| Utangulizi |
| |
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ni kati ya Wilaya 5 za Mkoa wa Morogoro. Wilaya ipo kaskazini mashariki ya Mkoa wa Morogoro, kati ya Latitudo 8°00' na 6°45' kusini mwa ikweta na pia kati ya Longitudo 37°00' na 38°30' Mashariki. Wilaya imepakana na Mkoa wa Pwani kwa upande wa mashariki, na Wilaya ya Kilombero upande wa kusini na upande wa magharibi na kaskazini imepakana na Wilaya ya Mvomero. Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ina ukubwa wa km. za mraba 11,925. Asilimia 60% ya eneo hilo ni mapori, misitu na wanyama ikiwa ni pamoja na mbuga za wanyama, Pori la Selous (Selous Game).
|
| |
| |
| |
| |
| UMBILE LA ARDHI |
| |
Umbile la ardhi ya halmashauri ya Wilaya ni mchanganyiko wa milima, mabonde na tambarare. Maeneo ya milima yamechukuliwa na milima ya Uluguru na mabonde na tambarare yamegawanywa na mito inayoanzia milimani, baadhi ya mito hiyo ni Ruvu, Ngerengere na Mgetakafa.
Hali ya hewa ya Wilaya ya Morogoro ni nyuzi joto kati ya 20°sentigredi hadi 30°sentigredi. Wilaya inapata mvua za wastani wa mm 300 hadi 600mm maeneo ya tambarare na maeneo ya milimani.
Mvua za masika huanza kunyesha mwezi Machi hadi Mei na ukame kuanzia mwezi Januari mpaka Februari, ambapo Agosti mpaka Novemba ni kipindi cha joto, na kipindi cha baridi ni Juni hadi Julai. |
| |
| |
| |
| IDADI YA WATU |
| |
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002 Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ilikuwa na jumla ya watu 263,920 ambapo wanaume walikuwa 129,285 na wanawake 134,635 na Kaya 56,723. Halmashauri ya Wilaya Morogoro inakadiriwa kuwa na ongezeko la watu kwa asilimia 2.6 kila mwaka. Kutokana na ongezeko la watu kuwa asilimia 2.6 kwa mwaka, mwaka 2007 Halmashauri ya Morogoro inakadiriwa kuwa na jumla ya watu 283,858
|
| |
| Utawala |
Halmashauri inamajimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Morogoro Kusini na Morogoro Kusini Mashariki. Mh
Hamza Mfaume ndiye Mwenyekiti wa Halmashauri na Bw E. Munisi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. |
| |
| Sekta ya Kilimo |
| |
Asilimia 90% ya wakazi wa wilaya ya Morogoro ni wakulima, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ina eneo la kilometa za mraba 11,925.75 ambazo ni sawa na hekta 1,192,575. Eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 447,000, eneo linalolimwa ni hekta 94,160.85, eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni hekta 28,075, eneo linalomwagiliwa kwa sasa ni hekta 161.5.Eneo linaiojengewa miundo mbinu ambayo inatarajiwa kukamilika katika msimu wa kilimo wa 2008/2009 ni hekta 910
|
| |
| Maeneo ya uzalishaji |
Katika kutekeleza mpango huu, Halmashauri iLiainisha maeneo maalumu ya kuanzia katika mpango huu kwa mwaka 2007/2008.
Maeneo yamegawanywa katika Kanda tano, zenye Kata kumi na moja (11) na vijiji 44 kati ya vijiji 132 vya Wilaya ya Morogoro, Mazao yaliyohusishwa ni Mpunga, Mahindi na jamii ya mikunde.
|
|
|
Upatikanaji wa pembejeo. |
Pembejeo zilipatikana vizuri katika maduka ya mawakala wa pembejeo walioko mjini. Pembejeo zenye ruzuku pia upatikanaji wake ulikuwa mzuri, wakulima walipata mahitaji yao kupitia mawakala.
Pembejeo za ruzuku zilizopatikana ni mbolea aina ya urea tani 76, DAP tani 20 na mbegu za mahindi 2.2. Ambazo zilinunuliwa na mawakala na kuuzwa kwa wakulima. Wakulima walipata pembejeo kupitia mawakala waliopo vijijini na mjini.Vile vile wakulima katika vijiji 15 vya wilaya waliweza kuzalisha mbegu bora za mahindi tani 10 na kuwauzia wakulima wenzao kwa bei nafuu .Hii iliwezekana baada kupata mafunzo ya kuzalisha mbegu bora chini ya mradi wa ASDP. |
| |
| Ushirika na Masoko |
| |
Halmashauri ya wilaya ina jumla ya vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa vilivyoandikishwa kumi na vinne vyenye jumla ya wanachama 4,232 na jumla ya hisa Tsh. 141,691,365/= na akiba ya Tshs 1,124,030,232/= pamoja na amana zenye thamani ya jumla ya Tsh. 267,235,454/=.
Vilevile halmashauri ina vyama vya mazao vitatu ambavyo hununua na kuuza mazao. |
| |
| Na |
Aina Ya Chama |
Idadi Ya Wanachama |
Jumla |
| Me |
Ke |
Vikundi |
| 1 |
SACCOS |
2,708 |
1,381 |
142 |
4,231 |
| 2 |
Mazao |
127 |
20 |
- |
147 |
| 3 |
Shughuli Maalum |
27 |
- |
- |
27 |
| Jumla |
2,885 |
1,401 |
142 |
4,398 |
|
| |
| Elimu |
| Elimu ya Awali |
Halmashauri ya Wilaya inayo madarasa ya Elimu ya Awali 122 (mia moja na ishirini na mbili) yanayoendeshwa chini ya Usimamizi wa shule zetu za Msingi Wilayani kati ya madarasa hayo darasa 1 linasimamiwa na kanisa Katoliki Mikese. Jumla ya wanafunzi 4,868 wakiwemo wavulana 2,443 na wasichana 2,425 wanasoma katika madarasa hayo. Mara wamalizapo Elimu hiyo hujiunga na Elimu ya Msingi.
Shule zilizobaki 23 hazijaanzisha nadarasa ya elimu ya awali kutokana na sababu zifuatazo:
Uhaba wa waalimu shuleni
Mwitikio hafifu wa wananchi katika uanzishaji wa madarasa ya elimu ya awali |
|
Elimu ya Msingi |
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ina shule za msingi 144 (mia moja arobaini na nne) zinazomilikiwa na Serikali na Shule moja inayomilikiwa na shirika la dini hivyo kuifanya wilaya kuwa na jumla ya shule 145 (mia moja arobaini na tano) za msingi.Katika shule hizo 145 za msingi wapo jumla ya wanafunzi 63,352. Katika Idadi hiyo wasichana ni 30,008 na wavulana ni 33,344. |
Jedwali lifuatalo linaonyesha hali ya uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza 2005 – 2008.
|
MWAKA |
MAKISIO |
IDADI HALISI |
% |
2005 |
18,082 |
17,975 |
99.41 |
2006 |
8,774 |
7,859 |
89.5 |
2007 |
9,130 |
9,131 |
100 |
2008 |
8,911 |
8,557 |
96 |
Chanzo: Taarifa za Idara ya Elimu, 2008
Takwimu hizi zinaonesha kwamba Halmashauri ya Wilaya katika mwaka 2007 iliandikisha wanafunzi wote waliokuwa na umri wa kwenda shule |
| |
| Maji |
Upatikanaji wa Maji
Wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wanapata huduma ya maji kutoka katika vyanzo vya maji kutoka vyanzo mbalimbali ambapo inasimamiwa na Halmashauri ya Wilaya. Vyanzo hivyo ni miradi ya Maji mserereko, visima virefu, visima vifupi, mabwawa mito pamoja na miradi ya uvunaji maji ya mvua.
Mahitaji halisi ni lita za ujazo 7.918 milioni kwa siku, wakati kiasi halisi cha maji kinachopatikana ni lita za ujazo 4.909 milioni kwa siku sawa na asilimia 62 tu ya wakazi wa Halmashauri ya Morogoro wanaopata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao umbali usiozidi mita 400.
Kiasi hiki kimeongezeka kutoka lita 2.455 milioni kwa siku mwaka 2004 hadi kufikia liata za ujazo 4.909 milioni kwa siku, ongezeko hilo ni sawa na asilimia 50. Ongezeko hili limetokana na juhudi za Halmashauri kwa kushirikiana na Wafadhili na wananchi kuongeza idadi ya visima na miradi ya maji ikilinganishwa na idadi iliyokuwepo kwa mwaka 2000 |
| |
| Changamoto |
-
Kuboresha huduma ya maji safi na salama kwa kushirikiana na Wizara ya maji.
-
Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's), Makampuni binafsi na ya Kiserikali, Taasisi za Kiserikali (DDCA) na zisizo za Kiserikali pamoja na wadau mbalimbali.
-
Kuendelea kutafuta na kuvutia wafadhili katika miradi ya maji ili tuweze kuboresha na kuifanyia matengenezo miradi iliyoharibika hasa ya mserereko ambayo inatoa matokeo haraka na inaweza kuhudumia vijiji zaidi ya kimoja.(Quick wins )
-
Kuendesha miradi ya maji ya jamii kwa kutumia jumuia za watumiaji maji. (WUA) zilizosajiliwa kisheria au mawakala.
-
Halmashauri kupitia timu ya uhamasishaji masuala ya maji na usafi wa mazingira ya wilaya (DWSST) kwa kushirikiana na shirika la EEPCO pia WATSANET imeweza kuunda na kusajili jumuiya mbili (2) za watumia maji (WUA) kati ya 6 zilizohitajika. Hata hivyo jitihada za kukamilisha jumuiya zilizobaki zinaendelea pamoja na kuhamasisha vijiji vingine vinavyotumia kamati za maji kuweza kubadili mfumo wa uendeshaji.
-
Kuhakikisha kuwa vyombo vinavyoendesha miradi ya maji jamii vinapatiwa mafunzo juu ya usimamizi na uendeshaji ili miradi hiyo iwe endelevu.
-
Kuhamasisha jamii juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na usafi wa mazingira.
-
Kutoa elimu kwa jamii juu ya utaratibu na kanuni za uchimbaji visima ili kudhibiti uchimbaji holela, pia kudhibiti matumizi ya maji kwa kuwapatia Water right wale wanaovuna maji zaidi ya kiwango kilichowekwa na Wizara.
|
| |
| Mifugo |
Idadi ya Wafugaji na Mifugo
Wilaya ya Morogoro ina jumla ya wafugaji 3,263 wanaomiliki mifugo kama ifuatavyo: Ngo'mbe wa kienyeji 133,967 ng'ombe wa maziwa 2,527 Mbuzi 28,986, Kondoo 14,200, Nguruwe 453, Kuku wa asili 431,782, Bata 2,029 Mbwa 2,011.
Utengaji Maeneo ya Ufugaji
Wilaya inaendelea na kazi ya kutenga maeneo ya malisho katika Vijiji vya Kongwa, Tulo, Kisaki Kituoni, Mikese, Kisanga Stendi, Seregete A na B pamoja na Mvuha. Lengo ni kupunguza migogoro ya Wakulima na Wafugaji katika maeneo hayo.
Hali ya Mifugo
Hali ya mifugo kiafya ni nzuri. Malisho na maji yanapatikana japo yamepungua kwa kipindi hiki kutokana na ongezeko kubwa la mifugo iliyovamia katika maeneo mbalimbali wilayani.
Shughuli za Maendeleo ya Mifugo zinazotekelezwa:
Shughuli zinazotekelezwa katika kuboresha maendeleo ya mifugo ni:-
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu mbinu za ufugaji bora na uboreshaji mifugo
- Kutoa tiba na kinga kwa magonjwa ya milipuko.
- Kufanya ukaguzi wa nyama
- Kudhibiti magonjwa ya kupe na ndorobo
- Kuendeleza nyanda za malisho kwa kuboresha majosho na malambo
- Kusimamia minada na kukusanya mapato ya Halmashauri
- Kutoa mafunzo kwa wafugaji 30 juu ufugaji wa kiabiashara
Huduma za Mifugo
a) Majosho
Wilaya ina jumla ya majosho 8 yote yanafanya kazi. majosho 2 ya watu binafsi na 2 ya taasisi za serikakali na majosho 4 yanayomilikiwa na jamii katika vijiji vya Kisanga stendi,Diguzi,Kongwa na Tununguo.
b) Malambo
Wilaya ina jumla ya malambo 4 kati ya hayo malambo 3 yanafanya kazi na 1 halifanyikazi
c) Uboreshaji mifugo
(i) Matumizi ya madume bora
Wilaya inaendelea kufanya uboreshaji wa kuku, mbuzi, na ng'ombe kwa kusambaza majogoo, madume bora ya ng'ombe na mbuzi kwenye Vijiji vya Kata za Mikese,Mvuha na Ngerengere.
Unenepeshaji Ng'ombe
Wafugaji wengi wamezoea kuuza mifugo yao bila ya kunenepesha, kwa msimu wa 2008 /2009 Wilaya imelenga kufundisha jumla ya wakulima 30 kutoka vijiji vya Kongwa,Tulo na Diguzi, kila kijiji wafugaji 10 juu ya utaalamu wa unenepeshaji wa ng'ombe. Kila baada ya miezi mitatu ng'ombe 100 watakuwa wamenenepeshwa na kuuzwa hivyo kuongeza tija kwa wafugaji na kuondoa tabia ya kuchunga badala ya kufuga.
Mashamba ya mifugo
Mashamba ya mifugo yaliyopo Wilayani ni 4 na yanajumuisha ranchi za uzalishaji wa mifugo (LMU) Magereza pamoja na mashamba ya watubinafsi ya watu binafsi na serikali |
Na: |
Jina La Shamba |
Mahali Lilipo |
1 |
LMU |
Ngerengere |
2 |
KFS (Magereza ) |
Mkambarani |
3 |
Salmiin |
Ngerengere |
4 |
Mfinanga |
Ngerengere |
Chanzo: Taarifa za Kilimo, 2008 |
| |
| Viwanda, Biashara na Masoko |
Hali ya Viwanda
Kitengo cha Viwanda na Biashara na Masoko kinatoa huduma kwa wafanya biashara wenye lengo la kuanzisha na kuwekez biashara za aina mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, zenye mwelekeo wa kiviwanda, na biashara nyinginezo.
Tangu mwaka 2005 hadi Novemba 2008 kumekuwa na ongezeko la huduma mbalimbali za kibiashara kutokana na upatikanaji wa mitaji kama ilivyoainishwa kwa kigezo cha miaka tofauti.
Matumizi ya Vipimo Halali
Katika kutekeleza agizo la matumizi ya vipimo halali kama ilivyoelezwa katika sheria Namba 20 ya mwaka 1982 katika maeneo mbalimbali ya biashara Halmashauri ya Wilaya ilichukua hatua ya kuwaandikia Uongozi wa Kata zote kusisitiza matumizi ya vipimo halali katika biashara.
Vilevile wakala wa Vipimo wa Mkoa ametekeleza agizo la ukaguzi wa vipimo katika maeneo mbalimbali ya biashara ili kuzuia matumizi ya vipimo visivyo sahihi. |
| |
| |
|
|
| |
| |
| AFYA |
Hali Ya Afya
Halmashauri inatoa huduma za afya ya msingi tiba katika ngazi ya vijiji, kata na Wilaya.
Halmashauri haina hospitali ya wilaya hivyo wagonjwa toka vituo vya afya hupata rufaa kwenda hospitali ya Mkoa kwa ajili ya matibabu zaidi. Hali hii inasababisha msongamano mkubwa katika hospitali hiyo. Wagojwa husafiri muda mrefu kufuata huduma hiyo, aidha baadhi ya wagonjwa hushindwa kabisa kumudu kulipia gharama za usafiri huo.
Halmashauri hushirikisha Jamii katika utoaji wa huduma za afya kwa kuunda Bodi ya Afya ya Wilaya, Kamati za Afya katika Vituo vyote vya Afya na Zahanati na kuanzisha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF). Mfuko wa Afya ya jamii kaya hulipia fedha Tsh 5,000/= na kuiwezesha kaya hiyo kutibiwa katika Kituo cha Afya au zahanati kwa mwaka mzima. Hadi Septemba 2008 kaya zipatazo 14,006 zimeshajiunga na mfuko huo na kuchangia kiasi cha Tsh. 70,030 |
|
Malengo |
Kununua madawa/vifaa muhimu na kusambaza katika vituo vyote vya tiba kwa wakati
Kujenga hospitali ya wilaya ifkapo 2012
Kujenga vituo vya tiba katika kila kijiji ifikapo 2017
Kukarabati/kupanua majengo ya huduma za afya
Kuongeza idadi ya watumishi wenye taaluma kutoka 43% ya sasa hadi 90 ifikapo 2011
e) Kusimamia kwa karibu na kufanya mafunzo kazini kwenye vituo vyote vya huduma ili kuongeza uelewa wa watumishi
f ) Kushirikisha wadau wote wanaojishughulisha na utoaji wa huduma za afya hasa katika Uhifadhi, Utunzaji na Usafi wa mazingira na katika
uboreshaji na ujenzi wa vituo vya huduma
g) Kuinua kiwango cha usafi na ubora wa majengo ya biashara na maeneo yanayo uza vyakula na madawa.
Watumishi:
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imeendelea kuwa na upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali kama inavyoonesha katika jedwali: |
AINA YA KADA |
MAHITAJI |
WALIOPO |
PUNGUFU |
Daktari |
1 |
1 |
0 |
Daktari Msaidizi |
4 |
4 |
0 |
Daktari msaidizi meno |
1 |
1 |
0 |
Afisa Tabibu |
126 |
56 |
70 |
Afisa Tabibu meno |
3 |
1 |
2 |
Afisa Muuguzi |
8 |
6 |
2 |
Muuguzi mkunga |
126 |
50 |
76 |
Fundi sanifu maabara msaidizi |
38 |
8 |
30 |
Afisa afya |
25 |
13 |
12 |
Katibu wa Afya |
1 |
1 |
0 |
Fundi sanifu maabara |
3 |
2 |
1 |
Fundi sanifu Xrays |
1 |
1 |
0 |
Afisa Ustawi wa jamii |
1 |
0 |
1 |
Jumla |
338 |
144 |
194 |
|
| |
| Idadi ya vituo vya tiba |
|
Halmashauri ina vituo 63 vya tiba kati ya hivyo vituo vya Afya 3 ( vyote vya serikali), zahanati 42 (za serikali), zahanati 8 za Taasisi, zahanati 11 za Madhehebu ya Dini na zahanati 2 za binafsi. Halmashauri haina Hospitali ya Wilaya. Katika mpango wa MMAM tunatarajia kujenga hospitali ya wilaya na kujenga/kupanua vituo vya afya 22 na kujenga zahanati mpya 68 ifikapo 2017 katika kutekeleza agizo la kila kijiji kuwa na zahanati na kata kuwa na kituo cha afya.
|
| |
| |
| Changamoto |
Ukosefu wa Fedha kwa ajili ya kununulia vifaa muhimu vya kutolea huduma , kulipa masurufu ya watumishi wanaofanya kazi za ziada ukizingatia uhaba wa watumishi uliopo
Uhaba wa watumishi wenye taaluma mbalimbali inaotokana na watumishi wengi kukataa kufanya kazi katika sehemu zenye mazingira magumu hivyo kuacha kazi wakipangiwa kufanya kazi huko
Ukosefu wa nyumba za watumishi katika vituo karibuni vyote vya kutolea huduma, hali hii uongeza mazingira ya kazi kuwa magumu zaidi hivyo kuwa kichocheo hasi kwa watumishi.
Uhaba wa Madawa na Vifaa katika vituo vya tiba hali inayoathiri utoaji huduma bora kwa jamii
Ukosefu wa vyombo vya Usafiri wa uhakika kwa ajili ya usimamizi wa huduma na kwa watumishi hasa wale watoao huduma za mkoba na wale wanaohitajika kusimamia usafi wa mazingira katika jamii
Miuundo mbinu nduni ambayo hunasababisha usafirishaji wa wagonjwa, usambazaji wa madawa na vifaa muhimu kuwa mgumu hasa wakati wa masika
Uelewa mdogo wa jamii juu ya wajibu wao katika utoaji huduma za Afya na utunzaji wa afya zao
Hali duni za maisha ya wananchi ( Kipato kidogo, chakula duni , nyumba dun ink)
Ongezeko kubwa la wagonjwa wa ukimwi na waathirika wa ukimwi. |
| |
| Barabara |
Hali ya Barabara
Halmashauri inashughulikia ujenzi, ukarabati, matengenezo ya muda maalum na ya kawaida katika mtandao wa barabara zote zilizomo wilayani zenye urefu wa jumla ya Km 891 na madaraja/vivuko vilivyomo katika barabara hizo.
Mtandao wa Barabara na hali yake hadi Desemba 2008
Wilaya ina mtandao wa barabara zenye jumla ya Km 1,062.5 ikiwa ni barabara za lami, changarawe na udongo, kati ya hizo km 891 hutunzwa na Halmashauri ya wilaya na km 171.5 ni barabara Kuu na za Mkoa zinazohudumiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS). Hata hivyo wilaya humudu kutengeneza Km 339 tu kati ya Km 891.
|
| |
| Urefu wa barabara zilizopo Wilayani |
Na |
Aina ya barabara |
Vijiji (Km) |
Wilaya (Km) |
1 |
Udongo |
463.3 |
0 |
2 |
Changarawe |
0 |
364 |
3 |
Lami |
0 |
63.5 |
|
| |
| Hifadhi ya Mazingira |
(i) Hali ya Utunzaji Mazingira:
Uchomaji moto: Mpango mkakati wa kuzuia moto kati ya Halmashauri ya Wilaya na Wizara ya Maliasili unaandaliwa kwa kuanzisha Brigedi za kuzuia moto Wilayani.
Upandaji Miti
Katika uendelezaji wa hifadhi ya misitu na vyanzo vya maji kwa kipindi cha 2006/2007 na 2007/08 Halmashauri ya wilaya ilijiwekea lengo la kupanda miche ya miti 2,458,108 katika maeneo yake. Halmashauri ya Wilaya imeweza kupanda miche ya miti ipatayo 2,015,000 katika maeneo yaliyotajwa katika majedwali yafuatayo: |
| |
| Mikakati |
Mikakati:
Wizara ya Mali Asili na Utalii ipo katika hatua za mwisho kutangaza Misitu ya Milima ya Uluguru kuwa Hifadhi Asilia,
Kuendelea kuhamasisha na kuelimisha wananchi kuhusu ushirikishwaji wa utunzaji wa misitu na mazingira kwa ujumla,
Kufanya doria shirikishi kwa kutumia wananchi walio katika maeneo ya mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu,
Kuhakikisha kwamba wananchi wanaondokana na umaskini kutokana na rasilimali zinazowazunguka.
Kuongeza idadi ya miti itakayopandwa kwa mwaka 2008/09 kufikia miti 1,500,000
(iv) Changamoto
Ukosefu wa Fedha kwa ajili ya kununulia vifaa muhimu vya kutolea huduma, kulipa masurufu ya watumishi wanaofanya kazi za ziada ukizingatia uhaba wa watumishi uliopo
Uhaba wa watumishi wenye taaluma mbalimbali
Ukosefu wa nyumba za watumishi vijijini
Ukosefu wa vyombo vya Usafiri wa uhakika
Uelewa mdogo wa jamii juu ya wajibu wao katika kuhifadhi mazingira
Hali duni za maisha ya wananchi (hii husababisha uchomaji ovyo kwa Mkaa, kuchoma moto kwa ajili ya uwindaji |
| |
| Ardhi |
Utayarishaji wa mpango shirikishi wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji:
Jumla ya Vijiji vitano (5) katika Kata 3 Tarafa mbili 2 vimetayarishiwa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji.
Vijiji hivyo ni kama inavyoonyeshwa katika Jedwali hapa chini |
| |
NA. |
TARAFA |
NA. |
KATA |
NA. |
VIJIJI |
1. |
Ngerengere |
1. |
Ngerengere |
1 |
Kiwege |
2. |
Mikese |
2. |
Tununguo |
2 |
Mlilingwa |
| 3 |
Kisanga Stand |
| 3 |
Mikese |
4 |
Fulwe |
| 5 |
Muhungamkola |
|
| |
| Upimaji viwanja, Idadi ya vyeti na Hati zilizotolewa |
Upimaji viwanja
Upimaji wa viwanja 118 umefanyika na kukamilika katika mji mdogo wa Ngerengere.
Mchoro (Layout Plan) wenye jumla ya viwanja 451 katika eneo la Kiburumo, Ngerengere umeandaliwa na kupata kibali cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kazi ya upimaji wa viwanja hivyo imeshafanyika. Kazi iliyopo sasa ni kukamilisha ramani ya upimaji (Survey plan) na kupeleka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupata kibali cha Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani. |
| |
| Utoaji hati na vyeti vya ardhi |
Katika kipindi cha 2005/06 – 2007/08 jumla ya hati miliki za mashamba 18 zimetolewa na hakuna hati na vyeti vya ardhi vilivyotolewa
Malengo ya 2008/09
- Kuandaa mchoro (Layout Plan) wa viwanja 690
- Upimaji viwanja 690 katika maeneo yafuatayo:-
- Mtamba 118
- Duthumi 192
- Kisaki 290
- Fulwe 500
- Kingolwira 90
- Kutoa hati kwa viwanja 690
Utoaji wa Hati Miliki:
Mashamba 18 yamepimwa na hati miliki kuandaliwa na kupelekwa kwa Kamishna wa Ardhi |
| |
| Uendelezaji wa miji midogo |
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ina jumla ya Vijiji 132 yenye Miji midogo sita (6) inayotambulika kisheria.
Katika kudhibiti ujenzi holela katika Miji midogo ndani ya Halmashauri ya Wilaya Morogoro, michoro miwili ya upimaji wa viwanja (layout plan) wenye jumla ya viwanja 451 katika eneo la Kiburumo, Ngerengere imeandaliwa na kupata kibali cha upimaji kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pia viwanja 90 vimepimwa Kingolwira. Michoro imewasilishwa kwenye vikao vya Baraza kwa ajili ya kupitisha ramani (Survey plan) na kupelekwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kupata kibali. |
| |
| |
| |
|