|
||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||
Mtandao wa barabara za MkoaMkoa wa Morogoro una mtandao wa barabara zenye jumla ya urefu wa km.3, 000,kati ya hizo km.1,627.92 ziko chini ya TANROAD na km.1,372.08 ziko chini ya Halmashauri za Wilaya na Manispaa. Jedwali la Barabara za Mkoa wa Morogoro.
Chanzo: Wakala wa Barabara Mkoa ,2008. 11.2 Mafanikio ya matengenezo ya barabara Mkoani ni kama ifuatavyo:Barabara ya Mziha – Magole – Kilosa hadi Mikumi Serikali imepania kujenga barabara ya lami kati ya Mziha – Magole – Kilosa – Mikumi na hadi sasa upembuzi yakinifu umekamilika na barabara hiyo kuimarishwa ili iwekwe lami. Serikali inaendelea na juhudi za kuhakikisha barabara hiyo inawekwa lami. Barabara ya Ifakara – Taweta Sehemu ya barabara ya Mpanga - Taweta yenye urefu wa km 34 ilifunguliwa mwaka 2006/2007; baada ya matengenezo makubwa Barabara ya Mvomero – Ndole (Maskati Jct) – Kibati – Lusanga Barabara hii imekwisha tengenezwa katika sehemu korofi za Matale hadi Ndole na kupitika kwa mwaka mzima. Usanifu wa Daraja la Mwere/DDC Usanifu wa Daraja la Mwere/DDC umefanywa na TanRoads ili kupunguza msongamano wa magari yanayotoka katikati ya mji kuelekea posta. Mkoa unatafuta fedha za ujenzi wa daraja hili. Daraja la Mto Kilombero Upembuzi yakinifu na usanifu wa awali wa daraja la mto Kilombero umekamilika ili kujenga daraja hilo. Hatua za maandalizi ili ujenzi uanze zinaendelea. Daraja la Mto Sagamaganga Daraja limejengwa na kukamilika hivyo kuwaondolea kero wananchi wa Wilaya ya Kilombero na Uranga. Daraja la Mto Mwatisi Usanifu wa daraja hili umekamilika na hatua za kukamilisha ujenzi zinaendelea. Barabara ya Ifakara Mjini Ujenzi wa Km 7 za barabara ya Ifakara mjini kwa kiwango cha Lami umekamilika na hivyo kuboresha usafiri na maisha ya wananchi. 12.0. UJENZI WA MAJENGO YA SERIKALIUkarabati umefanyika kwa nyumba za Wakuu wa Wilaya Ulanga, Kilosa na Kilombero; na nyumba ya Katibu Tawala Wilaya Ulanga.Ujenzi wa jengo na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mvomero upo katika hatua za mwisho ( finishing ). Nyumba ya Mkuu wa Wilaya Mvomero inaendelea kujengwa Pia jengo la ofisi na nyumba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Mvomero. Watumishi wa Ulanga wamejengewa nyumba mpya na ukumbi wa Mikutano na ujenzi unaendelea.Ukarabati wa jengo Kongwe Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Awamu ya Kwanza imekamilika na jitihada zinaendelea za kukamilisha ujenzi huo.
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||
| Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, TEL: 026 - 2604237/2600973, FAX: 026 2601000 | ||