|
||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||
Maendeleo ya Viwanda Viwanda muhimu vinavyoendelea na uzalishaji ni kama ilivyo katika Jedwali Viwanda vinavyozalisha
Changamoto iliyopo upande wa viwanda ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya Kilimo na Mifugo ili yasindikwe na kuongezwa thamani. Hii ni pamoja na kubaini maeneo mengine ya uanzishaji wa viwanda vingine vidogo na vya kati vyenye kutumia teknolojia rahisi na sahihi ili kusindika mazao ya wakulima na wafugaji kwa lengo la kuongeza thamani ya mazao hayo na kukidhi mahitaji katika soko.. MAENDELEO YA BIASHARA Ofisi za biashara za Halmashauri za Wilaya zinaendelea kutoa leseni za biashara, kukagua leseni za biashara na kutoa ushauri kwa wafanyabiashara. Aidha, kitengo cha Mizani na Vipimo kinaendelea na ukaguzi wa vipimo na mizani kwa lengo la kudhibiti uhalali wa vipimo pamoja na kukusanya maduhuri ya Serikali. Wafanyabiashara wameshauriwa ili waweze kuimarisha jumuiya zao hususan Taasisi ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Wakulima Tanzania (TCCIA) kwa lengo la kuipa sekta binafsi nguvu na uwezo zaidi wa kumiliki uchumi. Changamoto iliyopo upande wa Biashara ni kuwakomboa wananchi wa Mkoa hasa wakulima na wafugaji kwa kuwapa elimu ya biashara ili waweze kuchambua na kuchanganua gharama za miradi wanayoianzisha na kuiendeleza. Mtazamo mkubwa wa mafunzo hayo ya ujasiriamali ni katika: Kubuni miradi inayofaa kulingana na mahali na wakati. Utunzaji wa kumbukumbu sahihi za biashara. Kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba. Kufanya tathmini ya mara kwa mara kuhusu uendeshaji wa biashara. Kukuza mitaji ya biashara kwa njia ya mikopo kwa kuzingatia kukopa kwa busara. Usimamizi bora wa biashara. Kuendesha biashara katika mfumo rasmi na uwazi ili kuiwezesha Serikali kupima pato halisi la Taifa.
Suala la utoaji wa elimu ya ujasiriamali kwa wananchi ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2005 inayohimiza kuongeza uzalishaji, kuongeza tija na kuongeza pato.
MAENDELEO YA MASOKO Uzalishaji unakamilika na unakuwa wenye manufaa endapo kilichozalishwa kinauzika. Umuhimu wa masoko ni kumkomboa mzalishaji hasa mkulima mdogo. Hali ilivyo ni kwamba hakuna masoko mengi ya uhakika ya kuuzia mazao na wakulima wengi hawatafuti soko kabla ya kulima Aidha, kuna ubovu wa miundombinu ya barabara Vijijini. Tatizo la uwazi wa bei na kutokutumia mizani bora wakati wa kuuza mazao pia linawakabili wazalishaji na wauzaji wa mazao ya kilimo. Vile vile kuna ukosefu wa mawasiliano na masoko mengine ili kujua bei za mazao kwenye masoko hayo. Changamoto iliyopo ni kuanzisha na kuendeleza masoko na magulio ya wakulima yenye kutumia mizani bora ili kunusuru mkulima kupunjwa njia ya “lumbesa”. Masoko bora ya mazao ya kilimo yaliyopo ni Mgeta na Nyandira Wilayani Mvomero, pamoja na Tandai, Tawa na Kinole Wilayani Morogoro. Wilaya za Ulanga, Kilombero na Kilosa zimejiwekea malengo ya kuanzisha masoko bora ya mazao ya kilimo. Mkoa una fursa za masoko ndani ya Mkoa, nje ya Mkoa – Kitaifa, na kimataifa mathalani soko la Umoja wa Falme za Kiarabu, Soko la Marekani, Soko la Umoja wa Nchi za Ulaya, Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Soko la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika. Mkoa una jumla ya Masoko rasmi 69 kama ilivyokatika Jedwali Jedwali Masoko rasmi
Changamoto nyingine ni kuzalisha bidhaa zenye kiwango cha ubora wa juu zenye vifungashio bora vyenye kuvutia na zinazoweza kupatikana kwa uhakika kwa kuzingatia mtazamo wa kibiashara wa kuzalisha kinachohitajika badala ya kuuza kinachozalishwa. Kuwepo kwa watu 2,021,714 Mkoani ni fursa nzuri ya soko ndani ya Mkoa endapo watahamasishwa kununua bidhaa zinazozalishwa Mkoani Hili litawezekana endapo matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika biashara yatazingatiwa ili kutoa habari za masoko na biashara. Vyombo hivyo vya kupashana habari ni pamoja na Luninga (TV) za Wilaya, Redio, Magazeti, Simu na Mtandao wa Kompyuta (Tovuti).
|
|
||||||||||||||||||||||||
| Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, TEL: 026 - 2604237/2600973, FAX: 026 2601000 | ||