|
||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||
Sekta hii kama ilivyoanishwa kwenye sera ya elimu ya mwaka 1995 msisitizo umewekwa kwenye elimu ya awali, Msingi,Sekondari na elimu ya juu. Elimu ya AwaliMkoa umepata mafanikio katika elimu ya awali kwa kuwa na madarasa 626 (2008) ukilinganisha na madarasa 326 yaliyokuwepo mwaka 2005. Pia umeandikisha wanafunzi 30,140 (2008) ikilinganishwa na mwaka 2005 ambao walikuwepo wanafunzi 22,971. Jedwali la: Elimu ya Awali
Elimu ya MsingiShule za Msingi zimeongezeka toka 757 mwaka 2005 hadi 814 mwaka 2008 sawa na ongezeko la asilimia 7.5.Hali kadhalika madarasa yameongezeka toka 2,092 mwaka 2005 hadi 4,919 mwaka 2008. Aidha, wanafunzi walioko shule za msingi waliongezeka toka 379,079 mwaka 2005 hadi 435,375 mwaka 2008 sawa na ongezeko la asilimia 14.8. Mafanikio pia yamepatikana baada ya Mkoa kuwa wa 20 kati ya mikoa 21 mwaka 2005 na kufanya vizuri miaka miwili mfululizo ambapo mwaka 2007 umekuwa wa 7 kati ya 21 na mwaka 2008 wa 9 kati ya mikoa 21 Tanzania Bara. Katika ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba. Mdondoko(dropout) umepungua kwa asilimia 52.2 toka wanafunzi 2,022 mwaka 2005 hadi wanafunzi 966 mwaka 2008. Jedwali Na.2: Elimu ya Msingi.
Chanzo: Taarifa za Wilaya 2005-2008 Elimu ya Msingi kwa walioikosa (MEMKWA ). Mkoa umefanikiwa kuanzisha vituo vya MEMKWA 781 mwaka 2008 ukilinganisha na 696 mwaka 2005. Pia umeweza kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 4,926 (2005) hadi 7,080 (2008) na kuwa na walimu 1,562 (2008) ukilinganisha na 1,392 mwaka 2005. Mafanikio haya yanaashiria kuongezeka kwa kiwango cha wanaojua kusoma na kuandika.
Jedwali Na.3: MEMKWA.
Chanzo:Taarifa za Wilaya 2005-2008 2.3. Elimu ya SekondariMwaka 2008 jumla ya wanafunzi 29,995 walifaulu mtihani wa darasa la saba ikilinganishwa na mwaka 2005 ambapo walifaulu wanafunzi 11,669 sawa na ongezeko la asilimia 157.
Idadi ya shule za Sekondari zimeongezeka kutoka shule 58 (2005) hadi 180 (2008). Aidha madarasa yameongezeka kutoka madarasa 418 (2005) hadi 763 (2008), wanafunzi wa sekondari waliongezeka kutoka 23,643 (2005) hadi 39,495 (2008). Mafanikio mengine ni kama yaliyoonyeshwa katika jedwali Na. 4 – elimu ya sekondari. Jedwali Na.4: Elimu ya Sekondari
Chanzo: Elimu taarifa za Wilaya 2005 -2008
|
|
||||||||||||||||||||||||
| Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, TEL: 026 - 2604237/2600973, FAX: 026 2601000 | ||