JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
   
     
     
 
     
TAKWIMU
 
[ Nyumbani ]
 

Mkoa wa Morogoro kiutawala umegawanyika katika Wilaya tano ambazo ni Wilaya ya Morogoro, Mvomero, Kilosa, Kilombero na Ulanga.

Kufuatana na Muundo wa Serikali za Mitaa Mkoa una Halmashauri za Wilaya tano na Halmashauri ya Manispaa moja ambazo ni Kilosa, Kilombero, Ulanga, Morogoro Vijijini, Mvomero na Manispaa ya Morogoro.

Sambamba na kupeleka madaraka zaidi kwa wananchi Mkoa una mamlaka za Miji Midogo zinazofanya kazi za Gairo, Kilosa, Mikumi, Ifakara na Mvomero. Mkoa unayo majimbo ya Uchaguzi yenye Wabunge 10, Kata 141, Vijiji 543 na Mitaa 274 vitongoji 2,948.

Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya watu na makazi ya 2002 idadi ya watu katika Mkoa wa Morogoro ilifikia watu 1,759,809 ukilinganisha na idadi ya watu 1,220,564 kutokana na Sensa ya mwaka 1988.

Kati ya watu 1,759,809, wanawake ni 882,575 sawa na asilimia 50.2 na wanaume ni 877,234 sawa na asilimia 49.8%. Wastani wa idadi ya watu katika Kaya ni 4.6. Makisio ya idadi ya watu kwa mwaka 2008 ni watu 2,021,714 kutokana na kiwango cha ongezeko la watu la asilimia 2.6 kwa mwaka.

Idadi ya Majimbo, Kata, Vijiji na Vitongoji Mkoa wa Morogoro

Na.

WILAYA

HALMASHAURI

MAJIMBO
YA
UCHAGUZI

TARAFA

KATA

VIJIJI

MITAA

VITONGOJI

1.

Morogoro

Morogoro(M)

1

1

19

-

274

 

2.

 

Morogoro

2

6

25

132

-

657

3.

Mvomero

Mvomero

1

4

17

101

-

583

4.

Kilosa

Kilosa

3

9

37

164

-

1040

5.

Kilombero

Kilombero

1

5

19

81

-

360

6.

Ulanga

Ulanga

2

5

24

65

-

308

JUMLA

5

6

10

30

141

543

274

2948

 

 
[ Nyumbani ]
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, TEL: 026 - 2604237/2600973, FAX: 026 2601000