JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
     
 
     
USHIRIKA
 
[ Nyumbani ]
 

Vyama vya Ushirika

Kufikia Desemba, 2008, vipo vyama vya ushirika vya aina mbalimbali 441 vyenye jumla ya wanachama 43,752 (Me 25,675 na Ke 18,077) na hisa zenye thamani ya shilingi 6,668,828,000/= Jumla ya vyama vya Akiba na Mikopo mwaka 2008 ilikuwa 314 ukilinganisha na vyama 97 vilivyokuwepo mwaka 2005 vyenye jumla ya Wanachama 25,6 79 ambapo wanaume ni 16,635 na wanawake 9,044 na jumla ya Mtaji wa Sh. 6,000,345,000. Vimeongezeka vyama vya Akiba na Mikopo 217 sawa na ongezeko la asilimia 223.7, vyenye jumla ya wanachama 18,003, (wanaume ni 9,040 na wanawake 8,963) na jumla ya mtaji wa Sh. 969,624,000.

Kipindi cha kuishia Oktoba, 2008, SACCOS ziliweza kutoa mikopo kwa wanachama kiasi cha Sh. 22,236,298,000 na marejesho ya Sh. 12,729,254,000 yalifanyika.

Kwa upande wa vyombo vya fedha, wananchi wamewezeshwa kiuchumi kupitia CRDB LTD ambayo imekopesha SACCOS Sh. 1,358,250,000 na Mfuko wa Rais umekopesha jumla ya shs. 100,000,000/=. Fedha hizi hazijawahi kutolewa kabla na zimesaidia kupunguza umaskini wa kipato na kuongeza ajira.

 

 

         
 
[ Nyumbani ]
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, TEL: 026 - 2604237/2600973, FAX: 026 2601000