Kikao cha Baraza la wafanyakazi kitafanyika tarehe 6/06/2009 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Baraza hili limeanzishwa kwa mujibu wa agizo la Rais la mwaka 1970. Lengo la agizo hilo ni kushirikisha Wafanyakazi katika Uongozi wa pamoja mahali pao kazi.
Aidha, ni kwa mujibu wa kifungu cha 30(3) cha Sheria Na.19 ya majadiliano ya mwaka 2003, ikisomwa pamoja na kifungu Na.108 cha kanuni za utumishi wa Umma za mwaka 2003.
Kimsingi, tunapaswa kufanya kikao cha Baraza hili mara mbili (2) kwa mwaka. Pamoja na mambo mengine, wajumbe watapaswa kupitia maeneo ya vipaumbele vya Bajeti ya Mkoa chini ya uenyekiti wa Katibu Tawala Mkoa.
|