-
Kuhakikisha Mkoa unakuwa na amani, utulivu, usalama na mshikamano kwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora.
-
Kuziwezesha na kuzijengea mamlaka za Serikali za Mitaa uwezo wa kiutendaji ili ziweze kutoa huduma zinazostahili kwa wananchi.
-
Kuhakikisha huduma bora za kiuchumi zinawafikia wananchi walio wengi kwa viwango na ubora unaostahili.
-
Kuhakikisha masuala mtambuka kama vile UKIMWI, Hifadhi ya mazingira na jinsia yanapewa kipaumbele katika kupanga mipango na kupewa rasilimali.
-
Kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA).
|