|
||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||
Wataalam wa Korea wakiongozwa na Mwakilishi mkazi wa wa shirika la ushirikiano la Korea (KOICA) bwana Holywater HO. Wengine aliofuatana nao ni Lee Kyong Koo, Lee Jin Woong, Lee Man Hom na Dr Lee Woo-Gun. Wataalam hao walikuwa na ziara ya siku 4 kuanzia tarehe 8-11/3/2010 na walitembelea eneo la Pangawe, Kiroka na Kibwaya ambayo ni maeneo yaliyopendekezwa katika mradi mpya wa Morogoro Integrated Community Development Project. Wataalam hao pia walitembelea maeneo ya Dakawa, Mkindo n Turiani wilayani Mvomero ambayo ni maeneo yalitopata ufadhili wa zana za kilimo kutoka Korea siku zilizopita. Katika majumuisho siku ya mwisho walifanya kikao na viongozi wa mkoa wa Morogoro wakiongozwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa Mhe Halima Dendego na viongozi wa Wilaya ya Morogoro ambapo ujumbe kutoka Korea walifurahishwa sana na ziara hii na wakaahidi kuwa mradi uliopendekezwa utapata ufadhili ingawa walisema kuwa wataanza na kijiji cha Pangawe ambapo watafadhili mradi wa umwagiliaji, ujenzi wa shule ya msingi, barabara na zahanati. Kiasi cha fedha kitajulikana baadaye. Vijiji vinavyofuata vitafadhiliwa baadaye.
|
|
||||||||||||||||||||||||
| Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, TEL: 023 - 2604237/2600973, FAX: 023 2601000 | ||