Kimsingi kazi za Mkaguzi wa Ndani na zile za Mkaguzi wa Nje hazitofautiani kwani wote wawili wanafanya ukaguzi wa mahesabu, ili kuhakikisha ufanisi kiutendaji na matumizi bora ya fedha na mali za Sekretarieti ya Mkoa/Halmashauri. Tofauti iliyopo ni kwamba Mkaguzi wa Ndani ni mtumishi wa Sekretarieti ya Mkoa/Halmashauri na anawajibika kwa Sekretarieti ya Mkoa/Halmashauri kiutendaji, wakati Mkaguzi wa Nje ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na ambaye anawajibika kwa Bunge.
|