JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
     
 
     
KILIMO
 
[ Nyumbani ] au
 

 

Mkoa umeendelea na utekelezaji wa Mkakati wa Fanya Morogoro Ghala la Taifa (FAMOGATA). Utekelezaji wa mkakati huu unatokana na agizo la Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati alipofanya ziara Mkoani Morogoro tarehe 10/06/2006 na kuagiza Mkoa wa Morogoro uwe Ghala la Taifa. Mkakati wa FAMOGATA unalenga:-

  1. Uboreshaji wa Miundo mbinu, Usafirishaji na Mawasiliano.
  2. Kuongeza ufahamu, stadi na matumizi ya teknolojia kama vile matumizi ya matrekta makubwa, madogo, pikipiki na wanyamakazi.
  3. Kumuwezesha mkulima kupata bei nzuri ya mazao katika soko la nje na ndani.
  4. Kuongeza thamani ya mazao kwa njia ya usindikaji

Jedwali la Mazao ya chakula Mkoani Morogoro

Msimu

Eneo (ha)

Mavuno (Tani)

Mahitaji (Tani)

Ziada (tani)

Aslimia ya kujitosheleza chakula

2005/06

358,576

1,118,108

462,659

111,5 79

124

2007/08

404,612

1,117,573

476,010

163,908

134

Chanzo: Taarifa za Wilaya 2005-2008

 Msimu wa mwaka 2005 eneo lililolimwa mazao ya chakula ni hekta 358,576 na kuvuna tani 1,118,108. Mahitaji ya chakula kwa mwaka 2005 yalikuwa tani 462,659 za nafaka kulikuwa na ziada ya tani 111,579 za mazao makavu na mabichi.

Msimu wa mwaka 2008 eneo lililolimwa mazao ya chakula ni hekta 404,612 na kuvuna tani 1, 117,573. Mahitaji ya chakula yalikuwa tani 476,010 kwa mwaka na ikawepo ziada ya tani 163,908 za nafaka (Cereal equivalent). Mkoa ulijitosheleza kwa chakula kwa asilimia 100 na ziada kuuzwa nje ya Mkoa. Eneo lililolimwa mazao ya biashara ni hekta 50,584 na kuvuna tani 842,803 (2008) ukilinganisha na eneo la hekta 47,317 lililolimwa mwaka 2005.

MIFUGO NA UVUVI

Katika kipindi cha miaka mitatu jumla ya majosho 24 yalijengwa na 12 yalikarabatiwa. Huduma ya kinga kwa wanyama ilitolewa ambapo ng'ombe 389,387 walipata chanjo ya kujikinga na magonjwa mbalimbali kama Ndigana kali, Homa ya mapafu na Homa ya bonde la ufa.

Mbuzi 58,000 na kondoo 55,000 walipatiwa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo. Nguruwe 42,155 walipata kinga ya Magonjwa ya Minyoo. Chanjo na Tiba ya mifugo imeinua ufugaji na ulaji wa nyama ya Nguruwe. Kuku 939,635 walipatiwa chanjo dhidi ya mdondo wa kuku na ndui.

Mkazo pia uliwekwa kwenye kupata pembejeo na kote Wilayani zinapatikana kupitia maduka 16 yaliyopo. Aidha, machinjio 6 yamejengwa na kusaidia wananchi kupata nyama isiyo na madhara kwa afya za binadamu. Minada mipya 6 imeanzishwa pia kimefunguliwa kiwanda cha nyama eneo la Nguru ya Ndege ambacho kinaongeza ubora wa nyama na pato. Machinjio ya Kiwanda hicho ina uwezo wa kuchinja ng'ombe 250 na kuku 1,000 kwa situ.

 

 

         
 
[ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, TEL: 026 - 2604237/2600973, FAX: 026 2601000