JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
     
 
     
SERIKALI ZA MITAA
 
[ Nyumbani ]
 

Mkoa wa Morogoro ulitekeleza mpango wa uboreshaji wa Serikali za mitaa awamu ya kwanza na kufanikiwa katika maeneo yafuatayo

• i. Kuongeza tija katika ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi ya fedha hivyo, kuwezesha Mkoa na Halmashauri zake kupata hati safi za ukaguzi wa hesabu.

• ii. Kutunga na kusimamia sheria ndogondogo ili kudhibiti uvunjaji wa sheria.

• iii. Halmashauri zote na Sekretarieti ya Mkoa zimeanzisha Ofisi za kushughulikia malalamiko na kero za wananchi. Rejesta na masanduku ya maoni yamewekwa katika sehemu zote za huduma.Aidha, Ofisi zote za Tarafa, Kata na Serikali za Vijiji zinapokea malalamiko na kero za wananchi na kuzifuatilia.

• iv. Kuwashirikisha wananchi katika kupanga mipango ya bajeti kwa kutumia mfumo wa fursa na vikwazo vya maendeleo (O&OD).

• v. Taarifa zote za Halmashauri zinazohusu mapato na matumizi, zabuni na taarifa za miradi ya maendeleo zimetangazwa kwenye magazeti na kubandikwa katika mbao za matangazo ili kukuza dhana ya uwazi na uwajibikaji kwa wananchi na wadau wengine.

• vi. Halmashauri na Mkoa zimezingatia masuala ya jinsia katika ajira na shughuli mbalimbali za kiutumishi.

• vii. Halmashauri na Mkoa zimeunda Kamati za Kisheria na kuendesha vikao vya kamati husika kwa mujibu wa sheria na miongozo iliyopo.

• viii. Halmashauri zote ndani ya Mkoa zimeendelea kuendesha vikao vya Serikali za Vijii/Mitaa na mikutano ya wananchi ili kutoa fursa kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika shughuli za utawala na uendeshaji wa mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo yao.

• ix. Mkoa wa Morogoro tayari umeunda kamati za Ushauri ngazi ya Wilaya (DCC) na kufanya jumla ya vikao 6.

 

Kwa ujumla mapato ya Halmashauri yameongezeka tangu mwaka 2005 kutoka shs. 2, 251, 478,924.36 na mwaka 2008 mapato yamefikia shs. 2,498,129,082.28 sawa na ongezeko la asilimia 10.96.

 

 

         
 
[ Nyumbani ]
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, TEL: 026 - 2604237/2600973, FAX: 026 2601000