JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
     
 
     
MALIASILI
 
[ Nyumbani ] au
 

Maliasili katika Mkoa wa Morogoro inahusisha misitu, mito, mabwawa ya asili, samaki, ufugaji nyuki, wanyamapori na hifadhi ya mazingira.Rasilimali hizi ni muhimu katika uhifadhi wa vyanzo vya maji, urutubishaji wa udongo, uzuiaji wa mmomonyoko, vyanzo vya nishati na malighafi za viwandani na vyanzo vya umeme ambavyo ni muhimu kwa wakazi wa Mkoa na Taifa.

Jumla ya kilometa za mraba 64,000 za Mkoa zimetengwa kwa ajili ya hifadhi ikiwemo mito 143 ambayo ni vyanzo vya maji.Eneo hili ni kubwa kuliko maeneo ya hifadhi katika Mikoa yote Tanzania; na kuhusisha misitu 80 ya hifadhi, mbuga 3 za Hifadhi za Taifa za Mikumi na Udzungwa na sehemu ya pori la akiba la Wanyamapori la Selous lenye umaarufu mkubwa duniani.

Mkoa umewahamasisha wananchi kupanda miti kwa wingi kwa kila mwananchi kupanda miti kati ya 6-8 hivyo na kuwa na hekta 6,000 za miti iliyopandwa kila mwaka kwa ajili ya kuni, matunda, mbao na mijengo. Mafanikio kwa mwaka 2008 upandaji miti ni kama ifuatavyo:

Jedwali la Hali ya Upandaji Miti mwaka 2008

Wilaya

Lengo

Mafanikio

Asilimia

Ulanga

1,500,000

1,170,000

78

Kilombero

1,500,000

1,100,000

73

Kilosa

1,500,000

1,365,000

91

Mvomero

1,500,000

1,050,000

70

Morogoro

1,500,000

1,010,000

67

Manispaa

150, 000

100,000

67

Jumla

7,650,000

5,795,000

76

Chanzo: Taarifa za Wilaya 2008

Kwa kipindi cha miaka mitatu miche 21,453,441 ilipandwa ambayo ni sawa na asilimia 93.5 ya lengo la upandaji wa miti 22,950,000 kwa miaka mitatu.

Wanyamapori na Utalii

Mkoa wa Morogoro una utajiri wa rasilimali za Wanyamapori. Halmashauri, Serikali Kuu, Wadau na wananchi wanashirikiana kuhifadhi kwa lengo la kukuza na kuendeleza utalii. Maeneo haya ya uhifadhi ni yale yaliyo jirani na Pori Tengefu la Selous, Mbuga za Taifa za Mikumi, na Udzungwa na eneo la ardhi Oevu la bonde la Kilombero ambalo lina wanyama, ndege na mimea adimu kama vile sheshe ambaye anakabiliwa na hatari ya kutoweka kwa sababu ya uharibifu wa maskani yake. Wapo pia mbega wekundu (Sanje mangabay) na mlima Bokela ambayo ni vivutio, katika mbuga ya Udzungwa, vyura wa Kihansi wasiopatikana pengine duniani na ndege ”Kilombero Weavers”.Vivutio vingine ni eneo la mazalia samaki la Boma Ulanga na Stieglers Gorge katika mto Kilombero.

Mkoa umeendelea kuhifadhi na kuwalinda Wanyamapori kwa manufaa ya Taifa na vizazi vijavyo.

Utalii

Watalii wengi hutembelea Mkoa wa Morogoro kwa nia ya kutembelea hifadhi za Mbuga za Mikumi, Udzungwa na pori tengefu la Selous.Aidha, shughuli za watalii zinazofanyika ni kuona vivutio hivi na uwindaji. Uwindaji wa kitalii huzipatia Halmashauri kati ya shilingi milioni 40-45 kwa mwaka.

Ufugaji nyuki

Ufugaji nyuki Mkoani Morogoro unakuwa kwa kasi kutokana na mikakati ya Serikali ya kukuza na kupunguza umaskini Tanzania (MKUKUTA) pamoja na FAMOGATA kwa lengo la kuongeza kipato na kuleta maisha bora. Takwimu za mwaka 2008 zimebainisha kuwepo jumla ya mizinga ya kisasa 28,521 na 25,762 ya kienyeji iliyozalisha jumla ya kilo 111, 165 za asali na kilo 58,798 za nta. Katika kipindi hiki jumla ya mapato kutokana na asali yalikuwa shilingi 338,457,620 na shilingi 65,620,000/= kutokana na nta.

Mazingira

Mkoa umefanikiwa kuhamasisha Serikali za vijiji kutunga sheria ndogo zinazozuia uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji. Kutungwa kwa sheria ndogo kumepunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uchomaji moto misitu na mapori na kuweza kuhamasisha upandaji miti na kuitunza. Mkoa tangu mwaka 2006 umefanikiwa kupanda miti zaidi ya hekta 18,000 hadi kufikia Desemba, 2008.

 

 

 

         
 
[ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, TEL: 026 - 2604237/2600973, FAX: 026 2601000