| Utangulizi |
| |
Manispaa ya Morogoro iko umbali wa kilometa 195 kutoka Jiji la Dar es Salaam. Manispaa ya Morogoro inapakana na Milima ya Uluguru kwa upande wa Kusini na Milima ya Mindu upande wa Magharibi. Upande wa Kaskazini inapakana na Wilaya ya Mvomero na upande wa Mashariki Morogoro Vijijini. |
| |
| |
| |
| |
| UMBILE LA ARDHI |
| |
Halmashauri ya Manispaa ina eneo la kilometa za mraba 531 sawa na asilimia 0.73 ya Mkoa wa Morogoro wenye eneo la kilometa za mraba 72,939 . Ipo kati ya Latitudo 4.5 Kusini na Longitudo 37.4 Mashariki. Iko kiasi cha mita 488 kutoka usawa wa bahari.
Hali ya hewa
Ipo misimu miwili ya mvua ambayo ni Mvua za Vuli na Mvua za Masika. Mvua za vuli huanza mwezi Novemba na kuisha mwezi Januari. Wastani wa mvua hizo ni milimeta 400 . Mvua za Masika huanza mwezi Machi na huishia mwezi Mei. Mvua hizo hunyesha kwa wastani wa kati ya milimeta 821 hadi 1,505 . Wastani wa joto ni nyuzi 10 o C hadi 14 0 C wakati wa baridi (Juni – Agosti) na wakati wa joto (Novemba – Desemba) kati ya nyuzi 28 o C hadi 30 o C .
|
| |
| |
| |
| IDADI YA WATU |
| |
Manispaa ya Morogoro imekuwa ikipanuka kwa kasi kutokana na ongezeko la watu. Kwa mujibu wa takwimu ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002, idadi ya watu imeongezeka kutoka 24,999 mwaka 1967 hadi watu 227,921 mwaka 2002. Wastani wa ongezeko la watu kwa mwaka ni asilimia 4.7. Kwa mwaka huu 2008 maoteo ya idadi ya watu ni 284,171 Wanaume ni 142,262 (50.06%) na Wanawake 141,909 (49.94%).
|
| |
| Utawala |
Halmashauri ya Manispaa ina jimbo moja la uchaguzi ambalo ni Morogoro Mjini. Mhe. Prof. Romanus Ishengoma ni Mstahiki Meya wa Manispaa Morogoro
na
Bw. R. S. Ndunguru
ni Mkurugenzi wa Manispaa |
| |
| Sekta ya Kilimo |
| |
Hali ya kilimo msimu 2007/2008 haikuwa nzuri kwani mvua zilinyesha kwa wingi miezi ya Machi na Aprili 2008 na kukatika mwanzoni mwa mwezi Mei, hivyo baadhi ya wakulima walivuna chini ya malengo.
|
| |
| Maeneo ya uzalishaji |
Manispaa imeainisha maeneo maalum ya uzalishaji ambapo: Hekta 1400 za mpunga zilitarajiwa kulimwa kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji maeneo ya Wami Luhindo.( Wilaya ya Mvomero), Hekta 1,200 za mahindi zilitarajiwa kulimwa maeneo ya Kimambira (Wilaya ya Mvomero) kwa ajili ya uzalishaji wa mahindi na mazao mengine kama alizeti na jamii ya mikunde na hekta 650 katika eneo la nguvu kazi Mkundi.
|
|
|
Upatikanaji wa pembejeo. |
Pembejeo za kilimo kwa msimu 2007/2008 zilipatikana kwenye maduka ya pembejeo ikiwa ni pamoja na mbolea, mbegu, na madawa ya kilimo. Aidha wakala 18 walitoa huduma ya uuzaji wa pembejeo ambao kati ya hao 12 waliuza mbolea na mbegu za ruzuku.
|
| |
| Ushirika na Masoko |
| |
Pembejeo za kilimo kwa msimu 2007/2008 zilipatikana kwenye maduka ya pembejeo ikiwa ni pamoja na mbolea, mbegu, na madawa ya kilimo. Aidha wakala 18 walitoa huduma ya uuzaji wa pembejeo ambao kati ya hao 12 waliuza mbolea na mbegu za ruzuku. Kama inavyooneshwa kwenye jedwali lifuatalo |
Na |
Aina ya chama |
Idadi ya vyama |
Me |
Ke |
Jumla ya wanachama |
1 |
Akiba & Mikopo(SACCOS) |
93 |
4162 |
4021 |
8183 |
2 |
Kilimo/Mazao |
8 |
194 |
173 |
367 |
3 |
Viwanda |
3 |
72 |
9 |
81 |
4 |
Wafugaji |
2 |
23 |
21 |
44 |
5 |
Ujenzi & Nyumba |
2 |
56 |
16 |
72 |
6 |
Maduka ya Ushirika |
1 |
- |
50 |
50 |
7 |
Madini |
1 |
10 |
- |
10 |
8 |
Usafirishaji |
1 |
10 |
- |
10 |
9 |
Vyama vingine |
17 |
279 |
28 |
307 |
|
Jumla |
128 |
4806 |
4318 |
9124 |
|
| |
| |
| Elimu |
|
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ina taasisi 167 zinazotoa elimu katika ngazi mbalimbali. ikiwa ni pamoja na elimu ya awali, elimu ya msingi, elimu ya sekondari, elimu ya ualimu, elimu ya ufundi na elimu ya juu
|
Elimu ya Awali
|
Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2005 hadi 2010, kumekuwepo na Maendeleo katika utoaji Elimu ya awali. Idadi ya wanafunzi waliosajiliwa katika elimu ya awali imeongezeka
|
|
Elimu ya Msingi
|
Uandikishaji wa wanafunzi darasa la Kwanza :
Katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM 2002 – 2008), hali ya uandikishaji iliendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka |
| |
Ufaulu Kitaifa mwaka 2007.
Halmashauri ya Manispaa Morogoro ilikuwa ya pili kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2007. Jedwali namba 18 linaonyesha takwimu za wanafunzi waliofaulu kuanzia mwaka 2005 hadi 2007 |
| |
| Elimu ya Sekondari |
Shule za Sekondari za Serikali:
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ina jumla ya shule za Sekondari 34. Kati ya hizo, 20 ni za Serikali. Idadi ya shule za sekondari za serikali imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka. Ongezeko hili la shule za sekondari limesaidia kuwaingiza sekondari watoto wote waliofaulu darasa la saba mwaka 2007. |
| |
| Maji |
Manispaa ya Morogoro ni miongoni mwa Halmashauri zilizo kwenye Mpango wa Kitaifa wa kuboresha huduma ya maji, usafi binafsi na usafi wa mazingira ( National Rural Water and Sanitation Programme ) vijijini kuanzia mwaka wa fedha wa 2007/2008. Katika kipindi hicho Halmashauri ya Manispaa ilipokea kiasi cha Tshs 71.409,000/= kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.Mpango huu unaratibiwa na Wizara ya maji na umwagiliaji na kutekelezwa na Halmashauri kwa kushirikiana na jamii na wadau mbalimbali.
Dhumuni ikiwa ni kuondoa umasikini vijijini kwa kuboresha upatikanaji wa maji safi , salama na ya kutosha.
Halmashauri ya Manispaa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi binafsi, Mamlaka ya Maji Safi na Taka Morogoro, imeweza kuweka kamati za utunzaji Mazingira
|
| |
Upatikanaji wa huduma ya maji
|
Halmashuri ya Manispaa ya Morogoro Kupitia mpango wa kuboresha huduma ya maji, usafi binafsi na usafi wa mazingira ( National Rural Water and Sanitation Programme) vijijini kwa kushirikiana na Jamii inatekeleza miradi kwa Kata za pembezoni. Kuanzia mwaka wa fedha 2007/2008, Halmashuri ya Manispaa kwa kupitia ufadhili wa Benki ya Afrika (ADB) imeweza kutekeleza miradi mikuu matatu ya:
Ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 120,000 lenye uwezo wa kuhudumia wakazi wapatao 7000 katika Kata ya Bigwa na maeneo yaliyo karibu na Kata hiyo. Hadi sasa tanki hilo limegharimu jumla ya Shs.30,106,400.00.
ukarabati wa mfumo wa maji safi na uongezaji wa huduma ya maji kwa shule ya sekondari Kauzeni kata ya Mzinga umegharimu jumla ya Tshs 17,780,000.
ujenzi wa matandao wa maji safi (water distribution system)Katika Mtaa wa Mgambazi kwa ajili ya vitongozi vya Mvule,Gongo na Mbata vikiwa na jumla ya wakazi 414 umegharimu jumla ya Shs 13,180,600.00.
Kwa mitaa ambayo tayari ina miradi ya Maji wameunda Kamati zao za Maji zenye wajumbe wasiozidi kumi na mbili, na zina mifuko ya maji kwa ajili ya kufanyia ukarabati. Mamlaka ya Maji safi na taka Morogoro ndiyo inayohusika na miundo mbinu yote ya maji safi na taka kwa zile Kata zote ambazo zipo katikati ya mji.
Kwa wakazi wa Kata zile ambazo ziko pembezoni mwa Manispaa, uhamasishaji umefanyika kuhusu umuhimu wa kuvuna maji ya mvua. |
| |
|
|
| |
| |
| Afya |
| |
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ina jumla ya vituo 56 vya kutolea huduma za Afya ambavyo vinamilikiwa na taasisi mbalimbali kwa sasa, Halmashauri ya Manispaa haina hospitali yake bali inamiliki vituo vya Afya 3 na Zahanati 9, kati ya zahanati hizi 9, zahanati 4 zinatoa huduma na 5 zinatarajiwa kufunguliwa mwakani. Hata hivyo Halmashauri inatoa shukrani kwa serikali kwa kukubali na kuiruhusu Halmashauri ipanue kituo cha Afya cha Sabasaba kuwa Hospitali ya Wilaya.
Ukarabati wa Vituo vya Afya:
Kwa kutumia Ruzuku ya Ukarabati wa Vituo vya Afya (JRF), kazi ya ukarabati imefanyika katika vituo mbalimbali
Huduma ya Uzazi
Katika kipindi cha kuanzia 2005 hadi 2007 kumekuwepo na mwamko wa akina Mama kujifungulia katika vituo vya huduma ya Afya. Hii ni kutokana na uhamasishaji unaofanywa na watoa huduma katika vituo na katika Jamii.
Usafi wa Mji
Kazi ya uzoaji wa taka zinazozalishwa kila siku umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka ikiwa ni sambamba na ongezeko la vifaa na magari ya kuzolea taka ngumu. Jedwali namba 32 linaloonyesha mtiririko wa uzalishaji taka, uzoaji na vyombo/vifaa vinavyohusika.
|
Hali ya Lishe
Taarifa zinaonyesha kuwa utapiamlo mkuwa kwa sasa ni asilimia 0.2 ambapo mwaka 2005 ilikuwa 0.6 na utapiamlo wa kiasi kwa mwaka 2008 ni wastani wa asilimia 1.2 wakati mwaka 2005 ilikuwa asilimia 7.2
|
|
MMAM
|
Idara ya Afya iliainisha mahitaji ya vituo vya Afya na Zahanati kwa kuzingatia hali halisi ya mazingira ya kimji ambapo mwongozo huu haukuwa wazi moja kwa moja kwa misingi ya idadi ya watu, ukubwa wa maeneo na urahisi, ugumu wa kufikika na upatikanaji wa huduma mbadala za vituo vya kutolea huduma binafsi.
|
Mapambano dhidi ya UKIMWI
|
| |
Manispaa ni miongoni mwa miji iliyo katika njia kuu za usafiri, hivyo kupelekea kuwa eneo la kupitiwa na wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi. Kutokana na hali hii suala la maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya ngono haliepukiki. Halmashauri inaendelea kutoa Elimu kwa Jamii.
Jitihada za kuelimisha jamii zinazofanywa na Halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika yasiyo ya Kiserikali, hali ya kiwango cha maambukizo ya VVU inaendelea kupungua kutoka asilimia 11.5 ya mwaka 2005 hadi asilimia 6.9 ya mwaka 2007. |
| |
| |
| Mifugo |
| |
| |
Migogoro ya wakulima na wafugaji:
Hakuna migogoro kati ya wakulima na wafugaji katika Manispaa ya Morogoro.
Ulaji wa nyama na maziwa:
Katika kipindi cha 2007/08 jumla ya lita 3,342,496 za maziwa zilizalishwa na kilogram 1,506,180 za nyama ziliuzwa katika mabucha mbalimbali yaliyopo katika manispaa.
Mikakati ya Kuondoa Migogoro Kati ya Wakulima na Wafugaji.
Manispaa ya Morogoro huzuia migogoro kati ya wafugaji na wakulima kwa kutowaruhusu wakulima kufanya shughuli za kilimo katika eneo liliotengwa kwa ajili mifugo na malisho. Aidha Manispaa ilitunga sheria ndogo ya ufugaji katika Manispaa ya mwaka 2002.
Mauzo ya mifugo:
Katika Mwaka 2007/08 jumla ya ng'ombe 18,168 waliuzwa kwa wastani wa shilingi 625,000 kwa ng'ombe mmoja. Manispaa ilikusanya ushuru wa shilingi 18,168,000 unaotokana na mauzo ya ngombe hao.
Upatikanaji wa dawa za mifugo:
Katika Manispaa ya Morogoro kuna jumla ya maduka 18 ya dawa za mifugo. Maduka hayo yanamilikiwa na watu binafsi.
Mahitaji ya watalaamu wa mifugo:
Wapo wataalamu 26 wa mifugo ambao kulingana na mahitaji wanatosheleza. |
| |
| Hali ya viwanda |
Katika Manispaa ya Morogoro kuna viwanda mbalimbali vikiwemo viwanda vikubwa 15, viwanda vya kati 4 na viwanda vidogo vidogo 437. Kufuatia sera ya ubinafsishaji baadhi ya viwanda vilivyokuwa chini ya Umma vilibinafsishwa na kupata wawekezaji lakini baadhi havijapata wawekezaji hadi sasa. Angalia jedwali Na. 26, 27, 28, yanaonyesha orodha ya viwanda vilivyopo. Viwanda vidogo vidogo vimeongezeka kutoka 247 mwaka 2005 hadi 437 mwaka 2008 ambayo ni nyongeza ya asilimia 72%.
Matumizi ya Vipimo Halali
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imelipa kipaumbele suala la matumizi ya vipimo halali kutokana na utaratibu uliokuwepo wa wakulima na wateja kupunjwa kwa kutotumika vipimo sahihi. Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa walipewa jukumu la kuhakikisha matumizi ya vipimo halali kwenye maeneo yao kwa kushirikiana na wakala wa vipimo Mkoa wa Morogoro. Matumizi ya Lumbesa, makopo, vibaba na vipimo vingine visivyo sahihi vimepigwa marufuku na uhakiki unaendelea.
Leseni za biashara zilizotolewa
Marekebisho ya sheria ya utoaji wa Leseni za biashara Na. 25 ya mawaka 1972 yaliyofanyika mwaka 2004 yalisaidia utoaji wa leseni mpya za biashara kuongezeka kwa asilimia 16.6%. Kutokana na mabadiliko hayo, leseni hutolewa mara moja tu na hazina muda wa kumalizika ( Expiry date ). Leseni zilizoendelea kutolewa kuanzia muda huo ni mpya tu kwa wale wanaoanza biashara. Idadi ya leseni za biashara 3444 zilitolewa kwa kipindi cha Oktoba 2005 hadi Oktoba 15, 2008.
|
|
| |
| |
| |
| |
| |
|
| |
| |
| |
| |
|