Wilaya ya Morogoro ni kati ya Wilaya 5 za Mkoa wa Morogoro. Wilaya ipo kaskazini mashariki ya Mkoa wa Morogoro, kati ya Latitudo 8°00' na 6°45' kusini mwa ikweta na pia kati ya Longitudo 37°00' na 38°30' Mashariki. Wilaya imepakana na Mkoa wa Pwani kwa upande wa mashariki, na Wilaya ya Kilombero upande wa kusini na upande wa magharibi na kaskazini imepakana na Wilaya ya Mvomero.
|