|
||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||
Katika mwaka wa fedha 2008/2009 Mkoa wa Morogoro kupitia Fungu 79 uliidhinishiwa na Bunge kutumia jumla ya fedha za Tanzania shilingi 54,553,902,000/= kwa ajili ya kugharamia Matumizi ya Kawaida kwa watumishi wa Serikali Kuu na Halmashauri za Wilaya na Manispaa Aidha, Mamlaka za Serikali za Mitaa zitatumia shilingi 49,552,583,000/= kati ya fedha hizo shilingi 39,537,810,000/= zitatumika kulipia gharama za mishahara na shilingi 10,014,773,000/= zitatumika kwa ajili ya matumizi mengineyo Katika kipindi cha Julai 2008 hadi Machi 2009, Mkoa wa Morogoro umeshapokea jumla shilling 44,870,532,985/= za Mishahara sawa na asilimia 105.81 ya bajet. Kati ya fedha hizo, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimepokea shilingi 42,166,582,232/= sawa na asilimia106.65 ya bajeti na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imepokea shilingi 2,703,950,752 sawa na asilimia 94.30. Katika kipindi cha January 2009 hadi Machi 2009 jumla shilling 12,948,665,629/= za Mishahara zimepokelewa. Kati ya fedha hizo, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimepokea shilingi 12,490,766,599 na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imepokea shilingi 457,899,030/= Fedha za Matumizi Mengineyo zilizopokelewa katika kipindi cha Julai 2008 hadi Machi 2009 ni shilling 9,493,129,500/= sawa na asilimia 78.14 ya bajet. Kati ya fedha hizo, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimepokea shilingi 7,808,381,500/= sawa na asilimia 77.97 ya bajeti na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imepokea shilingi 1,684,748,000/= sawa na asilimia 78.95. Katika kipindi cha January 2009 hadi Machi 2009 jumla shilling 2,280,871,500/= za Matumizi Mengineyo zimepokelewa. Kati ya fedha hizo, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimepokea shilingi 1,708,379,500/= na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imepokea shilingi 572,492,000/= Aidha Mkoa umeshapokea jumla shilling 13,018,487,356/= .za Maendeleo sawa na asilimia 65.67 ya bajeti. Ambapo kati ya fedha hizo, za Ndani ni Shilingi 2,913,099,000 sawa na asilimia 95.45 ya bajeti na za nje ni Shilingi 10,105,388,356/= sawa na asilimia 60.25 ya bajeti. Katika kipindi cha JanuarI 2009 hadi Machi 2009 jumla shilling 5,735,714,407 za Maendeleo zimepokelewa. Kati ya fedha hizo, za Ndani zilizopokelwa ni Shilingi 698,322,000/= na za Nje ni Shiling 5,037,392,407. Mkoa umetumia jumla shillingi 44,870,532,985/= za Mishahara sawa na asilimia 105.81 ya bajet. Kati ya fedha hizo, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimetumia shilingi 42,166,582,232 sawa na asilimia 106.65 ya bajeti na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imetumia shilingi 2,703,950,752/= sawa na asilimia 94.30 Katika kipindi cha January 2009 hadi Machi 2009 jumla shilling 12,948,665,629/=.za Mishahara zimetumika. Kati ya fedha hizo, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimetumia shilingi 12,490,766,599/=i na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imetumia shilingi 457,899,030. Mkoa umetumia jumla shilling 9,362,538,111/= za Matumizi Mengineyo sawa na asilimia 77.07 ya bajet. Kati ya fedha hizo, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimetumia shilingi 7,808,381,500 sawa na asilimia 77.97 ya bajeti na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imetumia shilingi 1,554,156,611/= sawa na asilimia 72.83 ya bajeti. Katika kipindi cha January 2009 hadi Machi 2009 jumla shilling 2,279,320,241/= za Matumizi Mengineyo zimetumika. Kati ya fedha hizo, Halimashauri za wilya zimetumia shilingi 1,708,379,500/= na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imetumia shilingi 570,940,741/=. Kwa upande wa Fedha za Maendeleo umetumia jumla shilling 11,766,287,606/= sawa na asilimia 72.98 ya bajeti. Kati ya fedha hizo, fedha za Ndani ni shilingi 1,775,899,250/= sawa na asilimia 17.73 ya bajeti na za Nje ni Shilingi 9,990,388,356/= .sawa na asilimia 59.56. Katika kipindi cha Januari 2009 hadi Machi 2009 jumla shilling 5,315,114,657/= .za Maendeleo sawa zimetumika. Kati ya fedha hizo, za ndani ni shilingi 392,722,250/= na za nje ni shilingi 4,922,392,407. Hizi ni fedha zilizopokelewa na kutumika hadi mwezi Machi 2009
|
|
||||||||||||||||||
| Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, TEL: 026 - 2604237/2600973, FAX: 026 2601000 | ||