| Utangulizi |
| |
Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero ina eneo la Kilomita za mraba 14,918 ambazo zimegawanyika kiutawala.
Kwa upande wa mipaka, Wilaya imepakana na Wilaya za Kilosa na Kilolo; na upande wa Kusini umepakana na Wilaya ya Ulanga. Kwa upande wa Mashariki imepakana na Wilaya ya Morogoro Vijijini na Magharibi imepakana na Wilaya za Njombe na Mufindi.
|
| |
| |
| UMBILE LA ARDHI |
| |
Hali ya hewa ya Wilaya hii ni ya joto mithili ya pwani kwa wastani wa 26 o – 32 o C . Wilaya ina vipindi viwili vya mvua ambavyo ni mvua za vuli na mvua za masika. Mvua za vuli huanza kunyesha mwezi Novemba na kuishia miezi ya Januari au Februari. Mvua za masika huanza mwezi Machi na kwisha mwezi Mei au Juni kila mwaka. Wastani wa mvua ni kati ya milimita 1200 hadi 1600. Kutokana na wingi wa mvua na maeneo mengi kuwa katika bonde la mto Kilombero, mara nyingi hutokea mafuriko katika maeneo mengi ya Wilaya hii.
Sehemu kubwa ya Wilaya ya Kilombero imo katika bonde la Mto Kilombero na kiasi kidogo kiko katika bonde la mto Rufiji na mbuga ya akiba ya wanyama ya Selous. Bonde la mto Kilombero linakingwa na milima ya Udzungwa ambayo pia ni Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa kwa upande wa Kaskazini. Milima hii imefunikwa na kupambwa na miti ya Miombo na pia baadhi ya wanyama ambao ni nadra kuwaona katika Hifadhi zingine za Taifa na hata maeneo mengine duniani. Milima ya Udzungwa ina urefu wa meta 1700 kutoka usawa wa bahari.
|
| |
| |
| |
IDADI YA WATU
|
| |
Kufuatana na taarifa za Sensa ya mwaka 2002, Wilaya ina jumla ya wakazi 321,611. Kati ya hao wanaume ni 162,214 na wanawake ni 159,397. Watu wenye uwezo wa kufanya kazi kulingana na sensa ya mwaka 2002 ni 180,531 ambao kati ya hao wanaume ni 91,458 na wanawake ni 89,073. Wilaya inaonekana kuwa na idadi kubwa ya wanaume kuliko wanawake hii ni kwa sababu wanaume wengi huja katika Wilaya kufanya kazi katika Kampuni ya Sukari Kilombero, kadhalika wanaume wengi huja na mifugo kutoka katika Wilaya na Mikoa mingine hasa ya Shinyanga, Arusha na Manyara, na wengine huingia katika Wilaya kwa shughuli za kilimo.
|
| |
| Utawala |
Wilaya ina Jimbo moja la uchaguzi ambalo ni Kilombero, .
Mhe. Goagoa
ndiye Mwenyekiti wa Halmashauri na
Bibi Rehema Madenge
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. |
| |
| Sekta ya Kilimo |
| |
Wilaya ina eneo la hekta 1,491,800. Eneo hilo linajumuisha pia sehemu ya Mbuga ya wanyama ya akiba ya Selous na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa pamoja na ardhi oevu ambayo ni sehemu ya bonde la mto Kilombero na inakuwa imejaa maji kwa kipindi kirefu cha mwaka.
Eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 445,896.
- Eneo linalolimwa kwa sasa ni hekta 114,672
- Eneo la misitu ni hekta 220,000.
- Eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni hekta 35,239
- Eneo linalolimwa kwa sasa ni hekta 557.
Asilimia 80 ya wakazi wa wilaya ya Kilombero hutegemea kilimo kwa chakula na biashara. Mazao yanayolimwa kwa ajili ya chakula ni: mpunga,mahindi,mhogo,ndizi, v/vitamu na Jamii ya Kunde. Mazao ya biashara ni miwa, ufuta, alizeti na mpunga pia unatumika kama zao la biashara
|
| |
|
|
Upatikanaji wa pembejeo. |
katika suala la pembejeo za kilimo mawakala wa pembejeo wamepata msukumo kutika uongozi wa wilaya na Wizara juu ya kuleta pembejeo katika maduka yao mapema ili wananchi waweze kuzipata kwa karibu, mapema na kwa wakati.
Kwa msimu wa 2007/2008 matrekta hamsini (50) yaliingia wilayani kutoka nje ya wilaya na zilisambazwa sehemu mbalimbali za wilaya kulingana na mahitaji. Kupitia mfuko wa Pembejeo wananchi waliweza kukopeshwa trekta saba (7) na uhamasishaji wa kuomba mikopo hiyo kwa wakulima na wafanyabiashara wengine unaendelea.
Maandalizi ya upatikanaji wa mbolea ya ruzuku kwa kutumia Mpango wa Hati Punguzo yamenafanyika. Jumla ya vijiji 50 kati ya 81 vimeteuliwa kutekeleza mpango huu. Kwa kutumia Mpango wa Hati Punguzo, kijiji cha Mkula kimeshaanza kutumia kiasi cha tani 25 za mbole aina ya Urea na tani 20 za Minjingu kwa ajili ya kuzalisha zao la mpunga kwa kilimo cha umwagiliaji.
Matatizo yanayokabili shughuli za kilimo:
Uzalishaji mdogo kutokana na sababu mbalimbali mfano uhaba wa zana za kisasa za kulimia, wanyama na wadudu waharibifu, magonjwa na uhaba na bei kubwa ya pembejeo.
Mikakati ya kuinua hali ya kilimo wilayani
Wilaya imejiwekea mikakati mbalimbali ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na kuinua hali ya maisha ya mkulima kwa kuzalisha ziada. Mikakati hiyo ni pamoja na;-
Kila mkulima azingatie kanuni za kilimo bora na kufuata kalenda ya kilimo.
Wataalam wa kilimo na mifugo vijijini kutumia vikundi vya wakulima na wafugaji na mashamba darasa (Farmers Field Schools).
Kuunda kamati za kuhimiza Kilimo
Kudhibiti magonjwa na wadudu waharibifu
Kuunda mfuko wa Pembejeo wa Wilaya
Kutoa elimu kwa jamii juu ya Uhifadhi na usindikajiwa mazao ya kilimo
Kuboresha na kuendeleza kilimo cha umwagiliaji
Kuendeleza kilimo cha wanyama kazi.
Kuboresha shughuli za ughani kwa Wakulima na Wafugaji. |
|
|
| Ushirika na Masoko |
| |
Katika mwaka wa fedha 2006/07 serikali ilitenga wastani wa shillingi bilioni moja kwa kila mkoa kwa lengo la kuwawezesha wananchi wa kawaida vijijini na mijini kiuchumi, ili kuongeza ajira na kipato. Matarajio ya serikali ni kuwawezesha wananchi katika vikundi na mtu mmoja mmoja wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji mali na biashara kupata mikopo yenye masharti nafuu itakayowapatia mitaji ya kujiendeleza katika shughuli zao na hivyo kujiondolea umaskini. Fedha hizo zitatolewa kupitia mfumo wa kibenki na mabenki yanayohusika na mpango huu ni NMB na CRDB kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa kutumia taratibu za kibenki.
Uundaji wa SACCOS
Wilaya ya Kilombero inazo jumla ya Tarafa tano, Tarafa hizo ni Mang'ula, Kidatu, Ifakara, Mngeta na Mlimba, kwa kipindi cha mwaka 2005 mpaka hivi sasa idara ya ushirika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imehamasisha wananchi juu ya uundaji wa vyama vya akiba na mikopo (SACCOS), na hatimaye kila Tarafa kuna vyama vya akiba na mikopo zaidi ya kimoja. Haya ni mafanikio makubwa kwa kuwa kupitia vyama hivi, wananchi wanaweza kupata mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za kiuchumi na kijamii ikiwa ni njia ya kuongeza kipato, kukuza ajira na kuinua hali zao za maisha.
Katika wilaya tuna idadi ya vyama vya ushirika wa mazao vya msingi 9 pamoja na Chama Kikuu 1, idadi kubwa ya vyama hivi ni Sinzia. Wilaya imeweka mikakati ya kuvifufua vyama hivi vya ushirika na tayari kuna mchakato wa kutathimini hali ya uchumi ya vyama husika, na maandalizi ya malipo yaliohakikiwa kwa wakulima wanaodai fedha zao za mazao katika Chama Kikuu cha Ushirika cha UKICU Ltd yanaendelea kufanyika.
Vyama vya ushirika wa akiba na mikopo SACCOS – katika Wilaya ya Kilombero Kitengo cha Ushirika kimefanikiwa kuwahamasisha wakulima, wafugaji, wavuvi na wafanyabiashara ndogo ndogo na wameweza kuanzisha jumla ya SACCOS 80 hii ikiwa ni ongezeko la SACCOS 45 kwa kipindi cha mwaka 2005 – 2008.
|
|
Elimu |
| |
Utekelezaji wa Maendeleo ya Elimu Wilayani unaenda sambamba na utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES), Sera ya Elimu na Mafunzo, Mikakati ya kuondoa umaskini pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 - 2010 ya chama tawala.
Ili kutekeleza mpango huu wa uboreshaji Elimu, Wilaya imejiwekea mikakati ifuatayo:
Kuandikisha watoto wote wenye rika stahili la kujiunga na Elimu ya Msingi.
- Kuboresha mazingira ya kutolea Elimu yakiwemo madarasa bora, na nyumba bora za walimu.
- Kuhakikisha upatikanaji wa walimu wenye Taaluma, utaalam na ari ya kuwawezesha watoto kujifunza kwa urahisi
- Kuendelea na jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa vifaa mbalimbali vya kufundishia na kujifunzia kama vile vitabu na zana mbalimbali.
Aidha mikakati mingine ya uboreshaji wa Elimu nchini ni kuhakikisha kuwepo kwa majengo ya kutosha katika shule za msingi, kama vile madarasa, nyumba za walimu, matundu ya vyoo, ofisi, bwalo na jiko kwa baadhi ya shule ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa samani za kutosha katika shule za ufundi.
|
| |
Elimu ya Awali |
|
Shule za awali ziko 140 na zina jumla ya watoto 6,940 kama ifuatavyo:
Mwaka wa 1 |
Mwaka wa II |
| Wav |
Was |
Jumla |
Wav |
Was |
Jumla |
2,172 |
2,143 |
4,315 |
1,259 |
1,366 |
2,625 |
|
Elimu ya Msingi
|
Wilaya ya Kilombero ina shule za msingi 150. Kati ya shule hizo tatu (3) ni za Watu Binafsi nazo ni Lupa na Kapolo zilizopo Ifakara Mjini na Papango iliyopo katika mji mdogo wa Mlimba. Shule hizo tatu za binafsi hutumia lugha ya kiingereza kama lugha ya kufundishia. Shule hizo zina jumla ya wanafunzi 82,651 wakiwemo wavulana 41,912 na Wasichana 40,739. |
| |
Hali ya uandikishaji wa wanafunzi katika shule za msingi katika wilaya ya Kilombero imekuwa ni ya kuridhisha. Takwimu zifuatazo zinaonyesha ongezeko la idadi ya wanafunzi katika shule hizo mwaka hadi mwaka. |
Jedwali la Uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza tangu mwaka 2006-2008:
Mwaka |
Tara
jiwa |
Wav. |
Was. |
Andiki
shwa |
Wav. |
Was. |
% |
2006 |
13,058 |
|
|
12,244 |
|
|
98.8 |
2007 |
14,071 |
|
|
13,202 |
|
|
98.8 |
2008 |
9001 |
4,504 |
4497 |
11,617 |
5,805 |
5,812 |
129 |
Aidha, uandikishaji wa watoto kuingia darasa la kwanza kwa mwaka 2008 uliongezeka kutokana na watu wengi kuingia katika Wilaya kwa shughuli za kilimo na ufugaji. |
Walimu wa Shule za Msingi |
|
Wilaya ya Kilombero ina jumla ya walimu 1,530. |
|
Elimu ya Sekondari |
Wilaya ya Kilombero ina Shule za Sekondari 38, kati ya hizo, 31 ni za serikali na shule saba (7) ni za watu binafsi na mashirika ya dini. Halmashauri ya Wilaya ina kata 19 na kila kata kwa sasa ina shule ya Sekondari na kata 7 zina shule za Sekondari zaidi ya moja ikiwa ni pamoja na shule zilizojengwa na tarafa kama ifuatavyo; kata ya Kidatu shule tatu (3), kata ya Ifakara shule nne (4), Mlimba shule tatu (3), Mchombe shule tatu (3), Mang'ula shule mbili (2), Kiberege shule mbili (2) na sanje shule (2). Kuanzia sasa mipango iliyopo ni kuendelea na juhudi za kujenga vyumba vya madarasa vya kutosha na pia kujenga Hosteli kwa kuanzia na watoto wa kike. |
| |
| Maji |
Halmashauri ikishirikiana na wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo kama vile shirika la Plan International - Ifakara na Serikali Kuu imeweza kupunguza tatizo sugu la maji wilayani ambapo inakadiriwa kuwa asilimia 66.97 ya wakazi wa Kilombero ambao ni 251,000 wanapata maji safi na salama. |
|
Changamoto
Katika utekelezaji wa shughuli za utoaji wa huduma ya maji tunakabiliana na changamoto zifuatazo;
- Watumiaji wa maji kuwa na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa kuwa na mifuko ya maji kwa ajili ya utoaji huduma endelevu.
- Uwezo mdogo wa kifedha kuweza kutimiza mahitaji ya watumiaji maji.
- Gharama kubwa za uendeshaji wa skimu za maji zinazotumia nishati ya umeme.
- Uhaba wa vitendea kazi mfano zana za kufanyia utafiti na kuchimbia visima na zana za ujenzi.
- Upungufu wa watumishi hasa mafundi sanifu.
- Ili kupambana na changamoto hizo Wilaya inaendelea kuwahamasisha wananchi ili wachangie na kuimarisha mifuko yao ya maji.
|
| Mifugo |
Utangulizi
Shughuli za ufugaji katika wilaya ya Kilombero ziliongezeka kwa haraka kuanzia mwanzoni mwa mwaka 1990. Wafugaji wengi walihamia hapa wilayani na mifugo yao kutoka mikoa ya Arusha, Mwanza, Tabora na Shinyanga na Mbeya. Aidha, katika kipindi cha hivi karibuni, baadhi ya wafugaji wameingia Wilayani wakitokea katika Bonde la Ihefu Mkoani Mbeya. Kumekuwepo pia na ongezeko kubwa la ufugaji wa ng'ombe wa maziwa, nguruwe, kuku wa asili
na wale walioboreshwa.
Pamoja na mifugo hiyo asili, baadhi ya wananchi wameanza kufuga ng'ombe wa maziwa pamoja na kuku wa mayai na wale nyama walioboreshwa.
|
| |
| |
| Viwanda, Biashara na Masoko |
Kitengo cha Biashara
Moja ya kazi ya kitengo cha Biashara ni kutoa vibali vya kufanyia biashara ambavyo huitwa leseni. Leseni hizi zimegawanyika katika makundi mawili , leseni za kawaida na leseni za Vileo.
atika kipindi cha kuanzia Julai 2005 hadi Septemba 2008, jumla ya leseni za biashara za kawaida 1,352 na leseni 407 za vileo zimetolewa
|
Viwanda
Wilaya ina viwanda vikubwa vitatu ambavyo ni Kiwanda cha Sukari ILOVO, Mgodi wa Umeme wa Kidatu na wa Kihansi. Aidha kuna Viwanda viwili vya maji ya Kunywa, kimoja kipo Ifakara na Kinaitwa Kilombero Maji Ltd na Kingine kipo Sanje katika tarafa ya Kidatu na kinaitwa SALMANS and Sons Company. Kuna mashine za kusaga na kukoboa mpunga zipatazo 150. Aidha kuna vikundi vingi vinavyojishughulisha na shughuli mbalimbali za ufundi kikiwemo kikundi cha akina Mama Ifakara (Ifakara Women Weavers Association –IWWA) ambao hujishughulisha na useketaji wa nyuzi za nguo.
Vipimo vya Lumbesa
Wilaya inaendelea na upigaji vita ununuzi na usafirishaji wa mazao kwa kutumia vipimo batili vya lumbesa. Kwa Halmshauri imetunga sheria ndogo ya kuzuia vipimo hivyo batili. Sheria hizo zimepitishwa na kikao cha Baraza kilichoketi mwezi Aktoba 2008 na sasa zitapelekwa kwa Waziri kwa ajili ya kupitishwa na zianze kutumika.
Changamoto
Pamoja na kupanda kwa gharama za maisha, ada za leseni za vileo ni viwango vya zamani mno kiasi kwamba thamani halisi ya ada hiyo ni ndogo sana ukilinganisha na wakati hivyo vilipowekwa.
Mkanganyiko mwingine uliopo ni kuwa biashara zenye mauzo yasiyozidi shilingi 20,000,000/- kwa mwaka leseni zake hutolewa bure. Kwanini leseni za vileo bado zinalipiwa ada. Huu ni mkanganyiko ambao unajitokeza wakati wa utendaji. |
| |
|
|
| |
| |
| AFYA |
Wananchi wa Wilaya ya Kilombero hupata huduma za afya kutoka katika vituo vipatavyo 44 kama ifuatavyo
|
| |
Kituo cha Huduma |
Idadi |
| 1 |
Hospitali za Mashirika ya Dini |
1 |
| 2 |
Hospitali za mashirika |
1 |
| 3 |
Vituo vya afya vya Serikali |
4 |
| 4 |
Zahanati za Serikali |
15 |
| 5 |
Zahanati za mashirika ya Umma |
4 |
| 6 |
Zahanati za mashirika ya Dini |
13 |
| 7 |
Zahanati za watu binafsi |
6 |
| Jumla |
44 |
|
| |
|
MMAM
|
Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
Ili kutekeleza agizo la Serikali la kuwa na zahanati katika kila kijiji, wilaya imepanga kujenga zahanati, vituo vya afya na nyumba za waganga kama ifuatavyo;
- Kupandisha hadhi zahanati 3 kuwa vituo vya Afya katika kata 3
Kujenga nyumba za watumishi 18 katika zahanati 18
- Kujenga nyumba 5 za watumishi katika vituo vya Afya 5
- Kununua na kusambaza vifaa vya kitaalam katika vituo vya Afya 8 na zahanati 18.
- Kuwapa watumishi mafunzo ya kujiendeleza Kupandishwa hadhi zahanati 9 kuwa vituo vya Afya
- Kujenga vituo vya Afya 8
- Kujenga nyumba za watumishi 15 katika vituo vya Afya 15
Malengo hayo ni kwa awamu ya kwanza kwani zahanati zinahitajika ni 54.
|
| |
Mikakati ya kuboresha huduma za Afya Wilayani:
- Kuanzisha usimamizi tegemezi kwa kupitia Kanda (cascade supervision system).
- Kuwapa mafunzo ya muda mfupi na mrefu watumishi waliopo kazini.
- Kuhamasisha jamii ili waweze kushiriki ujenzi wa zahanati mahali ambapo hakuna huduma hiyo.
- Kutoa mafunzo na kuhamasisha jamii juu ya utumiaji wa vyandarua vyenye dawa.
- Kuendeleza mashindano ya usafi wa mazingira katika ngazi zote.
- Kuhamasisha mama wajawazito kujifungulia katika vituo vya tiba.
- Kuongeza vituo vya huduma ya mkoba ili kuinua kiwango cha chanjo kwa akina mama na watoto kwa maeneo ambayo hayana huduma hiyo kwa sasa.
- Kuhakikisha kuna kata zote zinakuwa na vituo vya afya Serikalini
- Kuhakikisha kuwa kila kijiji kinakuwa na zahanati ya Serikali kama agizo la Serikali lilivyotolewa.
- Kuhakikisha kuwa kila kituo cha huduma za afya kina watumishi wa kutosha kwa mujibu wa Ikama.
|
| |
Malengoya Wilaya ifikapo 2010 imepanga kutekeleza yafuatayo;
- Kupandisha hadhi zahanati 12 kuwa vituo vya afya ifikapo 2010
- Kujenga vituo vya afya 3 Masagati, Kisawasawa na Mofu.
- Kujenga zahanati 56 kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na wananchi wenyewe.
- Kukamilisha ujenzi wa zahanati 5 za Matema, Ipinde, Udagaji, Mkangawalo na Ikule. Zahanati hizi zinatarajiwa kukamilika mwaka huu.
|
| |
| |
| |
| Barabara |
Wilaya ya Kilombero inahudumia miundo mbinu ya barabara zipatazo 29 zenye urefu wa kilomita 230.1. Barabara hizi pia ziko katika mgawanyiko ufuatao Kilomita 50.26 za barabara ni za changarawe na kilomita 180.84 ni za udongo. Wilaya ya kilombero vilevile inapitiwa na barabara za mkoa zenye urefu wa jumla ya kilomita 285 ambazo ni kilomita 75 kutoka Kidatu hadi Ifakara na kilomita 210 kutoka Ifakara hadi Taweta. Barabara hizi ziko chini ya wakala wa barabara Mkoa wa Morogoro (TANROADS).
Wilaya ya Kilombero inahudumia barabara zake kwa kutumia chanzo kikuu kimoja cha Fedha kutoka Mfuko wa Barabara kwa kuzifanyia matengenezo ya kawaida, matengenezo ya muda maalum, matengenezo ya sehemu korofi na matengenezo ya madaraja na makalvati.
Wilaya ya Kilombero inapitiwa na reli ya TAZARA inayotoka Dar es Salaam kwenda Zambia kupitia Mikoa ya Pwani, Morogoro, Iringa na Mbeya. Urefu wa reli inayopita katika eneo la wilaya ya Kilombero ni karibu kilomita 300. Reli hii imekuwa ni kiungo na kichocheo kikubwa cha maendeleo na kukua kwa uchumi katika wilaya hii. Miji mingi midogo na vijiji kando kando ya reli hii imekua kutokana na kuwepo kwa reli ya TAZARA. |
| |
| |
Hifadhi ya Mazingira
|
Sehemu kubwa ya Wilaya imo katika bonde la Mto Kilombero na kiasi kidogo kiko katika bonde la mto Rufiji na mbuga ya wanyama ya Selous ambayo ina wanyama wa aina mbalimbali. Kuna milima ya Udzungwa ambayo pia ni Hifadhi ya Taifa. Milima hii imefunikwa na miti ya Miombo na pia baadhi ya wanyama ambao ni nadra kuwaona katika Hifadhi zingine za Taifa. Kuna miti mbalimbali inayofaa kwa upasuaji wa mbao. Shughuli za uwindaji wa kitalii hufanyika katika vitalu viwili vya Uwindaji wa kitalii ambavyo viko katika bonde la Mto Kilombero. Vitalu hivi ni chanzo kimojawapo ambacho huliingizia taifa fedha za kigeni na pia Halmashauri hupata kati ya shilingi milioni 40 hadi 45 kila mwaka kutokana na ushuru wa uwindaji katika vitalu hivyo.
Wilaya pia ina misitu mitano ya Hifadhi. Misitu hiyo ni Iyondo, Udzungwa Scarp, Matundu, Mwanihana na Nyanganje. Wilaya ina jumla ya mito 38 inayotiririsha maji kwa kipindi cha mwaka mzima. Kutokana na kuwepo na maliasili hizo katika Wilaya, wananchi wengi wamepata fursa ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi na hivyo kupunguza umasikini kwa kutumia maliasili.
Misitu ya Hifadhi
Wilaya ya Kilombero ina maeneo ya misitu ya Hifadhi ya Serikali Kuu, Halmashauri na vijiji, vilevile Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa, Pori la akiba la Wanyama la Selous na maneneo ya kuhifadhi wanyamapori ya Bonde la Mto Kilombero.
Uchomaji moto
Wilaya ya Kilombero ni miongoni mwa Wilaya za Mkoa wa Morogoro zenye matatizo ya uchomaji moto.
Vyanzo vya moto hapa Wilayani vinatokana na shughuli zifuatazo;
- Utayarishaji wa mashamba
- Uwindaji wa wanyamapori kwa ajili ya nyama na nyara
- Wafugaji kwa ajili ya kutafuta nyasi mpya na kuangamiza wadudu waharibifu kama ndorobo.
- Watumiaji/wafanyabiashara wa mazao ya misitu – wapasuaji mbao, wachoma mkaa, wakataji kuni, warina asali na wavuvi.
- Watu wenye imani potofu kwamba mvua haiwezi kunyesha bila misitu na mapori kuungua au kushindana kupima umri wa mtu kwa kutumia moto.
Hifadhi ya vyanzo vya maji na faida zake
Wilaya ya Kilombero ina mito 38 ya kudumu. Mito hiyo mingi inaanzia Mkoa wa Iringa na Mbeya lakini bado kuna chemchem ambazo zinaanzia kwenye msitu wa Asilia wa Kilombero, misitu ya Hifadhi ya Serikali Kuu na Hifadhi ya Taifa ya milima ya Udzungwa,
Kutokana na kuhifadhi mazingira na hasa misitu, mito mingi iliyopo Wilayani imekuwa ikitiririsha maji yake mwaka mzima na hivyo kutumika katika shughuli mbalimbali kama vile kuzalisha umeme katika Migodi ya kufua umeme ya Kihansi na Kidatu na pia katika shughuli za umwagiliaji mashamba katika mashamba makubwa ya kuzalisha Sukari ya ILOVO na katika mashamba madogo ya wakulima. Aidha kuna miradi midogo ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji huko Mngeta kwenye shamba la Mpunga na katika kituo cha Masista wa Upendo Mbingu kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Mahenge.
Aidha mito hiyo imekuwa hifadhi ya viumbe hai kama vile samaki, mamba viumbe vingine vilivyopo majini.
|
| |
Utalii na Vivutio vya utalii katika Wilaya ya Kilombero
Wilaya ya Kilombero ina vivutio vingi kwa ajili ya utalii na utafiti, vivutio ambavyo vinaweza kuonekana ni kama ifuatavyo:-
Hifadhi yaTaifa ya Milima ya Udzungwa
Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ni Hifadhi katika Tanzania ambayo ina wanyama (Mbega Wekundu) ambao hawapatikani katika asehemu yoyote Duniani. Pia ina mimea ambayo haipatikani katika sehemu yoyote dunuani isipokuwa katika hifadhi hii pekee. Vivutio vingine ni Maporomoko ya Sanje, Nyani waitwao Sanje Mangabay, Kilele cha Mlima Bokela na wanyama wengine wengi.
Vyura wa Kihansi (Kihansi Spray Toad)
Vyura wa Kihansi waligunduliwa mwaka 1996 wakati wa zoezi la tathmini ya athari za Kimazingira wakati Ujenzi wa Mgodi wa kufua Umeme wa maji katika Mto Kihansi. Uvumbuzi wa vyura hawa mwanzoni ilifikiriwa kuwa ni jambo la kawaida na ujenzi wa mradi wa umeme ulidhaniwa kuwa hautakuwa na athari kubwa kwa vyura. Hata hivyo baada ya mgodi huo kuanza kazi mazingira na makazi ya asili ya vyura hao yalibadilika na idadi ya vyura hao ilianza kupungua kwa kasi. Hivi sasa inasadikiwa kuwa vyura hao wametoweka katika bonde la Mto Kihansi na waliochukuliwa ili kunusuru uhai wao bado wanatunzwa katika Bustani ya wanyama ya Toledo na Bronx huko Marekani. Aidha kwa sasa mazingira yanaandaliwa katika Bonde la Kihansi ili vyura hao waweze kurejeshwa katika makazi yao ya asili.
Bonde la Mto Kilombero
Wilaya ya Kilombero iko ndani ya Bonde la Mto Kilombero na sehemu nyingine katika mbuga ya wanyama ya Selous. Bonde la Mto Kilombero ni maarufu kwa shughuli za uvuvi na uwindaji wa kitalii. Pia kuna ndege wanaoitwa Kilombero Weever Bird ambao wanapatikana katika Wilaya ya Kilombero pekee hususan katika Bonde la Mto Kilombero.
Maeneo mengine ya vivutio ni yale yaliyoko katika Mbuga ya wanyama ya Selous kama vile maajabu ya eneo linaloitwa Boma Ulanga, Stiglers Gorge katika Mto Kilombero.
Msitu wa Hifadhi Asilia wa Kilombero
Hivi karibuni Wizara ya Maliasili na Utalii iliipandisha hadhi Misitu ya Hifadhi ya Kilombero Magharibi, Iyondo na Matundu kuwa Msitu wa Mazingira Asilia ya Kilombero na kuutangaza kuwa Eneo la Urithi wa Dunia katika Milima ya Tao la Mashariki. |
|
| Ardhi |
Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi
Halmashauri inaendelea kuandaa Mpango wa Matumizi Bora ya ardhi ili kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji katika vijiji. Mpaka sasa Wilaya ina vijiji 10 vyenye Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi. Aidha Wilaya kupitia Mpango wa Usimamizi wa Ardhi Oevu ya Bonde la Mto Kilombero-Ramsar Site vijiji 22 vinaandaa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi.
Upimaji wa Viwanja, Mashamba na Mpango wa Hati Miliki za Kimila
Wilaya ya Kilombero ni miongoni mwa wilaya 30 zilizoteuliwa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi kutekeleza mpango wa utoaji wa Hati za Kimila. Utekelezaji wa mpango huo umeanza katika vijiji 8 kati ya 22 vinavyokusudiwa. Jumla ya Hati Miliki za Kimila 254 zimeandaliwa na ziansubiri kusajiliwa na sambamba na ukamilishaji wa masjala ya Ardhi ya Wilaya. Viwanja na mashamba vilivyopimwa na kukamilihwa katika kipindi cha 2005/06-2007/08 ni kama ifuatavyo;
Jedwali Na. Upimaji wa Viwanja, Mashamba na Hati Miliki
| |
Eneo la Upimaji |
Idadi |
1 |
Viwanja Vilivyopimwa |
542 |
2 |
Mashambayaliyopimwa |
8 |
3 |
Hati miliki za viwanja |
180 |
4 |
Hati Miliki za Mashamba |
6 |
5 |
Hati Miliki za Viwanja zinazosubiri |
362 |
6 |
Hati Miliki za mashamba zinazosubiri |
2 |
Jitihada za kupunguza Migogoro ya Ardhi -
Kuendelea na Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi, kwani katika vijiji vilivyo na Mpango huo migogoro ya mipaka imetatuliwa kwa kiasi kikubwa.
-
Halmashauri imeanzisha Mabaraza ya Ardhi kuanzia ngazi ya kijiji hadi kata na kuhakikisha yote yanafanya kazi.
-
Halmashauri inajitahidi kutoa Elimu ya Ardhi kwa jamii ili uelewa wa mtu mmoja mmoja usaidie kupunguza migogoro ya ardhi.
- Halmashauri inajitahidi kupima maeneo kwenye makazi holela ili kila kipande cha ardhi kitambulike mipaka yake kisheria na hivyo kupunguza migogoro ya mipaka ya kienyeji miongoni mwa makazi holela
Mikakati ya wilaya katika kuboresha makazi na maendeleo ya ardhi.
-
Kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa Hati Miliki za viwanja.
-
Kuhakikisha kuwa vijiji vyote ambavyo havijapimwa vinapimwa. Kazi ya kuhakiki mipaka hiyo imeanza.
-
Kuendelea na zoezi la Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi kwa ajili ya kupunguza migogoro baina ya watumiaji wa ardhi. kazi hiyo inaendelea.
-
Kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuwa na Hati Miliki za kimila zitakazowawezesha wananchi kuzitumia kukopa katika vyombo vya fedha
|
| |
Uvuvi
Uvuvi unaotumika hapa Wilayani ni Uvuvi wa nyavu, ndoana, Uvuvi wa mitego na uvuvi wa asili (Ndanga). Pato la samaki hapa Wilayani limepungua kutokana upungufu wa mvua, Uvuvi haramu na uharibifu unaosababishwa na makundi ya mifugo.
Takwimu za upatikanaji wa samaki 2005-2007
Na |
Mwaka |
Kiasi (Tani) |
Thamani (Tsh) |
1 |
2005 |
201 |
198,990,000 |
2 |
2006 |
199 |
238,800,000 |
3 |
2007 |
259 |
5,827,500,000 |
Aidha kuna jumla ya mabwawa 56 yaliyochimbwa na wananchi kwa ajili ya ufugaji wa samaki.
Mabwawa ya asili katika Mto Kilombero.
Kuna jumla ya Mabwawa ya asili ishirini na nne (24) katika bonde la mto Kilombero kwa upande wa wilaya ya Kilombero ambayo ni Chagugu, Nakwiri, Mbugasiri, Lumemo, Kumbalamungu, Mkweka, Kinyasi, Kitope, Kahema, Rufiji, Kitandala, Ipundi, Kihata, Naupe, Sangulingu, Luta, Mkwajuni, Lukanga, Kibasila, Igawilo, Mkombeyi, Ndolo, Ngapemba, Masufunia. Mabwawa haya ni muhimu kwa kuwa ni mazalia ya viumbe hai wa majini wakiwemo samaki.
|
| |
Ufugaji nyuki
Ufugaji nyuki katika Wilaya ya Kilombero umekuwa na mwitikio mkubwa kwa mtu mmoja mmoja na vikundi. Kuna jumla ya mizinga elfu nne (4000) katika Wilaya. Mizinga 500 kati ya hiyo ni ya kisasa na 3500 ni ya Asili. Kuna jumla ya vikundi 25 vya wafugaji nyuki vilivyoanzishwa hapa Wilayani. |
| |
| |
|