JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
     
 
     
MOROGORO
 
[ Nyumbani ]
 

Mkoa wa Morogoro umepewa changamoto ya kuhakikisha kwamba unakuwa Ghala la Taifa kupitia agizo lako Mhe. Rais ulilolitoa tarehe 10/6/2006 ulipotembelea Mkoa wa Morogoro kuwashukuru wananchi baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005

Katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mpango huu, jumla ya shilingi 5,772,852,426/- (sawa na asilimia 13.8) zilitolewa kati ya lengo la shilingi 41,726,500,111/=. Katika awamu ya pili ya utekelezaji mwaka 2008/09 – 2009/10 gharama zilizokadiriwa ni shilingi 58,455,110,251/= ili kuongeza eneo la umwagiliaji kufikia hekta 18,321 toka hekta 8,804 za mwaka 2008. Lengo ni kufikia hekta 53,076 za mazao ya chakula na biashara.

Mpango Mkakati wa Fanya Morogoro Ghala la Taifa (FAMOGATA)

umeandaliwa . Utekelezaji wa mkakati huu una malengo yafuatayo:

• i. Uboreshaji wa Miundombinu, Usafirishaji na Mawasiliano.

• ii. Kuongeza ufahamu, stadi na matumizi ya teknolojia kama vile matumizi ya matrekta makubwa, madogo, pikipiki na wanyamakazi.

• iii. Kumuwezesha mkulima kupata bei nzuri ya mazao katika soko la nje na ndani.

• iv. Kuongeza thamani ya mazao kwa njia ya usindikaji na biashara za kilimo.

Ili kutekeleza Mpango wa FAMOGATA kwa ufanisi, hatua zilizofikiwa ni pamoja

na:-

•  Kuainishwa kwa maeneo ya uzalishaji katika kila Wilaya na mazao yanayotakiwa kulimwa. Ni mategemeo ya Mkoa kuona kwamba eneo la hekta 114,700 linaendelezwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ifikapo mwaka 2015 ikilinganishwa na eneo linalotumika la hekta 8,804

•  Upatikanaji wa pembejeo za kilimo (mbolea, zana, mbegu bora, n.k). Mkoa ulihitaji tani 12,366 za mbolea na tani 3,854.7 za mbegu bora. Mgao wa mbolea iliopatikana ni tani 5,904 na mbegu bora tani 77. Kiasi cha mbolea kilichosambazwa ni tani 3,285 na mbegu tani 67.3.

•  Katika jitihada za kutekeleza Mapinduzi ya kijani kama nia ya kutekeleza Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) zana bora za kilimo hazina budi kutumika.

•  Ili kuhakikisha kuwa zana za kilimo yakiwemo matrekta makubwa na madogo yanapatikana, Uongozi wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri unasisitiza kupanua wigo wa matumizi ya matrekta makubwa na madogo (Power Tillers) pikipiki na wanyama kazi wa kukokota majembe ya kulimia kama njia mbadala ya kuachana na kilimo cha mazoea cha jembe la mkono.

•  Kampuni ya DEMACO kwa kushirikiana na Kampuni ya Africatic imeshafikisha matrekta 12 kati ya mahitaji ya matrekta 200 waliyoingia mkataba wa kuyaleta nchini.

•  Mradi wa Participatory Agriculture Development and Empowrment Projects kuendeleza Sekta ya Kilimo (PADEP) umewawezesha wakulima wa vijiji vya Kalengakero,Mwaya na Kipenyo kununua matrekta matatu katika Wilaya ya Ulanga.

Aidha jumla ya matrekta 80 yalipelekwa Wilayani Ulanga yakitokea eneo la Kibaigwa Wilayani Kongwa katika msimu wa 2007/2008 ili kuitikia wito uliotolewa na Wilaya wa mahitaji ya matreka katika Wilaya hiyo.

•  Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri na Sekta binafsi hadi kufikia mwezi Agosti, 2008 umewezesha ununuzi wa matrekta 58 kati ya mahitaji ya trekta 790.Matrekta 12 aina ya ya Catic yalikabidhiwa kupitia Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo vilivyokopeshwa na Federal Bank of Middle East , tarehe 12 Julai, 2008 kwa Udhamini wa Private Agriculture Sector Support (PASS). Benki hiyo inatarajia kukopesha matrekta 112 ifikapo mwezi Desemba, 2008 kati ya trekta 200 yatakayouzwa na kampuni ya AFRICATIC Mkoani.

•  Katika msimu wa 2007/2008 Mfuko wa Pembejeo wa Kilimo ulisaidia kutoa mikopo Mkoani kwa ajili ya kununulia matrekta 17 pamoja na majembe yake kwa gharama ya sh.559,500,000/= kama ifuatavyo;-

•  Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imepata sh.189,500,000/= za kununua matrekta sita.

•  Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero imepata sh.160,000,000/= za kununua matrekta matano.

•  Halmashauri ya Manispaa imepata sh.35,000,000/= za kununulia tekta moja

•  Halmashauri ya Kilosa imepata sh.175,000,000/= za kununua matrekta matano.

•  Kati ya matrekta 58, matrekta 30 yamenunuliwa kwa mikopo kupitia Taasisi za Fedha na Serikali kama ifuatavyo:-

•  Kikundi cha Mshikamano kilichopo Tarafa ya Gairo Wilaya ya Kilosa wamenunua matrekta 7.

•  Watu binafsi wamenunua matrekta kumi katika vijiji vya Kidodi,Mbigiri,Ilonga,Ukwamani Gairo na Kimamba Wilayani Kilosa

•  Matrekta matano yamenunuliwa na watu binafsi katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro katika vijiji vya Mikese, Pangawe, Mkambarani, Duthumi na Ngerengere.

•  Watu binafsi wamenunua matrekta manne Wilayani Ulanga katika vijiji vya Iragua, Lupiro na Itete.

•  Matrekta matatu yamenunuliwa na watu binafsi katika vijiji vya Chanzuru, Kimamba na Kilangali Wilayani Kilosa.

•  Matrekta madogo (Power tillers) manne yamenunuliwa na kikundi cha Mshikamano katika Kata ya Rudewa Wilayani Kilosa kwa kukopeshwa na Asasi ya Wanawake iitwayo Women and Poverty Alleviation in Tanzania (WOPATA)

•  Pikipiki 65 zimenunuliwa Wilaya ya Kilosa kwa ajili ya watumishi wa ugani.

Ili kuhakikisha kuwa mazao yanayozalishwa Mkoani yanajulikana kwa wingi pamoja na thamani yake, Mkoa kwa kushirikiana na Meneja wa Vipimo Mkoa unatilia mkazo zaidi matumizi sahihi ya vipimo (mizani) katika kuuza na kununua mazao kwa kuzingatia Sheria Na.20 ya Vipimo ya mwaka 1982, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku suala la lumbesa.

Aidha, Mkoa kwa kushirikiana na Ofisi Kuu ya Wakala wa Takwimu Taifa (NBS), unaandaa utaratibu utakaowezesha kupatikana Freight Indicators ili kubaini kiasi halisi cha mazao yanayosafirishwa kwenda nje ya Mkoa kwa kutumia vituo vya masoko vilivyopo.

 

•  Utekelezaji wa Malengo ya Kilimo na Hali ya chakula 2007/2008

Katika msimu wa 2007/2008 malengo yalikuwa kulima hekta 637,438 zikiwemo hekta 562,617 za mazao ya chakula na hekta 74,821 za mazao ya biashara ili kuvuna tani 1,829,920 za chakula na tani 841,488 za mazao ya biashara.

Katika utekelezaji jumla ya hekta zilizolimwa za mazao ya chakula ni 404,612 na kiasi kilichovunwa ni tani 1,117,573. Aidha, kwa upande wa mazao ya biashara zililimwa jumla ya hekta 50,584 na kuvuna tani 842,803. Kwa ujumla hali ya chakula msimu wa 2007/2008 ilikuwa si nzuri kulinganisha na msimu uliopita kutokana na mvua za vuli kutonyesha kwa wakati na ziliponyesha hazikuwa na mtawanyiko mzuri.

Mwenendo huo ulisababisha maeneo kadhaa Mkoani kupata upungufu

wa chakula kama ifuatavyo:-

Wilaya ya Mvomero vijiji 70, Ulanga vijiji 12, na Morogoro kijiji 1. Vijiji vilivyokuwa na hali mbaya sana ni Melela na Kibati katika Wilaya ya Mvomero, Ketaketa na Luhombero katika Wilaya ya Ulanga na Mkono wa Mara katika Wilaya ya Morogoro.

Malengo ya Kilimo 2008/2009

Uwekaji wa malengo ya kilimo msimu wa 2008/2009 ulizingatia kuwa kila kaya

iwe na ekari zisizopungua tano (5) zikiwemo mbili za mazao ya chakula, moja (1) zao la mhogo na ekari mbili (2) za mazao ya biashara.

Katika msimu wa 2008/2009 Mkoa unalenga kulima jumla ya hekta 594,952.4 za mazao ya chakula ili kuvuna tani 2,120,613.7 na kwa upande wa mazao ya biashara lengo ni kulima hekta 94,339.4 ili kuvuna tani 1,650,463.3

Mikakati ya kufikia malengo hayo ni pamoja na:-

i) Kupima vijiji ili kutenga maeneo ya matumizi bora ya ardhi na kuyamilikisha.

ii) Kuhamasisha wananchi kulima ekari mbili za zao la chakula, mbili mazao ya biashara na moja zao linalostahimili ukame.

•  Kuhamasisha kilimo cha kutumia wanyama kazi na uingizaji wa matrekta ya bei nafuu.

•  Kuelimisha wananchi kuwekeza katika vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) ili kupata mitaji ya kuzalisha katika kilimo.

 

Uongezaji wa thamani ya mazao

Kwa kutambua tatizo la masoko ya uhakika kwa ajili ya matunda yanayozalishwa na wananchi Mkoa ulifanya uhamasishaji na kufanikiwa kuvutia mwekezaji aliyeanzisha kiwanda cha kusindika matunda cha Unnat, chenye uwezo wa kutoa ajira kwa watu 80. Kwa mwaka wa kwanza kiwanda hiki kitanunua matunda tani 20,000.

Kiasi hiki kitakuwa kinaongezeka mwaka hadi mwaka na hadi kufikia mwaka wa tatu kitanunua tani 25,000. Kuanzishwa kwa kiwanda hiki imekuwa ni changamoto kwa wananchi wetu ili waweze kuongeza uzalishaji wa matunda na endapo kiasi cha matunda yanayozalishwa Mkoani Morogoro kitashindwa kukidhi mahitaji, basi kiasi kingine kitanunuliwa kutoka Mikoa ya jirani.

Mashine ya kukoboa mpunga ya Chama cha ushirika cha Akiba na Mikopo cha Walimu Ulanga kilichopo Lupiro Wilayani Ulanga kinafanya kazi na kinakoboa mpunga tani 30 kwa siku na kupangamchele katika madaraja manne ( grading )

 

.Katika kukabiliana na changamoto ya wananchi kutegemea mazao ya chakula kwa ajili ya biashara, Mkoa umeandaa rasimu ya Mpango Maalum wa Uzalishaji Chakula, Biashara na Masoko kwa mwaka 2006/2007 – 2008/2009 ili kutoa elimu na hamasa kwa wananchi katika kujiletea maendeleo yao wenyewe. Mpango huu umeandaliwa kwa kutilia maanani utekelezaji wa agizo lako Mhe. Rais la kuufanya Mkoa wa Morogoro kuwa Ghala la Taifa. Mkoa umetoa elimu ya kilimo bora kwa wananchi kupitia magari ya sinema na vipeperushi mwaka 2006, 2007 na 2008. Magari maalumu yalipatikana kutoka Wizara ya Kilimo na Ushirika na Wizara ya Maliasili na Utalii.

 

Kwa mwaka 2008 Mkoa umepata gari moja la sinema la uhamasishaji masuala ya UKIMWI kutoka Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS). Pamoja na kutoa elimu ya janga la UKIMWI gari hilo pia litatumika katika kuhamasisha masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni njia mojawapo ya kumuongezea mwananchi kipato.

 

Mbolea na mbegu ya Ruzuku

Ili kuongeza tija katika uzalishaji, katika msimu wa 2007/2008 Mkoa ulipata mgao wa tani 5,904 za mbolea ya ruzuku na Mbolea iliyosambazwa ni tani 3,285.

Kampuni ya Mohamed Enterprises pamoja na Minjingu Mine & Fertilizer Ltd hazikufikisha mbolea Mkoani kama walivyokubali walipoingia mkataba kutokana na kuchelewa kuandaa mbolea ya chenga kabla ya msimu wa kupanda.

Ili kuhakikisha kwamba pembejeo za kilimo zinapatikana kwa wakati na kwa bei nafuu, Serikali imetoa mafunzo kwa mawakala wa pembejeo ili waweze kuwa viungo kati ya wauzaji wakubwa/viwanda vya mbolea na wakulima.Wataalamu walipelekwa Wilayani ili kuwatambua mawakala waliopo.

 

Aidha, kuna utaratibu mpya wa kutoa ruzuku ya pembejeo kwa kutumia vocha.Tarehe 19 Julai,2008 kulifanyika uzinduzi wa matumizi ya vocha kitaifa katika kijiji cha Mkula Wilayani Kilombero. Uzinduzi huo ulifanywa na Mhe.Stephen Masatu Wassira (Mb) Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika. Mkoa ulipata mgao wa tani 77 za mbegu bora ya mahindi na tani 67.3 ziliuzwa.

Kilimo cha Umwagiliaji

Mkoa una eneo la hekta 123,507 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Eneo linalotumika kwa sasa ni hekta 8,804 tu.Lengo ni kufikia hekta 53,076 ifikapo 2010.

 

Huduma za Ugani

Mkoa una Kata 141 na mahitaji ya wataalamu wa Ugani katika ngazi hiyo ni 560. Wataalamu wa Ugani waliopo ni 453, hivyo upo upungufu wa Wagani 107 ambao wanatakiwa kuajiriwa ifikapo mwaka 2010. Halmashauri zinafanya utaratibu wa kuomba kuwaajiri wataalamu hao.

Katika harakati za kuboresha huduma za ugani, baadhi ya Wilaya zimeandaa mpango wa kujenga nyumba za watumishi, kununua vyombo vya usafiri na vivunge (extension kits).

 Utekelezaji miradi ya kilimo

Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Kilimo (ASDP) ulianza kutekelezwa Mkoani 2005/2006. Katika kipindi cha mwaka 2007/08 kulikuwa na Miradi 424 chini ya Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADPs) iliyotekelezwa yenye thamani ya sh. 5,772,852,426/=. Miradi hiyo iliibuliwa kutokana na matakwa ya wananchi wa maeneo husika kupitia zoezi la Mpango Shirikishi wa Fursa na Vikwazo (O&OD). Mipango hiyo inalenga kufikia lengo la kuinua kilimo kufikia asilimia 6 ifikapo mwaka 2010. Katika mwaka 2008/09 zaidi ya sh.4,026,309,000/= zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kilimo katika Mkoa wa Morogoro.

Mradi wa Ushirikishwaji Jamii na Uwezeshaji (PADEP ) unatekelezwa katika Wilaya za Ulanga, Kilombero, Morogoro na Mvomero. Mradi huu unawashirikisha wakulima katika kuibua miradi, nao huchangia asilimia 20 katika miradi ya jamii na asilimia 50 ya gharama za miradi ya vikundi.

Hadi mwaka 2008 ipo miradi 41 ya jamii katika ngazi tofauti za utekelezaji yenye thamani ya sh. 1,879,801,906/=. Miradi ya vikundi ipo 154 katika vijiji 37 yenye thamani ya sh. 573,378,387/=. Lengo ni kufikia vijiji 90.

 

 

         
 
[ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, TEL: 026 - 2604237/2600973, FAX: 026 2601000