoani Morogoro imewataka watanzania  kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi ili kuepuka madhara mbalimbali ambayo yanaweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na umwagaji damu.

Hayo yamebanishwa Oktoba 20 Mwaka huu na Kamati hiyo, wakati wakizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mikutano wa  Morogoro Hotel  iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambapo wamewataka wananchi kulinda amani waliyonayo kwa maslahi ya nchi na vizazi vijavyo.

Akiwa katika kikao hicho  Askofu Jacob  Mameo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) amesema uwepo wa amani ndio unaopelekea watanzania  kuendelea kushiriki katika kazi mbalimbali bila woga ikiwa ni pamaja na kushiriki kwenda kwenye nyumba za ibada.

Hivyo, kukosekana kwa amani kutapelekea watanzania kutojihusisha na shughuli za kijamii na kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na kukosa utulivu kama baadhi ya nchi nyingine zilivopoteza amani na matokeo yake kuwa na vita visivyo na kikomo.

Ahmad Khailallah ambaye ni Katibu wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Morogoro amesema kwa upande wa Waumini wa dini hiyo hawana mgombea yeyote wa kiti cha urais ambaye waumini hao wanatarajia kumpigia kura kuwa Rais isipokuwa kila muumini atampigia kura Mgombea anayemtaka kulingana na sera alizotoa wakati wa kujinadi

“kama waislam hatuna mgombea ambaye tumemsema na kumtangaza ndiye atakayekuwa anasimamia Waislam, hatuna. mgombea wa Waislamu hatuna,  ila kila mtu anamgombea ambaye anajua nani ataenda kumpigia kura”alisema Khailallah.


Naye Askofu Dr. Peter Denis wa Kanisa la CPCT amewashauri vijana kutoshawishika kirahisi na wanasiasa ambao baadhi yao wanataka mara baada ya matokeo kutangazwa waingie mitaani na kufanya fujo jambo ambalo linaweza kuleta hasara kwao, akinamama, watoto na wazee.

Hata hivyo, Lawrence Mdee amewataka wanasiasa Kutumia busara zaidi na mazungumzo baina yao kwa lengo la kuleta maendeleo katika jamii na kuepuka kutumia silaha  dhidi ya wananchi  ili kunusuru taifa hili.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • Morogoro kumuenzi JPM kwa kudumisha Amani na Utulivu.

    March 24, 2021
  • RC MSTAAFU STEVEN MASHISHANGA ATOA SALAMU ZA POLE.

    March 19, 2021
  • RC Sanare awapa pole Wanamorogoro kwa Msiba Mkubwa, awataka watulie

    April 28, 2021
  • RC SANARE AIAGIZA TAKUKURU.

    March 13, 2021
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.