Katika mwaka wa fedha 2009/2010 Mkoa wa Morogoro unakadiria kutumia jumla ya fedha shilingi za Kitanzania 124,498,740,964 kutekeleza shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo, kulipa gharama za Mishahara na Matumizi Mengineyo kwa watumishi wa Mkoa, wilaya na Serikali za mitaa.
Fedha shilingi 95,691,298,110 kwa ajili ya Bajeti ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo, shilingi 26,372,489,448/= ni kwa ajili ya kugharamia matumizi mengineyo ( OC) na shilingi 69,318,849,662/= kwa ajili ya kulipia gharama za mishahara ( PE) kwa Mkoa na Serikali za Mitaa.
Fedha za Bajeti ya matumizi ya kawaida zinajumuisha Ruzuku ya shilingi 89,155,338,902 Kati ya hizo shilingi 64,916,849,454/= ni kwa ajili ya kugharamia mishahara na shilingi 24,238,489,448/= ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo.
Sekretariati ya Mkoa katika mwaka 2009/2010 inakadiria kutumia jumla ya shilingi 6,535,959,208 kati ya fedha hizo, shilingi 4,401,959,208/= ni kwa ajili ya kugharamia mishahara na shilingi 2,134,000,000/= kwa ajili ya kugharamia Matumizi Mengineyo. Aidha, kwa upande wa fedha za Maendeleo za ndani Mkoa unakadiria kutumia jumla ya shilingi 6,464,692,000/= Kati ya fedha hizo shilingi 698,774,000/= ni kwa ajili ya utekelezaji miradi ya Maendeleo inayosimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na fedha shilingi 5,772,631,000/= kwa ajili ya kutekeleza miradi inayosimamiwa na Serikali za Mitaa.
Aidha,Katika Mwaka wa fedha 2009/2010 Mkoa wa Morogoro unakadiria kutumia fedha za nje shilingi 22,027,079,758/= kutoka kwa Wadau mbalimbali wa maendeleo kwa ajili ya kutekeleza miradi iliyo chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa na serikali za mitaa. Kati ya fedha hizi sh. 415, 510,672/= ni kwa ajili ya miradi iliyo chini ya usimamizi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa na sh. 21,611,569,086/= kwa ajili ya kutekeleza miradi inayosimamiwa na Serikali za Mitaa.
|