JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
     
 
     
Uwekezaji
 
[ Nyumbani ]
 

Fursa za Uwekezaji Mkoani Morogoro

Mkoa wa Morogoro una fursa nyingi za uwekezaji hususan katika kilimo (ufugaji, uvuvi, mazao ya misitu, kilimo cha mazao); biashara, viwanda, utalii na madini.

Fursa za uwekezaji katika Kilimo

 Uwekezaji katika kilimo unajumuisha kilimo cha mazao ya chakula na biashara; ufugaji; uvuvi; na mazao ya misitu.

Fursa za Uwekezaji katika Kilimo cha Mazao ya Chakula na Biashara.

(i) Mkoa una eneo la hekta 2,226, 396 za ardhi nzuri inayofaa kwa kilimo.

(ii) Mkoa una mito 143 inayotiririka mwaka mzima na yenye kutosheleza kilimo cha umwagiliaji.

(iii) Kuna hali nzuri ya hewa na misimu miwili ya mvua kwa mwaka ambayo ni mvua za vuli zinazoonyesha mwezi Oktoba hadi Desemba; na mvua za masika zinazonyesha mwezi Februari hadi Mei.

(iv) Kuna vituo vya utafiti na vyuo vya mafunzo ambavyo ni pamoja na Dakawa, KATRIN Kilombero Agricultural Training and Research Institute), chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), MATI – Ilonga (Ministry of Agriculture and Training Institute), LITI – Morogoro (Livestock Training Institute).

(v) Mkoa una jumla ya masoko ya mazao 70; Kilosa ina masoko 29, Mvomero 12, Morogoro 9 Ulanga 8, Kilombero 6 na Manispaa ya Morogoro 6.

(vi) Kuwepo kwa idadi kubwa ya mashamba 533 yaliyopimwa ambayo hayazalishi kwa sasa; pamoja na maeneo mengine mazuri kwa uzalishaji ambayo hayajapimwa.

 

(i) Uwepo wa mito na mabwawa unatoa fursa ya uwekezaji katika uvuvi

(ii) Kuna kituo cha utotoleshaji wa samaki kwenye Manispaa ya Morogoro kilicho chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambacho hutotolesha samaki kwa ajili ya kupandwa kwenye mabwawa ndani ya Mkoa na nje ya MKoa.

Fursa za uwekezaji katika Mazao ya Misitu

 (i) Kuna misitu ya asili na isiyo ya asili ambayo inawezesha upatikanaji wa mbao kwa matumizi mbalimbali pamoja na nishati ya kuni na mkaa.

(ii) Uwepo wa misitu unaleta fursa ya ufugaji wa nyuki kwa ajili ya asali.

 Fursa za uwekezaji katika Utalii

(i) Mkoa wa Morogoro una vivutio vingi vya kitalii ambavyo ni pamoja na mbuga za wanyama Mikumi, Udzungwa na Pori Tengefu la Selous .

(ii) Yapo maporomoko ya maji ( Water Falls ) Chita , Sanje na Sali.

(iii) Kuna Bwana la Kibasila huko Mofu Kilombero ambalo ni kivutio kizuri cha Utalii.

(iv) Kuna Ndege wa kuvutia wa Utengeule na vyura adimu wa Kihansi.

Fursa za Uwekezaji katika Madini

6. Madini yanayopatikana Mkoani Morogoro ni pamoja na dhahabu, ruby, Chokaa, uranium, amazonite, moonstone, Feldspar, quartz, graphite, Ulanga, mawe, Kokoto, Changarawe na mchanga.

Fursa za uwekezaji katika Viwanda

(i) Viwanda vidogo vilivyopo kwa sasa ni vya ukamuaji wa mafuta ya kula, useketaji, useremala, ufinyanzi, uhunzi, uchongaji, ukoboaji nafaka na uchoraji.

(ii) Viwanda vya kati na vikubwa vilivyopo ni: usindikaji wa ngozi ( East Hides Ltd .) utengenezaji nguo ( 21 st Century Textile Ltd. ), utengenezaji magunia ( Tanzania Packaging Manufacturers Ltd. ), utengenezaji maturubai ( Morogoro Canvas Mills Ltd ), Ukamuaji mafuta ( Morogoro Oil Processing Company Ltd .), utengenezaji Nyaya, Utengenezaji sabuni ( Abood Soap Industry Ltd.), usindikaji nyama ( Tanzania Pride Meat ), usindikaji Tumbaku ( Alliance One ltd., Tanzania Tobacco Processing Company ); utengenezaji Sukari ( Mtibwa Sugar Company na Kilombero Sugar Company ).

(iii) Mazao mbalimbali yanayozalishwa Mkoani Morogoro ni fursa nzuri kwa viwanda vya usindikaji.

(iv) Umeme upo wilaya zote za Mkoa huu. Mitambo ya kufua umeme ipo Kihansi na Kidatu Mkoani Morogoro.

Fursa ya Uwekezaji katika Biashara

(i) Uwepo wa idadi kubwa ya watu Mkoani Morogoro ni fursa ya soko kwa bidhaa za biashara.

(ii) Huduma za Mawasiliano ya simu hupatikana kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL ), Zain, Vodacom, TIGO, Zantel na huduma za Posta na mtandao wa Kompyuta ( Internet) zinapatikana Wilaya zote.

(iii) Zipo barabara kuu na reli zinazounganisha 45 Mkoa wa Morogoro na Mikoa mingine.

MIKAKATI YA NAMNA YA KUFANIKISHA UWEKEZAJI MKOANI MOROGORO.

3.1 Kuongeza uzalishaji wenye tija wa mazao ya chakula na biashara ili eneo dogo liweze kuzalisha mazao mengi na bora.

3.2 Kutwaa mashamba yasiyoendelezwa ili yatumike katika uwekezaji wa mazao ya chakula na biashara.

3.3 kuongeza matumizi ya fursa ya umwagiliaji iliyopo Mkoani.

3.4 Kuboresha miundombinu hususan katika maeneo yenye fursa kubwa ya uzalishaji.

3.5 Kuwahamasisha wananchi wa Mkoa wa Morogoro, hasa vijana, kushiriki shughuli za uzalishaji hususan katika kilimo.

3.6 Kuhimiza usindikaji wa mazao ili kuongeza thamani

3.7 Kuandaa mazingira ya uapatikanaji wa taarifa za masoko.

3.8 Kuboresha ufahamu na Stadi za wakulima kwa kuwapa mafunzo kwa kutumia magari ya sinema, vielelezo na maonyesho ya Wakulima ya Nane Nane.

3.9 Kuhakikisha kuwa wakulima wanawezeshwa kupata zana bora za kilimo na pembejeo.

3.10 Kupiga marufuku shughuli za Unyago, Ngoma na Sherehe za kimila wakati wa kilimo.

3.11 Kuhimiza elimu ya ujasiriamali kwa wajasiriamali tarajiwa na watendaji wanaosimamia fani mbalimbali.

3.12 Kuwakaribisha wawekezaji walio nje ya Mkoa kuwekeza Mkoani Morogoro katika maeneo ya Kilimo, Biashara, Viwanda, Utalii, Madini, Uvuvi na Misitu.

 

 

 

         
 
[ Nyumbani ]
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, TEL: 026 - 2604237/2600973, FAX: 026 2601000